Risala uzinduzi wiki ya maji bunda by Eng Deule Tanu
1. Risala ya Uzinduzi wa Wiki ya Maji Wilayani Bunda
iliyosomwa na Eng. Tanu Deule, Mhandisi wa maji wa wilaya
ya Bunda kwenye Tengi la Maji la Mlima Kaswaka
Bunda Mjini
Tarehe 17 - Machi - 2011
Mh. Mgeni Rasmi (Mkuu wa Wilaya ya Bunda)
Wah. Viongozi mliofika hapa (Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Bunda)
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Bunda
Wafanyakazi wenzangu wa Idara ya Maji kwa ujumla wenu
Wafanyakazi wa Halmashauri yetu mliofika hapa kuungana nasi
Ndugu zetu waandishi wa habari
Ndugu Wananchi
Mabibi na mabwana
Tumsifu Yesu Kristo
Asalaam Aleykum
Bwana asifiwe
Kabla ya yote napenda kumshukuru mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa
kutujalia uzima na leo tupo hapa
Mh. Mgeni Rasmi
Leo Halmashauri yetu inaungana na taifa zima kuadhimisha wiki ya maji ambayo
imezinduliwa rasmi na Waziri wa Maji Mh. Prof Mark Mwandosya (MB) kwenye
viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza jana tarehe 16/3/2011. Wiki hii ya maji
itahitimishwa tarehe 22/3/2011 ambayo ni siku ya Maji kidunia yaani World Water Day.
2. Maadhimisho haya ya wiki ya maji ni ya 23 tangu yaanze kufanyika kitaifa mwaka 1988
na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Maji kwaajili ya Miji: kukabiliana na changamoto
mbalimbali Mijini”
Mh. Mgeni Rasmi
Miji inayotajwa kwenye kauli mbiu ya mwaka huu ni pamoja na mji wa Bunda. Na hii
ndiyo maana Halmashauri yetu ya Wilaya Ikaonelea kuwa ni vema uzinduzi huu wa
wiki ya maji kiwilaya ufanyike ndani ya viunga hivi vya Mjini na hasa kwenye mradi
mpya wa maji Bunda Mjini.
Mh. Mgeni Rasmi
Kuhusu chombo chenye mamlaka ya kutoa huduma ya maji Bunda mjini
Jukumu la utoaji huduma ya maji hapa Mjini, limekasimiwa kwa Mamlaka ya maji
Bunda mjini yaani Bunda Water Supply Authority. Hii ni Mamlaka kamili
iliyoanzishwa tarehe 21/6/2002 baada ya kutangazwa kwenye gazeti la serikali. Bodi
yake ya kwanza ilianza kutenda kazi tarehe 1Juni 2003 na hivi sasa kuna Bodi ya 3
iliyoteuliwa rasmi tarehe 10 januari mwaka huu wa 2011.
Mh. Mgeni Rasmi
Kuhusu huduma ya maji hapa mjini.
• Kiwango cha maji yanayozalishwa kwa siku yameongezeka kutoka lita 720,000
mwaka 2006 hadi liata 1,260,000 mwaka 2010
• Wateja wameongezeka kutoka 650 mwaka 2006 hadi wateja1,227 mwaka 2010
• Wastani wa watu wenye maji ya bomba wameongezeka kutoka asilimia 15.4 mwaka
2006 hadi asilimia 27.4 mwaka 2010
Mh. Mgeni Rasmi
Kuhusu mradi Mpya wa Maji Bunda Mjini
2
3. Takwimu iliyoonyeshwa hapo juu kwamba katika watu 100 ni watu 27 tu ndo
wanapata maji ya bomba inadhihirisha ukubwa wa tatizo lililopo na kwamba
changamoto hii ni kubwa sana kwetu. Hivyo basi, Halmashauri kwa kushirikiana na
Wizara ya Maji na kwa Msukumo wa pekee wa mheshimiwa Mbunge wa jimbo la
Bunda, Mh. Stephen M. Wasira (MB) na Waziri wa nchi ofisi ya raisi –Mawasiliano na
Uratibu, tumeanza kutekeleza mradi mpya wa maji hapa Bunda mjini utakaokuwa na
chanzo chake kwenye kijiji cha Nyabehu kilichopo umbali wa kilomita 26 kutoka hapa
mjini.
