SlideShare ist ein Scribd-Unternehmen logo
1 von 7
E-mail-kijogoogcd@yahoo.com
PROFILE
Kijogoo group for community development ni asasi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa
kwa sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali NGO ACT NO-24/2002 nakupewa usajili
namba NGO-0330 TAREHE 8/JANUARI/2008.
Makao makuu yake yapo
Mtaa wa. Mtawala
Kata ya Mwembesongo
Wilaya Morogoro Manispaa
Mkoa Morogoro
ANUANI YA SHIRIKA
Kijogoo Group For Community Development
P.o.box 1198
Morogoro
Simu na,0754 948767/0715 948797/0754201426/0754394192
DIRA YA SHIRIKA
Kuona jamii yenye uelewa wa kufanya ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya rasilimali
za umma
DHIMA YA SHIRIKA
Kuelimisha na kuhamasisha wananchi na viongozi kuhusu utawala unaozingatia
uwazi,ushikishwaji na uwajibikaji katika matumizi mazuri ya Rasilimali za Umma kwa
njia ya mafunzo,vyombo vya habari,vipeperushi,majarida na mikutano.
Kuanzishwa kwa asasi hii kulilenga kusukuma maendeleo kwa jamii kwa lengo la
kupambana na umasikini nchini Tanzania.
Kazi kubwa ni kuwaelimisha wananchi na jamii kwa ujumla waweze kujiletea
maendeleo yao kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini hasa kwa wakazi wa vijijini kwani
huko ndiko kwenye changamoto kubwa ya umasikini.
hususani walio katika mazingira magumu wakiwemo wanawake, vijana, watoto,
walemavu, wajane na wanaoishi na maambukizi ya vvu-Ukimwi
SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA SHIRIKA
Kuiweka pamoja jamii kwa kuwaelimisha na kuwahamasisha kupiga vita vitendo vyote
vinavyoashiria rushwa katika maeneo yanayotoa huduma za kijamii pamoja na jamii
kuelimishwa juu ya haki zao na kutambua wajibu wao kwa lengo la kuinua utawala bora
kupitia utetezi na njia nyingine zinazostaili kisheria ikiwa pamoja na kutafsiri kwa kuleta
uelewa kwa wote kuwapatia mafunzo/warsha kwa nadharia na vitendo kwa kuwapa ujuzi
na maarifa yatakayosaidia kujiletea maendeleo yao
KAZI TULIZOKWISHA FANYA
Kijogoo Group imefanya kazi ya mkutekeleza miradi 3 na tunaendelea na mradi wa 3 .
Miradi tuliyotekeleza ni pamoja na kuifundisha jamii mfumo wa kufanya ufuatiliaji wa
matumizi ya fedha za Umma kata tatu za Kisemu,Tawa na Kibangile Tarafa ya Matombo
Mwaka 2009
Mradi wa kufuatilia mapato na matumizi wa mgawo wa vocha za ruzuku za pembejeo
za kilimo kata 5 za Gairo,Rubeho,Kibedya,Chakwale na Iyogwe Tarafa ya Gairo,mradi
uliendeshwa kwa kuwapatia mafunzo watu 40 kwa siku 4 kwa kila kata na kila kata
iliteua watu 5 ambao walipatiwa mafunzo ya kina ya namna ya kukusanya takwimu na
waliweza kutengeneza zana ya kukusanyia takwimu,na baada ya kukusanya takwimu
zilipelekwa kwa wataalamu chuo kikuu cha mzumbe na kandikwa taarifa iliyotokana na
takwimu zilizokusanywa na taarifa hiyo ilipelekwa kwenye mkutano wa mrejesho ambao
ulihudhuriwa na watendaji wa kata zote 5,Madiwani wa kata zote 5,Maafisa kilimo
