SlideShare ist ein Scribd-Unternehmen logo
1 von 2
Downloaden Sie, um offline zu lesen
1 | K i l o g h a C i F r i d a y , M a r c h 2 3 , 2 0 1 8
Kuishi katika Karama ya Upendo1
1. Utangulizi
Maisha yetu hapa duniani kunavitu ambavyo tunaviona mara chache sana na tunavingine
tunavyosimuliwa na ambavyo vimebaki katika ndoto katika matarajio yasiyoonekana kwa sasa. Lakini
Vipo vitu ambavyo vinapatikana na hufanyika muda wote na vinaulazima kufanywa na kila mtu kadiri ya
mtu alivyo yaani hakuna fomula na utaratibu wa kudumu.2
Upendo ni moja kati ya karama zinazotakiwa
kuwepo kwa kila mtu. Hakuna asiyejua nini maana ya kupenda. Bahati nzuri tumejaliwa kutumia alama
zinazowakilisha vitu vilivyofichika. Hata upendo tunatumia alama…..mfano kuchora moyo uliochomwa
na mkuki… Licha ya ufahamu wetu juu ya upendo, bado si katika asilimia zote tunaweza kusema tunajua
maana ya Upendo… Hata hivyo upendo sio karama ya kiutu zinazotokana na mzoezi ya kibinadamu,
wenyewe ni moja ya karama zile tatu za Kimungu, hivyo kuifahamu karama ya upendo kwahitajika Imani
na kujikabidhi kwa Mungu…
2. Maana
a. Maana ilozoeleka
Kwa uchache tutaangalia namna tunavyo ufahamu Upendo katika namna ya kawaida.
Nitatumia mifano michache kuoanisha uelewa unaolinganishwa na upendo.
i. Wapo watu wanaoweza kusikitishwa na kuumizwa pale wanapoona wengine
Wakiteswa au kuumizwa. Je mtu anayeumizwa kwa mtindo huu anaonyesha mapendo kwa mtu yule
akiyeumizwa…? Hapana hiyo ni Hisia (Emotion) ambayo yaweza kuwepo kwa viumbe wengine pia. Kuna
hisia za furaha na hisia za uchungu na sio mapenzi ya furaha wala ya huzuni. Watu wanaojenga dhana ya
upendo kwa hisia hufanya hivyo kwa matukio, na tukio la kuumizwa likipita hakuna hisia tena.
Utapendwa tu pale utakapo kuwa umeingia katika shida.
ii. Wapo ambao wanaweza kuwasaidia watu kutokana na nafasi zao, mfano mwl
na mwanafunzi, mzazi na mtoto, nesi na mgonjwa, padre na muumini Konda na abiria na
kadhalika…nafasi inayotolewa na watu hao wanapojibidisha katika kuwasaidia walengwa wao sio
mapendo hayo ila ni Wajibu (Responsibility). Kwa wale tunaopaswa kuwajibika kwa wengine, waangalie
wasiwadanganye walengwa wao kuwa wanawapenda, watimize wajibu wao vyema na kwa vile kila
wajibu hulipwa basi tulipwe kwa haki kwa kuwajibika vyema kwa kuwatendea mema wanaohitajika.
iii. Upo wakati unakutana na mtu amependeza na kuvutia kiasi cha kukufanya
Uhamishe mawazo na muda kwa mtu huyo, kwa kufanya hivyo hutoi sura ya upendo hapo ila hali hiyo
huitwa Pumbazo (Admiration). Mapendo hayajengwi na msingi wa kuwapumbaza wengine kwa uzuri au
mengine ya kupendeza. Nao huwa ni upendo wa muda tu akitokea anaye kuzidi kwa pumbaziko ndio
basi huna nafasi katika maisha ya mtu.
iv. Kuna kipindi unaweza ukawa na mshawashawa wa kumwangalia mwanamke
Kiasi cha kutaka hata kumkumbatia, hali hiyo haiwezi na haithibitishi mapendo, bali hiyo ni Tamaa