Mradi huu ni mkubwa sana ukiangalia gharama zake hadi hapo utakapo kamilika, na
utaona kuwa umekuwa ukitengewa fedha kidogo hadi kupelekea utekelezwe kwa
awamu kadiri fedha zilivyokuwa zinapatikana, kwani kusubiri fedha hadi zitimie zote
ndiyo mradi uanze kujengwa haukuonekana kuwa ni uamuzi mzuri.
Kwa fedha zilizokuwa zinapatikana, mradi huu umetekelezwa kama ifuatavyo;
Awamu ya I: Zimenunuliwa pampu mpya 9 za kusukuma maji na tayari zipo hapa
Wilayani Bunda zimetunzwa kwenye Bohari yetu
Awamu ya II: Umefanyika ujenzi wa
i. Tengi la maji Migungani lenye ujazo wa lita 225,000
ii. Tengi la kwenye Mlima Kaswaka lenye ujazo wa lita 675,000
iii. Nyumba ya kufunga pampu (Pump House)
iv. Nyumba ya wahudumu wa pamp (pump attendant house) na choo yake
v. Barabara ya kwenda kwenye tengi la maji kwenye Mlima Kaswaka
Awamu ya II: Awamu hii bado haijatekelezwa lakini itahusisha kazi zifuatazo
• Ujenzi wa chujio (treatment plant)
• Kununua na kulaza mabomba ya bomba kuu kilometa 26
• Kusimika pampu
3
4. • Kuingiza umeme wenye msongo mkubwa, na
• Kusuka mtandao mpya wa usambazaji maji hapa mjini
Mh. Mgeni Rasmi
Awamu hii ya tatu ndiyo awamu inayohitaji fedha nyingi zaidi kuliko awamu
zilizopita. Makisio ya awali yanaonesha kuwa zitahitajika zaidi ya shilingi billion kumi
(10Billions) kukamilisha mradi huu kiasi ambacho ni kikubwa ukilinganisha na
takribani billion moja ambayo imekwishatumika kwa awamu ya I na awamu ya II.
Habari njema ni kwamba, mradi huu sasa utatengewa bajeti kubwa kwenye mwaka wa
fedha wa 2011/2012 ili ukamilike. Hii pia imepewa uzito na kauli ya Mh Waziri wa Maji
Jana tarehe 16/3/2011 kwenye uzinduzi wa wiki ya maji pale alipo thibitishia umma
kwa kusema, nanukuuu “ sasa tumedhamiria kuukamilisha mradi wa Bunda na
tutaukamilisha” mwisho wa kunukuu.
Hata hivyo mheshimiwa mgeni rasmi kazi za awali za maandalizi ya awamu hii ya tatu
zimeshaanza kufanyika kwani mhandisi mshauri ameshapatikana na anafanya kazi ya
kuandaa zabuni za ujenzi wa chujio, zabuni za ununuzi na utandazaji wa mabomba ya
maji, na anaandaa zabuni za uwekaji umeme wa msongo mkubwa na usimikaji wa
mitambo.
Mradi huu kwa ujumla unasimamiwa na Mamlaka ya Maji taka na Maji Safi Musoma
kwaniaba ya Wizara ya Maji na kwa upande wa Halmashauri wapo Mamlaka ya Maji
ya Bunda.
Mh. Mgeni Rasmi
Shughuli za awamu ya II ya mradi ambazo pamoja na kazi zingine ilihusisha ujenzi wa
tengi hili hapa tulipo kwenye Mlima Kaswaka, umechukua mwaka mmoja kutoka
tarehe 18/1/2009 hadi tarehe 31/12/2009 kwa gharamu ya Tsh. 226,567,000. Tengi
limejengwa kwa zege kali na nondo imara na limejengwa juu ya mwamba wa mawe ili
4
5. kuwa imara muda wote. Tengi limejengwa na mkadarasi wa daraja la juu kabisa na
amelijengwa kwa kiwango bora kabisa na limejazwa maji na halivuji maji.