kutoka Wilayani Kilosa,Maafisa ugani wa kata zote 5,watu maarufu viongozi wa dini na
jadi,na katika taarifa hiyo ilionyesha mapungufu makubwa kwa upande wa ugawaji wa
hizo vocha ikabainika upotevu na udanganyifu wa vocha za za ruzuku za pembejeo
zenye thamani kubwa ya fedha
CHANGAMOTO TULIZOKUTANANAZO NI PAMOJA NA.-:
• Nipamoja na kutishiwa maisha na baadhi ya waliohusika katika zoezi la
kuchakachukua vocha za ruzuku msimu mwa kilimo 2009/2010
• Kukosa taarifa kabisa kwa baadhi ya watendaji wa kata na vijiji sehemu nyingine
kupata taafifa za uongo ambazo zilipishana na maeneo mengine tuliyokwenda
kutafuta taarifa
• Miundo mbinu ya barabara ilikuwa mibovu hali iliyopelekea kufikika kwa tabu
kwa baadhi ya maeneo ya mradi ikiwemo kijiji cha kisitwi,majawanga,kilama
leshata,ndogomi na madege kwani kulikuwa na ugumu wa kupitika kutokana na
mabonde yaliyokatiza katika kwenye barabara za kutufikisha makao makuu ya
vijiji
Shirika letu limetekeleza mradi wa 3 wa ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma
sekta ya maji wilayani Gairo na ni kata 5 tu ndizo zilizopitiwa kwenye utekelezwaji wa
mradi huo ambazo ni Msingisi,Gairo,Chakwale,Kibedya na Iyogwe Tarafa ya Gairo
Katika utekelezaji wa mradi huu tumefanikiwa kubaini mapungufu ya matumizi mabaya
ya rasilimali za Umma zikiwemo fedha na matumizi mabaya ya madaraka kwa kubania
kugawa maji kwa wananchi na kuamua kujaza kwenye matenki yao na kuwauzia
wananchi kwa bei ya juu tofauti na bei halali wanapoteka maji hayo kwenye vituo
/visima vya maji.
C: Matokeo ya ufuatiliaji na habari za mafanikio(Success story):
Mbali na kufanya ufuatiliaji huu wa mapungufu, timu hii imeweza kupata pia habari za
mafanikio yaliyotokana na shughuli zote za mradi katika Tarafa ya Gairo. Mafanikio
hayo ni pamoja na:
• Moja ya mafanikio hayo ni kuwa halmashauri imeweza kusikiliza vilio vya
wakazi wa Tarafa ya Gairo katika huduma za maji na hivyo Halmashauri imetoa
fedha kwa ajili ya kuchimbwa Visima virefu kumi na viwili (12) na Mh. Mbunge
amepokea taarifa ya utekelezaji wa uchimbwaji wa visima hivyo katika tarafa
yote ya Gairo na tayari wakandarasi wameanza kazi.
• Pia baada ya asasi kupigia kelele bei kubwa ya maji inayotozwa kwa wananchi
wa Gairo na asasi kufikisha malalamiko hayo kwa viongozihusika, bei ya ndoo
moja ya maji inayotozwa sasa imerekekbishwa na kuwa kiwango sawa katika
maeneo yote badala ya kupishana kama ilivyokuwa hapo awali.
• Kupitia mafunzo yaliyotolewa na asasi ya Kijogoo Group wananchi
walikubaliana kuunda kamati za maji ili kusimamaia miradi yao ya maji katika
maeneoe yao ili kuleta ufanisi katika upatikanaji wa maji. Hivyo basi Kamati za
maji zimeundwa katika vijiji vyote vilivyoko ndani ya kata za mradi tofauti na
mwanzo ambapo hakukuwa na katamati hizo za usimamizi.
• Vivyo hivyo asasi imewezesha kijiji cha Italagwe kupata visima vyake ambavyo