(Desire au Lusty). Tamaa ipo kutokana na harara za mwili lakini hazionyeshi upendo wa kweli. Mtu
anaweza kukumbatia na kukubusu lakini linaweza kuwa ni busu la kukusaliti3
1
lKor 13:1-13 Upendo ndio karama iliyokuu
2
Mchapo wa Vipofu wawili na Tembo aliyeuawa.
3
Mt 26:48-49 Kisi la Uhaini
2 | K i l o g h a C i F r i d a y , M a r c h 2 3 , 2 0 1 8
Kwa ujumla wake mapendo ya kweli hayawezi kufananishwa na hisia, wajibu, pumbaziko na tamaa.
Neno Upendo ni zaidi ya hayo tuliyoyaona hapo juu. Vionjo hivyo vilivyoonyeshwa huashiria Mapendo
binafsi.
b. Maana inayokaribiana na Ukweli
Upendo hauna mbadala…wala si mbadala wa hisia, pumbaziko na tamaa. Ukiona humpendi mtu hadi
akutolee hisia zake ujue utapenda lakini kidogo tu. Mapendo ni Zawadi ya nafsi ya mtu kwa wengine.
Mapendo sio vionjo, lakini ni uchaguzi ufanywao kwa uhakika kwa kumvuta mwingine.
Mapendo ni Ufadhili au kwa Kiebrania Hesed4
mtu mmoja anapojitolea na kuvutika kwa mwingine bila
kutaka faida. Kama ni barabara, upendo ni one way road, hakuna kurudi au kupishanisha magari. Ni
mvuto unaotoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine bila faida. Haya sio mahusiano ya kawaida,
kwani tumezoea kuona watu wakionyeshana upendo wa kibiashara wa nipe nikupe. Upendo huu ndio
upendo wa Kimungu, Agape love ambao unafundishwa na Kristu mwenyewe. Aliwapenda watu upeo
kiasi cha kumwaga damu yake msalabani kwa wokovu wa kila kiumbe…5
Katika upendo wa Kristu tunajifunza principal ya kujiachia kwa ajili ya wengine, (ie detachment by
attachment.) Hali hii yahitaji mtu kuyatoa yote kwa ajili ya mwingine bila kufikiria faida inayoweza
kutokana na muungano huo. Katika kumpa kitu mtu hutoi umiliki wala dhamana ya kurudishiwa
uloyatoa. Na unachokitoa lazima kiwe na maana na kumjenga anayekipokea…sio kutoa maua kwa
mwingine kwa vile unaogopa hayo maua yasikukaukie… katika dhamana ya kupeana pia hakutakiwi
ulinganifu wa kile kinachotolewa.
Matunda ya upendo daima yanatakiwa kuwa furaha, amani na umoja.6
Upendo pia ndio barabara ya
kufika kwa Mungu kwani mahali mapendo yanapokuwa yamechangamka dhambi huwa haipo. Ni njia
pekee ya inayompeleka mtu katika matarajio ya kiroho.
c. Hitimisho
Upendo ni karama ya KiMungu yatokana na zao la bidii inayojengwa na Mungu Mwenyewe kupitia Roho
Mtakatifu. Tofauti na karama zingine za kiutu zitokanazo na bidii ya kibinadamu inayotokana na mazoezi
ya kimaadili, hupendo hubaki karama kubwa kuzishinda zote. Kielelezo cha upendo ni Mungu (I Jn 4:7-
12) mwenyewe na Kristu ndiye anayetuonyesha upendo huo.
Tafakari/Majadiliano
Mtu anauguliwa na mtoto na hana pesa, ila kuna sehemu wanatoa pesa endapo utatolea viungo vyako
vya mwili… je kuna uhalali wa kufanya hivyo, na kufanya hivyo ndio upendo?
4
Hos 2:19… Yer 2:2
5
Yn 13:1…. Aliwapenda watu upeo…
6
Mfano wa Meza ya Mbinguni na Motoni…na vijiko virefu…