Naomba kurudia eneo hilo kwamba tengi letu ni imara wala halivuji maji na hivi sasa
lina maji yamo ndani ya tengi yamejaa na hayavuji hata kidogo.
Mh. Mgeni Rasmi
Pamoja na jitahada hizo zote hapo juu lakini Mamlaka ya Maji inachangamoto
mbalilmbali ambazo inakabiliana nazo, changamoto hizi ni;
i. Miundimbinu ya maji inahujumiwa kwa bomba kutobolewa na wafugaji wa
vijiji vya Guta, Tairo na Migungani
ii. Uchakavu wa miundombinu ya maji hasa mabomba na mitambo
iii. Kukatika nishati ya umeme mara kwa mara kumesababisha kuunguza pampu
zetu za maji na vifaa vyake
iv. Watumiaji maji kutolipa Ankara zao za maji kwa wakati
v. Maji yanayosukumwa kutokidhi mahitaji ya jamii
vi. Ukosefu wa fedha za kulipia Billi ya Umeme kwani ruzuku mara inakuja
kidogo au miezi mingine ruzuku haiji kabisa na TANESCO hutishia kwa kutoa
masaa 48 kuwa wasipolipwa bili yao watakata umeme kwenye mitambo yetu
ya maji bila kujali kuwa Hospitali yetu ya wilaya (DDH) nayo itakosa maji
ikiwa ni pamoja na wao wenyewe TANESCO watakosa maji
Hata hivyo Mamlaka ya maji Bunda ina mikakati kadhaa ili kukabiliana na changamoto
hizi. Mikakati yenyewe ni pamoja na;
• Ukamilshaji wa mradi mpya wa maji wenye chanzo chake Nyabehu
• Kuendelea ukarabati wa miundombinu ya maji kwa kutumia fedha kidogo
tunazokusanya kwa wateja kila mwezi
5
6. • Ofisi ya Mkuu wa wilaya kusaidia namna ya kudhibiti hujuma na kwa
Kutumia vyombo vya dola kama vile Mahakama, Polisi na serikali za Vijiji
kusaidia kudhibiti hujuma dhidi ya miundombinu yetu
• Kuendelea kuiomba serikali kutoa fedha za ruzuku kwa wakati kama ilivyo
kwenye bajeti ili shughuli zisikwame
Mh. Mgeni Rasmi
Hitimisho
Tunapenda kutoa rai kwa watumiaji maji kulipia Ankara zao za maji kwa wakati na
kuwaasa waepukane na utumiaji wa maji salama kwa Bustani, kuoshea magari n.k Pia
wasikubali kuchepusha maji yasipite kwenye mita kwani kwa kufanya hivyo ni kosa la
jinai na wanaweza kushitakiwa kwa mjibu wa sheria. Wananchi waisaidie Mamlaka
yao kufichua waovu wanaoihujumu Mamlaka isisonge mbele.
Mh. Mgeni Rasmi
Napenda pia kutumia nafasi hii kukushukuru wewe binafsi kwa kukubali mwaliko
wetu na kuwa nasi hapa leo. Pili niwashukuru kwa namna ya pekee wenzetu wa
Mamlaka ya Maji Bunda kwa kufanikisha shughuli hii ya uzindizi wa wiki ya Maji
hapa wilayani kwetu Bunda. Niwashukuru watumishi wa idara ya maji kwa ujumla na
kwa umoja na ushirikiano wao kufanikisha shughui hii na nawaomba waendelee hivyo
hivyo hadi tumalize Wiki ya Maji. Niwashukuru watumishi na wananchi waliofika
hapa na kwa namna ya pekee niwashukuru waandishi wa habari wa TV, Radio na
magazeti.
Maji ni Uhai na Usafi wa Mazingira ni Utu
Wiki ya Maji Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Aksanteni kwa kunisikiliza
6