havikuchimbwa kwa muda mrefu mbali na fedha zake kuwa zilitengwa. Hivyo
basi visima viwili vya maji katika kijiji cha Italagwe vimeanza kuchimbwa na
tayari kisima kimoja kimeshachimbwa na kukamilika na kingine kipo hatua ya
awali ya uchimbwaji wake na hivyo kuwapatia maji wakazi hao.
• Mbali na hivyo asasi iliweza kuwahimiza viongozi wa wilaya kuhusiana na
upotevu wa maji ambayo yangefaa kuwapatia wananchi. Hivyo basi mpaka
sasa serikali imechukua hatua ya kudhibiti upotevu wa maji wenye ujazo wa lita
580 zilizokuwa zikipotea kwa kuziba miundombinu na kubadilisha pia
miundombinu baadhi.
• Wananchi wa kata ya Msingisi kutoka kijiji cha Luhwaji wamefanya maamuzi ya
kumfukisha kazi bwana maji aliyekuwa akitoa huduma hiyo kutokana na
kubainika kuwa alikuwa akitumia nafasi aliyokuwa nayo kufungulia maji kwa
muda mfupi kwa wananchi na kwa masaa 4 kwa siku badala ya kumi na mbili
(12) na amekuwa akiwauzia matajili na wafanya biashara ya maji kwenye mapipa
na hao wafanya biashara walikuwa wakiyauza kwa wananchi dumu 1 kati ya
1000/= na 1500/=na baada ya kuchuliwa hatua hiyo hali ya ununuzi wa maji kwa
dumu moja imeshuka hadi Tsh,400/= mpaka Tsh, 500/= kwa dumu moja.
• Wakazi wa chakwale wameifukuzisha kamati ya maji iliyokuwepo zamani
ambayo ilikusanya fedha kiasi cha Tsh, 5,000,000/= na zilitumika visivyo,
walipochukua hatua ya kufuatilia fedha zao hawajapata majibu ya kuridhisha
,kupitia hilo uongozi wote uliohusika umetimuliwa na hatua za kisheria za
kufikishwa mahakani zimefanyika na namba ya jalada la kesi ni no,95/2013
katika mahakama ya wilaya ya Kilosa, watuhumiwa hao na majina yao ni haya ..
1. ISMAILI MBAGA _ KATIBU
2 .BAKARI MAGUMBO _ MWEKA HAZINA
3. DANIEL GAMBAI _ MJUMBE
CHANGAMOTO TULIZOKUTANA WAKATI WA UTEKELEZAJI WA MRADI
HUU
• Ukosefu wa ushirikiano madhubuti: Asasi ilipata wakati mgumu sana katika
zoezi la kupata taarifa/takwimu zilizokuwa zikihitajika toka kwa wahusika ambao
ni Mawakala na Wasimamizi wa Vituo na Visima vya maji, Mhandisi wa maji wa
Wilaya na Mhandisi wa mji mdogo wa Gairo.
• Uoga wa wananchi katika kutoa taarifa: kutokana na Baadhi ya wananchi kuwa na
uelewa mdogo waliokuwa nao, walikuwa na uoga wa kutoa taarifa kwa dhana ya
kuhisi waratibu wa mradi kuwa ni maaskari, hali hiyo ilipelekea kukosa pia
baadhi ya taarifa toka kwao.
• Hofu za wananchi na viongozi juu ya Asasi katika suala la ufuatiliaji fedha na
matumizi yake viongozi wengi huwa na woga katika kutoa ushirikiano. Viongozi
wengi wlitaka kufahamu sisi ni akina nani, tumetoka wapi, tunatafuta nini, na
baada ya kubaini tunachokitafuta tutachukua hatua gani ?
• Uoga na uelewa mdogo wa washiriki: katika mikutano mingi iliyofanyika ya
mrejesho, wananchi wachache bado walion ekana kuwa na uoga wa kuchangia
hasa ikitokana na uwepo wa viongozi wao waliohudhuria, hii ilipelekea washiriki
wachache kuchangia mambo mengi ambayo yanawapata maeneo yao. Uoga huo