Weitere ähnliche Inhalte

Empfohlen

Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)contently
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024Albert Qian
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsKurio // The Social Media Age(ncy)
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Search Engine Journal
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summarySpeakerHub
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Tessa Mero
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentLily Ray
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best PracticesVit Horky
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementMindGenius
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...RachelPearson36
 
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...Applitools
 
12 Ways to Increase Your Influence at Work
12 Ways to Increase Your Influence at Work12 Ways to Increase Your Influence at Work
12 Ways to Increase Your Influence at WorkGetSmarter
 
Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...
Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...
Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...DevGAMM Conference
 
Barbie - Brand Strategy Presentation
Barbie - Brand Strategy PresentationBarbie - Brand Strategy Presentation
Barbie - Brand Strategy PresentationErica Santiago
 
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them well
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them wellGood Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them well
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them wellSaba Software
 
Empfohlen (20)

Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
 
How to have difficult conversations
How to have difficult conversations How to have difficult conversations
How to have difficult conversations
 
Introduction to Data Science
Introduction to Data ScienceIntroduction to Data Science
Introduction to Data Science
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best Practices
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project management
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
 
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
 
12 Ways to Increase Your Influence at Work
12 Ways to Increase Your Influence at Work12 Ways to Increase Your Influence at Work
12 Ways to Increase Your Influence at Work
 
ChatGPT webinar slides
ChatGPT webinar slidesChatGPT webinar slides
ChatGPT webinar slides
 
More than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike Routes
More than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike RoutesMore than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike Routes
More than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike Routes
 
Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...
Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...
Ride the Storm: Navigating Through Unstable Periods / Katerina Rudko (Belka G...
 
Barbie - Brand Strategy Presentation
Barbie - Brand Strategy PresentationBarbie - Brand Strategy Presentation
Barbie - Brand Strategy Presentation
 
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them well
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them wellGood Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them well
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them well
 