unatokana na baadhi ya viongozi kuwapa hadhabu mbalimbali watu wao
wanaotoa taarifa sahihi kwa vyombo vya maendeleo kama asasi hii.
MCHANGO WA SERIKALI KWA ASASI ZA KIRAIA
• Kutoa kibali kwa sisi asasi za kiraia kufanikisha zoezi la kufanya ufuatiliaji na
kutoa miongozo ya kuitekeleza sera
• Kuzifanyia kazi taarifa tunazowakabidhi kwa ajili ya utekelezaji kuwajibisha wale
wote waliobainika kwa namna moja ama nyingine katika ubadhirifu
• Kuziwezesha asasi kufanya kazi zao bila kuingilia na kutoa msaada wa muongozo
pale inapohitajika kufanya hivyo
Baada ya utekelezaji wa mradi huo shirika lilipata ufadhili mwingine kutoka The
Foundation For Civil Society kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa 4 wa Ufuatiliaji na
Uwajibikaji wa Jamii (UUJ) katika kufuatilia Rasilimali za Umma (SAM) Wilayani
Mahenge Tarafa ya Vigoi Kata za Nawenge na Msogezi.
MCHANGO WA MASHIRIKA MENGINE
Mchango wa mashirika mengine kwa mashirika madogo kama ili la Kijogoo Group ni
mkubwa sana ,mashirika hayo ni pamoja na The foundation for civil society ya mjini
Dar es salaam,kwa sasa yeye ndio mdau mkubwa sana kwa mashirika mengi hapa
Tanzania kwani ndio linaongoza kwa kutoa ruzuku za kutekeleza miradi mbalimbali
katika mikoa na wilaya zote hapa nchini.
The foundation for civil society (Fcs) imekuwa na mchango mkubwa sana kwa
maendeleo ya asasi na jamii kwa ujumla kwa kuwa linawezesha asasi kifedha na Elimu
ili asasi ziweze kutekeleza miradi kwa kwa kuleta mabadiliko kwa wananchi ufadhili wa
hao the foundation for civil society kwa miradi iliyoibuliwa na wananchi wenyewe na
wataalam kutoka kwenye asasi.
MUUNDO WA UONGOZI WA ASASI.
ELIMU TUNAZO PATA NA WAPI TUNAZIPATA HIZO ELIMU
Mashirika mengi hasa yanayofadhiliwa na The foundation for civil society huwa tuna
patiwa elimu za maramara ya kujengewa uwezo wa kuendesha mashirika,elimu hizo ni
pamoja na
• Uandishi wa miradi
• Usimamizi wamiradi
• Uandishi wa taarifa za utelezaji wa miradi
• Ufuatiliaji na kutathimini mradi
MAONI YETU.
Moja kati ya kazi ya kufanya asasi ni kuzidi kuelimishana kuijengea uwezo jamii kuhusu
kufuatilia mapato na matumizi za fedha za Umma ili kuwe na uwazi katika matumizi ya
rasilimali fedha na itapelekea matumizi mazuri katika rasilimali hizo,na pia kutapelekea
kuwepo kwa uwajibikaji wenye uwazi na ushirikishwaji jamii kwa watendaji na viongozi
katika matumizi ya rasilimali hizo kwakuwa hata tenda za ukandaras iwa ujenzi wa
barabara zitakuwa wazi na atakaeshinda tenda hiyo sifa zake zitaonekanana na barabara
zitakuwa na kiwango ambazo zitakaa/kuchukua muda mrefu kuharibika
Asasi ziwe na ushirikiano wa karibu kwa kutafuta na kupeana habari zenye kusaidia
kuchochea mabadiliko kwa kujadili kwa pamoja namna ya kutatua changamoto
zilizojitokeza na kutengeneza mpango kazi unaotekelezeka kwa kuleta mabadiliko yenye
manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla
PROFILE KIJOGOO

Weitere ähnliche Inhalte

Andere mochten auch

Ashton Pictures
Ashton PicturesAshton Pictures
Ashton PicturesTom Lord
 
Lego Minifigure Photography
Lego Minifigure PhotographyLego Minifigure Photography
Lego Minifigure PhotographyTom Lord
 
Profesija
ProfesijaProfesija
Profesijaausryt
 
¿Estamos formando analfabetos digitales?
¿Estamos formando analfabetos digitales?¿Estamos formando analfabetos digitales?
¿Estamos formando analfabetos digitales?Digital Pymes
 

Andere mochten auch (7)

Ativ 1 4-pablo
Ativ 1 4-pabloAtiv 1 4-pablo
Ativ 1 4-pablo
 
Marcha
MarchaMarcha
Marcha
 
Ashton Pictures
Ashton PicturesAshton Pictures
Ashton Pictures
 
Lego Minifigure Photography
Lego Minifigure PhotographyLego Minifigure Photography
Lego Minifigure Photography
 
Profesija
ProfesijaProfesija
Profesija
 
¿Estamos formando analfabetos digitales?
¿Estamos formando analfabetos digitales?¿Estamos formando analfabetos digitales?
¿Estamos formando analfabetos digitales?
 
Coma mixedematoso
Coma mixedematosoComa mixedematoso
Coma mixedematoso
 

Ähnlich wie PROFILE KIJOGOO

Risala kilele wiki ya maji by Eng Deule, tanu
Risala kilele  wiki ya maji by Eng Deule, tanuRisala kilele  wiki ya maji by Eng Deule, tanu
Risala kilele wiki ya maji by Eng Deule, tanuTanu Deule
 
TOLEO MAALUM MKOA WA TABORA
TOLEO MAALUM MKOA WA TABORATOLEO MAALUM MKOA WA TABORA
TOLEO MAALUM MKOA WA TABORAHubiri Burton
 
Sera ya maji ya taifa
Sera ya maji ya taifaSera ya maji ya taifa
Sera ya maji ya taifadarajatz
 
Implementation of NRM based project in Lushoto district Tanzania
Implementation of NRM based project in Lushoto district TanzaniaImplementation of NRM based project in Lushoto district Tanzania
Implementation of NRM based project in Lushoto district Tanzaniawickama
 
Risala kwa wananchi kilele wiki ya maji 2013 bulendabufwe bunda iliyosomwa na...
Risala kwa wananchi kilele wiki ya maji 2013 bulendabufwe bunda iliyosomwa na...Risala kwa wananchi kilele wiki ya maji 2013 bulendabufwe bunda iliyosomwa na...
Risala kwa wananchi kilele wiki ya maji 2013 bulendabufwe bunda iliyosomwa na...Tanu Deule
 

Ähnlich wie PROFILE KIJOGOO (6)

Risala kilele wiki ya maji by Eng Deule, tanu
Risala kilele  wiki ya maji by Eng Deule, tanuRisala kilele  wiki ya maji by Eng Deule, tanu
Risala kilele wiki ya maji by Eng Deule, tanu
 
TOLEO MAALUM MKOA WA TABORA
TOLEO MAALUM MKOA WA TABORATOLEO MAALUM MKOA WA TABORA
TOLEO MAALUM MKOA WA TABORA
 
Sera ya maji ya taifa
Sera ya maji ya taifaSera ya maji ya taifa
Sera ya maji ya taifa
 
Implementation of NRM based project in Lushoto district Tanzania
Implementation of NRM based project in Lushoto district TanzaniaImplementation of NRM based project in Lushoto district Tanzania
Implementation of NRM based project in Lushoto district Tanzania
 
Risala kwa wananchi kilele wiki ya maji 2013 bulendabufwe bunda iliyosomwa na...
Risala kwa wananchi kilele wiki ya maji 2013 bulendabufwe bunda iliyosomwa na...Risala kwa wananchi kilele wiki ya maji 2013 bulendabufwe bunda iliyosomwa na...
Risala kwa wananchi kilele wiki ya maji 2013 bulendabufwe bunda iliyosomwa na...
 
CCAP leaflet.
CCAP leaflet.CCAP leaflet.
CCAP leaflet.
 