4. wajibu wa wito wetu katika mapendo

  • 1. 1 | K i l o g h a C i F r i d a y , M a r c h 2 3 , 2 0 1 8 Kuishi katika Karama ya Upendo1 1. Utangulizi Maisha yetu hapa duniani kunavitu ambavyo tunaviona mara chache sana na tunavingine tunavyosimuliwa na ambavyo vimebaki katika ndoto katika matarajio yasiyoonekana kwa sasa. Lakini Vipo vitu ambavyo vinapatikana na hufanyika muda wote na vinaulazima kufanywa na kila mtu kadiri ya mtu alivyo yaani hakuna fomula na utaratibu wa kudumu.2 Upendo ni moja kati ya karama zinazotakiwa kuwepo kwa kila mtu. Hakuna asiyejua nini maana ya kupenda. Bahati nzuri tumejaliwa kutumia alama zinazowakilisha vitu vilivyofichika. Hata upendo tunatumia alama…..mfano kuchora moyo uliochomwa na mkuki… Licha ya ufahamu wetu juu ya upendo, bado si katika asilimia zote tunaweza kusema tunajua maana ya Upendo… Hata hivyo upendo sio karama ya kiutu zinazotokana na mzoezi ya kibinadamu, wenyewe ni moja ya karama zile tatu za Kimungu, hivyo kuifahamu karama ya upendo kwahitajika Imani na kujikabidhi kwa Mungu… 2. Maana a. Maana ilozoeleka Kwa uchache tutaangalia namna tunavyo ufahamu Upendo katika namna ya kawaida. Nitatumia mifano michache kuoanisha uelewa unaolinganishwa na upendo. i. Wapo watu wanaoweza kusikitishwa na kuumizwa pale wanapoona wengine Wakiteswa au kuumizwa. Je mtu anayeumizwa kwa mtindo huu anaonyesha mapendo kwa mtu yule akiyeumizwa…? Hapana hiyo ni Hisia (Emotion) ambayo yaweza kuwepo kwa viumbe wengine pia. Kuna hisia za furaha na hisia za uchungu na sio mapenzi ya furaha wala ya huzuni. Watu wanaojenga dhana ya upendo kwa hisia hufanya hivyo kwa matukio, na tukio la kuumizwa likipita hakuna hisia tena. Utapendwa tu pale utakapo kuwa umeingia katika shida. ii. Wapo ambao wanaweza kuwasaidia watu kutokana na nafasi zao, mfano mwl na mwanafunzi, mzazi na mtoto, nesi na mgonjwa, padre na muumini Konda na abiria na kadhalika…nafasi inayotolewa na watu hao wanapojibidisha katika kuwasaidia walengwa wao sio mapendo hayo ila ni Wajibu (Responsibility). Kwa wale tunaopaswa kuwajibika kwa wengine, waangalie wasiwadanganye walengwa wao kuwa wanawapenda, watimize wajibu wao vyema na kwa vile kila wajibu hulipwa basi tulipwe kwa haki kwa kuwajibika vyema kwa kuwatendea mema wanaohitajika. iii. Upo wakati unakutana na mtu amependeza na kuvutia kiasi cha kukufanya Uhamishe mawazo na muda kwa mtu huyo, kwa kufanya hivyo hutoi sura ya upendo hapo ila hali hiyo huitwa Pumbazo (Admiration). Mapendo hayajengwi na msingi wa kuwapumbaza wengine kwa uzuri au mengine ya kupendeza. Nao huwa ni upendo wa muda tu akitokea anaye kuzidi kwa pumbaziko ndio basi huna nafasi katika maisha ya mtu. iv. Kuna kipindi unaweza ukawa na mshawashawa wa kumwangalia mwanamke Kiasi cha kutaka hata kumkumbatia, hali hiyo haiwezi na haithibitishi mapendo, bali hiyo ni Tamaa (Desire au Lusty). Tamaa ipo kutokana na harara za mwili lakini hazionyeshi upendo wa kweli. Mtu anaweza kukumbatia na kukubusu lakini linaweza kuwa ni busu la kukusaliti3 1 lKor 13:1-13 Upendo ndio karama iliyokuu 2 Mchapo wa Vipofu wawili na Tembo aliyeuawa. 3 Mt 26:48-49 Kisi la Uhaini
  • 2. 2 | K i l o g h a C i F r i d a y , M a r c h 2 3 , 2 0 1 8 Kwa ujumla wake mapendo ya kweli hayawezi kufananishwa na hisia, wajibu, pumbaziko na tamaa. Neno Upendo ni zaidi ya hayo tuliyoyaona hapo juu. Vionjo hivyo vilivyoonyeshwa huashiria Mapendo binafsi. b. Maana inayokaribiana na Ukweli Upendo hauna mbadala…wala si mbadala wa hisia, pumbaziko na tamaa. Ukiona humpendi mtu hadi akutolee hisia zake ujue utapenda lakini kidogo tu. Mapendo ni Zawadi ya nafsi ya mtu kwa wengine. Mapendo sio vionjo, lakini ni uchaguzi ufanywao kwa uhakika kwa kumvuta mwingine. Mapendo ni Ufadhili au kwa Kiebrania Hesed4 mtu mmoja anapojitolea na kuvutika kwa mwingine bila kutaka faida. Kama ni barabara, upendo ni one way road, hakuna kurudi au kupishanisha magari. Ni mvuto unaotoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine bila faida. Haya sio mahusiano ya kawaida, kwani tumezoea kuona watu wakionyeshana upendo wa kibiashara wa nipe nikupe. Upendo huu ndio upendo wa Kimungu, Agape love ambao unafundishwa na Kristu mwenyewe. Aliwapenda watu upeo kiasi cha kumwaga damu yake msalabani kwa wokovu wa kila kiumbe…5 Katika upendo wa Kristu tunajifunza principal ya kujiachia kwa ajili ya wengine, (ie detachment by attachment.) Hali hii yahitaji mtu kuyatoa yote kwa ajili ya mwingine bila kufikiria faida inayoweza kutokana na muungano huo. Katika kumpa kitu mtu hutoi umiliki wala dhamana ya kurudishiwa uloyatoa. Na unachokitoa lazima kiwe na maana na kumjenga anayekipokea…sio kutoa maua kwa mwingine kwa vile unaogopa hayo maua yasikukaukie… katika dhamana ya kupeana pia hakutakiwi ulinganifu wa kile kinachotolewa. Matunda ya upendo daima yanatakiwa kuwa furaha, amani na umoja.6 Upendo pia ndio barabara ya kufika kwa Mungu kwani mahali mapendo yanapokuwa yamechangamka dhambi huwa haipo. Ni njia pekee ya inayompeleka mtu katika matarajio ya kiroho. c. Hitimisho Upendo ni karama ya KiMungu yatokana na zao la bidii inayojengwa na Mungu Mwenyewe kupitia Roho Mtakatifu. Tofauti na karama zingine za kiutu zitokanazo na bidii ya kibinadamu inayotokana na mazoezi ya kimaadili, hupendo hubaki karama kubwa kuzishinda zote. Kielelezo cha upendo ni Mungu (I Jn 4:7- 12) mwenyewe na Kristu ndiye anayetuonyesha upendo huo. Tafakari/Majadiliano Mtu anauguliwa na mtoto na hana pesa, ila kuna sehemu wanatoa pesa endapo utatolea viungo vyako vya mwili… je kuna uhalali wa kufanya hivyo, na kufanya hivyo ndio upendo? 4 Hos 2:19… Yer 2:2 5 Yn 13:1…. Aliwapenda watu upeo… 6 Mfano wa Meza ya Mbinguni na Motoni…na vijiko virefu…