PROFILE KIJOGOO

  • 1. E-mail-kijogoogcd@yahoo.com PROFILE Kijogoo group for community development ni asasi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa kwa sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali NGO ACT NO-24/2002 nakupewa usajili namba NGO-0330 TAREHE 8/JANUARI/2008. Makao makuu yake yapo Mtaa wa. Mtawala Kata ya Mwembesongo Wilaya Morogoro Manispaa Mkoa Morogoro ANUANI YA SHIRIKA Kijogoo Group For Community Development P.o.box 1198 Morogoro Simu na,0754 948767/0715 948797/0754201426/0754394192 DIRA YA SHIRIKA Kuona jamii yenye uelewa wa kufanya ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya rasilimali za umma DHIMA YA SHIRIKA Kuelimisha na kuhamasisha wananchi na viongozi kuhusu utawala unaozingatia uwazi,ushikishwaji na uwajibikaji katika matumizi mazuri ya Rasilimali za Umma kwa njia ya mafunzo,vyombo vya habari,vipeperushi,majarida na mikutano.
  • 2. Kuanzishwa kwa asasi hii kulilenga kusukuma maendeleo kwa jamii kwa lengo la kupambana na umasikini nchini Tanzania. Kazi kubwa ni kuwaelimisha wananchi na jamii kwa ujumla waweze kujiletea maendeleo yao kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini hasa kwa wakazi wa vijijini kwani huko ndiko kwenye changamoto kubwa ya umasikini. hususani walio katika mazingira magumu wakiwemo wanawake, vijana, watoto, walemavu, wajane na wanaoishi na maambukizi ya vvu-Ukimwi SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA SHIRIKA Kuiweka pamoja jamii kwa kuwaelimisha na kuwahamasisha kupiga vita vitendo vyote vinavyoashiria rushwa katika maeneo yanayotoa huduma za kijamii pamoja na jamii kuelimishwa juu ya haki zao na kutambua wajibu wao kwa lengo la kuinua utawala bora kupitia utetezi na njia nyingine zinazostaili kisheria ikiwa pamoja na kutafsiri kwa kuleta uelewa kwa wote kuwapatia mafunzo/warsha kwa nadharia na vitendo kwa kuwapa ujuzi na maarifa yatakayosaidia kujiletea maendeleo yao KAZI TULIZOKWISHA FANYA Kijogoo Group imefanya kazi ya mkutekeleza miradi 3 na tunaendelea na mradi wa 3 . Miradi tuliyotekeleza ni pamoja na kuifundisha jamii mfumo wa kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za Umma kata tatu za Kisemu,Tawa na Kibangile Tarafa ya Matombo Mwaka 2009 Mradi wa kufuatilia mapato na matumizi wa mgawo wa vocha za ruzuku za pembejeo za kilimo kata 5 za Gairo,Rubeho,Kibedya,Chakwale na Iyogwe Tarafa ya Gairo,mradi uliendeshwa kwa kuwapatia mafunzo watu 40 kwa siku 4 kwa kila kata na kila kata iliteua watu 5 ambao walipatiwa mafunzo ya kina ya namna ya kukusanya takwimu na waliweza kutengeneza zana ya kukusanyia takwimu,na baada ya kukusanya takwimu zilipelekwa kwa wataalamu chuo kikuu cha mzumbe na kandikwa taarifa iliyotokana na takwimu zilizokusanywa na taarifa hiyo ilipelekwa kwenye mkutano wa mrejesho ambao ulihudhuriwa na watendaji wa kata zote 5,Madiwani wa kata zote 5,Maafisa kilimo kutoka Wilayani Kilosa,Maafisa ugani wa kata zote 5,watu maarufu viongozi wa dini na jadi,na katika taarifa hiyo ilionyesha mapungufu makubwa kwa upande wa ugawaji wa hizo vocha ikabainika upotevu na udanganyifu wa vocha za za ruzuku za pembejeo zenye thamani kubwa ya fedha CHANGAMOTO TULIZOKUTANANAZO NI PAMOJA NA.-: • Nipamoja na kutishiwa maisha na baadhi ya waliohusika katika zoezi la kuchakachukua vocha za ruzuku msimu mwa kilimo 2009/2010
  • 3. • Kukosa taarifa kabisa kwa baadhi ya watendaji wa kata na vijiji sehemu nyingine kupata taafifa za uongo ambazo zilipishana na maeneo mengine tuliyokwenda kutafuta taarifa • Miundo mbinu ya barabara ilikuwa mibovu hali iliyopelekea kufikika kwa tabu kwa baadhi ya maeneo ya mradi ikiwemo kijiji cha kisitwi,majawanga,kilama leshata,ndogomi na madege kwani kulikuwa na ugumu wa kupitika kutokana na mabonde yaliyokatiza katika kwenye barabara za kutufikisha makao makuu ya vijiji Shirika letu limetekeleza mradi wa 3 wa ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma sekta ya maji wilayani Gairo na ni kata 5 tu ndizo zilizopitiwa kwenye utekelezwaji wa mradi huo ambazo ni Msingisi,Gairo,Chakwale,Kibedya na Iyogwe Tarafa ya Gairo Katika utekelezaji wa mradi huu tumefanikiwa kubaini mapungufu ya matumizi mabaya ya rasilimali za Umma zikiwemo fedha na matumizi mabaya ya madaraka kwa kubania kugawa maji kwa wananchi na kuamua kujaza kwenye matenki yao na kuwauzia wananchi kwa bei ya juu tofauti na bei halali wanapoteka maji hayo kwenye vituo /visima vya maji. C: Matokeo ya ufuatiliaji na habari za mafanikio(Success story): Mbali na kufanya ufuatiliaji huu wa mapungufu, timu hii imeweza kupata pia habari za mafanikio yaliyotokana na shughuli zote za mradi katika Tarafa ya Gairo. Mafanikio hayo ni pamoja na: • Moja ya mafanikio hayo ni kuwa halmashauri imeweza kusikiliza vilio vya wakazi wa Tarafa ya Gairo katika huduma za maji na hivyo Halmashauri imetoa fedha kwa ajili ya kuchimbwa Visima virefu kumi na viwili (12) na Mh. Mbunge amepokea taarifa ya utekelezaji wa uchimbwaji wa visima hivyo katika tarafa yote ya Gairo na tayari wakandarasi wameanza kazi. • Pia baada ya asasi kupigia kelele bei kubwa ya maji inayotozwa kwa wananchi wa Gairo na asasi kufikisha malalamiko hayo kwa viongozihusika, bei ya ndoo moja ya maji inayotozwa sasa imerekekbishwa na kuwa kiwango sawa katika maeneo yote badala ya kupishana kama ilivyokuwa hapo awali. • Kupitia mafunzo yaliyotolewa na asasi ya Kijogoo Group wananchi walikubaliana kuunda kamati za maji ili kusimamaia miradi yao ya maji katika maeneoe yao ili kuleta ufanisi katika upatikanaji wa maji. Hivyo basi Kamati za maji zimeundwa katika vijiji vyote vilivyoko ndani ya kata za mradi tofauti na mwanzo ambapo hakukuwa na katamati hizo za usimamizi.
  • 4. • Vivyo hivyo asasi imewezesha kijiji cha Italagwe kupata visima vyake ambavyo havikuchimbwa kwa muda mrefu mbali na fedha zake kuwa zilitengwa. Hivyo basi visima viwili vya maji katika kijiji cha Italagwe vimeanza kuchimbwa na tayari kisima kimoja kimeshachimbwa na kukamilika na kingine kipo hatua ya awali ya uchimbwaji wake na hivyo kuwapatia maji wakazi hao. • Mbali na hivyo asasi iliweza kuwahimiza viongozi wa wilaya kuhusiana na upotevu wa maji ambayo yangefaa kuwapatia wananchi. Hivyo basi mpaka sasa serikali imechukua hatua ya kudhibiti upotevu wa maji wenye ujazo wa lita 580 zilizokuwa zikipotea kwa kuziba miundombinu na kubadilisha pia miundombinu baadhi. • Wananchi wa kata ya Msingisi kutoka kijiji cha Luhwaji wamefanya maamuzi ya kumfukisha kazi bwana maji aliyekuwa akitoa huduma hiyo kutokana na kubainika kuwa alikuwa akitumia nafasi aliyokuwa nayo kufungulia maji kwa muda mfupi kwa wananchi na kwa masaa 4 kwa siku badala ya kumi na mbili (12) na amekuwa akiwauzia matajili na wafanya biashara ya maji kwenye mapipa na hao wafanya biashara walikuwa wakiyauza kwa wananchi dumu 1 kati ya 1000/= na 1500/=na baada ya kuchuliwa hatua hiyo hali ya ununuzi wa maji kwa dumu moja imeshuka hadi Tsh,400/= mpaka Tsh, 500/= kwa dumu moja. • Wakazi wa chakwale wameifukuzisha kamati ya maji iliyokuwepo zamani ambayo ilikusanya fedha kiasi cha Tsh, 5,000,000/= na zilitumika visivyo, walipochukua hatua ya kufuatilia fedha zao hawajapata majibu ya kuridhisha ,kupitia hilo uongozi wote uliohusika umetimuliwa na hatua za kisheria za kufikishwa mahakani zimefanyika na namba ya jalada la kesi ni no,95/2013 katika mahakama ya wilaya ya Kilosa, watuhumiwa hao na majina yao ni haya .. 1. ISMAILI MBAGA _ KATIBU 2 .BAKARI MAGUMBO _ MWEKA HAZINA 3. DANIEL GAMBAI _ MJUMBE CHANGAMOTO TULIZOKUTANA WAKATI WA UTEKELEZAJI WA MRADI HUU • Ukosefu wa ushirikiano madhubuti: Asasi ilipata wakati mgumu sana katika zoezi la kupata taarifa/takwimu zilizokuwa zikihitajika toka kwa wahusika ambao
  • 5. ni Mawakala na Wasimamizi wa Vituo na Visima vya maji, Mhandisi wa maji wa Wilaya na Mhandisi wa mji mdogo wa Gairo. • Uoga wa wananchi katika kutoa taarifa: kutokana na Baadhi ya wananchi kuwa na uelewa mdogo waliokuwa nao, walikuwa na uoga wa kutoa taarifa kwa dhana ya kuhisi waratibu wa mradi kuwa ni maaskari, hali hiyo ilipelekea kukosa pia baadhi ya taarifa toka kwao. • Hofu za wananchi na viongozi juu ya Asasi katika suala la ufuatiliaji fedha na matumizi yake viongozi wengi huwa na woga katika kutoa ushirikiano. Viongozi wengi wlitaka kufahamu sisi ni akina nani, tumetoka wapi, tunatafuta nini, na baada ya kubaini tunachokitafuta tutachukua hatua gani ? • Uoga na uelewa mdogo wa washiriki: katika mikutano mingi iliyofanyika ya mrejesho, wananchi wachache bado walion ekana kuwa na uoga wa kuchangia hasa ikitokana na uwepo wa viongozi wao waliohudhuria, hii ilipelekea washiriki wachache kuchangia mambo mengi ambayo yanawapata maeneo yao. Uoga huo unatokana na baadhi ya viongozi kuwapa hadhabu mbalimbali watu wao wanaotoa taarifa sahihi kwa vyombo vya maendeleo kama asasi hii. MCHANGO WA SERIKALI KWA ASASI ZA KIRAIA • Kutoa kibali kwa sisi asasi za kiraia kufanikisha zoezi la kufanya ufuatiliaji na kutoa miongozo ya kuitekeleza sera • Kuzifanyia kazi taarifa tunazowakabidhi kwa ajili ya utekelezaji kuwajibisha wale wote waliobainika kwa namna moja ama nyingine katika ubadhirifu • Kuziwezesha asasi kufanya kazi zao bila kuingilia na kutoa msaada wa muongozo pale inapohitajika kufanya hivyo Baada ya utekelezaji wa mradi huo shirika lilipata ufadhili mwingine kutoka The Foundation For Civil Society kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa 4 wa Ufuatiliaji na Uwajibikaji wa Jamii (UUJ) katika kufuatilia Rasilimali za Umma (SAM) Wilayani Mahenge Tarafa ya Vigoi Kata za Nawenge na Msogezi. MCHANGO WA MASHIRIKA MENGINE Mchango wa mashirika mengine kwa mashirika madogo kama ili la Kijogoo Group ni mkubwa sana ,mashirika hayo ni pamoja na The foundation for civil society ya mjini Dar es salaam,kwa sasa yeye ndio mdau mkubwa sana kwa mashirika mengi hapa Tanzania kwani ndio linaongoza kwa kutoa ruzuku za kutekeleza miradi mbalimbali katika mikoa na wilaya zote hapa nchini. The foundation for civil society (Fcs) imekuwa na mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya asasi na jamii kwa ujumla kwa kuwa linawezesha asasi kifedha na Elimu ili asasi ziweze kutekeleza miradi kwa kwa kuleta mabadiliko kwa wananchi ufadhili wa
  • 6. hao the foundation for civil society kwa miradi iliyoibuliwa na wananchi wenyewe na wataalam kutoka kwenye asasi. MUUNDO WA UONGOZI WA ASASI. ELIMU TUNAZO PATA NA WAPI TUNAZIPATA HIZO ELIMU Mashirika mengi hasa yanayofadhiliwa na The foundation for civil society huwa tuna patiwa elimu za maramara ya kujengewa uwezo wa kuendesha mashirika,elimu hizo ni pamoja na • Uandishi wa miradi • Usimamizi wamiradi • Uandishi wa taarifa za utelezaji wa miradi • Ufuatiliaji na kutathimini mradi MAONI YETU. Moja kati ya kazi ya kufanya asasi ni kuzidi kuelimishana kuijengea uwezo jamii kuhusu kufuatilia mapato na matumizi za fedha za Umma ili kuwe na uwazi katika matumizi ya rasilimali fedha na itapelekea matumizi mazuri katika rasilimali hizo,na pia kutapelekea kuwepo kwa uwajibikaji wenye uwazi na ushirikishwaji jamii kwa watendaji na viongozi katika matumizi ya rasilimali hizo kwakuwa hata tenda za ukandaras iwa ujenzi wa barabara zitakuwa wazi na atakaeshinda tenda hiyo sifa zake zitaonekanana na barabara zitakuwa na kiwango ambazo zitakaa/kuchukua muda mrefu kuharibika Asasi ziwe na ushirikiano wa karibu kwa kutafuta na kupeana habari zenye kusaidia kuchochea mabadiliko kwa kujadili kwa pamoja namna ya kutatua changamoto zilizojitokeza na kutengeneza mpango kazi unaotekelezeka kwa kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla