Diese Präsentation wurde erfolgreich gemeldet.
Wir verwenden Ihre LinkedIn Profilangaben und Informationen zu Ihren Aktivitäten, um Anzeigen zu personalisieren und Ihnen relevantere Inhalte anzuzeigen. Sie können Ihre Anzeigeneinstellungen jederzeit ändern.

Mofolojia

  • Loggen Sie sich ein, um Kommentare anzuzeigen.

Mofolojia

  1. 1. CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AGUSTINO, TANZANIA KITUO CHA BUKOBA KITIVO CHA ELIMU IDARA : KISWAHILI. JINA LA KOZI: MOFOLOJIA YA KISWAHILI. MSIMBO WA KOZI: SW 224 JINA LA MHADHIRI: LUPAPULA, ABEL. JINA LA MWANAFUNZI: MAPESA, NESTORY NAMBA YA USAJILI : BAEDII 41584 AINA YA KAZI: KAZI BINAFSI. TAREHE YA UWASILISHAJI: 28/03/2014 Swali; Unyambuzi na Uambatizi ni dhana telezi. Jadili
  2. 2. Rubanza (1996:98) Unyambuaji kama ulivyo uambishaji unahusu upachikaji wa mofimu katika mofimu mzizi aidha unahusu upachikaji wa mofimu zinazofuata mzizi yaani mofimu fuatishi. Matinde ( 2012:119) Unyambulishaji ni mbinu ya uuundaji wa maneno hivi kwamba viambishi mbalimbali huambikwa kwenye mzizi husika ili kuunda neno jipya. Massamba na wenzake ( 2009) Uambishaji katika lugha ni uwekaji pamoja na viambishi na mzizi kwa namna mbalimbali bila kutilia maanani suala la aina ya maumbo yanayopatikana alimradi tu miunganiko inayotolewa ikubalike kisarufi katika lugha, uambishaji kisarufi ndio wengine wanauita uambatizi. Rubanza (1996:90) Uambatizi ameuita kuwa ndio uambishaji ambao ni upachikaji wa mofimu katika mzizi ambao huonesha upatanisho wa kisarufi wa vipashio vingine vya sentensi. Habwe na Karanja (2004) anasema uambishaji ambao wengine huuita uambatizi ni utaratibu wa kuongeza viambishi katika mofimu mzizi wa neno wanasema viambishi huweza kuambikwa kabla, katikati na baada ya mzizi wa neno. TUKI ( 2009:89) Uambishaji katika taaluma ya mofolojia huu ni utaratibu wa kuweka kiambishi, kabla, katikati au baada ya mzizi. UTELEZI WA UAMBATIZI NA UNYAMBUZI Ni ukweli kwamba unyambuzi na uambatizi ni dhana telezi kwani kumekuwapo na mikanganyiko juu ya dhana hizi mbili kulingana na wataalamu mbalimbali katika kuelezea, kwa mujibu wa Rubanza amechanganya dhana mbili tofauti yaani uambatizi na Uambishaji kuwa ni kitu kimoja. Rubanza ameeleza kuwa Unyambulishaji unagawanyika sehemu mbili ambazo ni Uambishaji na Unyambuaji Vilevile kwa kuwarejelea Habwe na Karanja pamoja na TUKI (2009) wao wanatoa dhana ya Uambishaji pekee na wanashindwa kutoa dhana kamili ya Uambatizi hivyo kuzifanya dhana hizi kuendelea kuwa na mikanganyiko na kuwa telezi. Vile vile kuna wataalamu mbalimbali bado wanakinzana katika kuelezea dhana hizi. Kutokana na maelezo yao ninaweza kuthibitisha uambishaji ndio umegawanyika sehemu mbili ambazo ni Uambatizi na Unyambuzi, hivyo usahihi wa fasili za dhana hizi ni kuwa; Uambatizi ni mchakato unaohusu upachikaji wa viambishi tangulizi mwanzoni mwa mzizi wa neno ili kulipa nen hilo maana maalumu yaaani upatanisho wa kisarufi. Unyambuzi ni uwekaji viambishi fuatishi kwenye mzizi wa neno na tokeo lake ni kubadili aina ya neno mfano; msomi kutokana na kitenzi soma hivyo kile kinacholeta tofauti ni kinyambuzi na ni sharti kila nomino ziwe katika ngeli kwani nomino zenye sifa sifa moja zinazofanana huwekwa pamoja.Kila kinyambuzi kina maana yake.
  3. 3. fasili za dhana hizi mbili wapo wengine wanaochanganya dhana ya Uambishaji kuwa ni sawa na uambatizi kama alivyoeleza Rubanza na TUKI Kuna michakato au mifanyiko ya uambatizi kama vile; Nafsi; Nafsi hutazamwa kama kiima nafsi I, II na III ambapo katika tungo nafsi imegawanyika katika pande mbili yaani kiima kinaweza kuwa na viambishi kama ,ni-, -u-, -a-, -tu-, -m-,-wa- mfano; mtoto, utoto. Yambwa inaweza kuwa na viambishi kama vile ni- ku- m- tu- wa- ji –ni Ukanushi; katika ukanushi kuna viambishi kama vile ha----i, si----i mfano; hawalimi, sitaki Uhali; uambatizi wenye kuonesha uhali viambishi vyake ni kama vile po- ki- nge- ngali- ka- li- mfano; walipokula, Angekuja Unjeo; mchakato huu huonesha wakati tendo limetendeka. Katika mchakato huu viambishi vya vipo katika uyakinishi kama vile –li-, me-,-na, -ta-, mfano; Anakula, amekula, alikula atakula. Kiambishi na kinaonesha wakati uliopo, me inadokeza wakati uliopo katika hali timilifu li inadokeza wakati uliopita na ta wakati ujao. Vilevile kuna njeo inayodokeza ukanushi kama ku- ja i ta Idadi na wingi (viambishi ngeli): mchakato huu unaonesha makundi ya nomino yaani ngeli kama vile m-wa, ki- vi. Uambatizi huweza kufanyika katika aina mbalimbali za maneno kama ifuatavyo; Uambatizi huleta upatanisho wa kisarufi ; Upatanisho wa kisarufi hutokea kwani uambatizi huhusika na uambishaji kisarufi. Mofimu za aina moja za umoja na wingi na ambazo huleta upatanisho wa kisarufi wa namna moja katika vifungu. Hivyo maumbo yote yana upatanisho wa kisarufi. Mfano; Umoja wingi alomofu m-toto wa-toto m- wa- ki-ti vi-ti ki- vi- Økaka Økaka Ø- Ø- Uambatizi wa vitenzi; Katika uambatizi wa vitenzi upachikaji wa viambishi tangulizi ni vingi kwa mfano katika mzizi (pig-) Tu-ta-pig-a A-li-ye-pig-a Uambatizi hufuata kanuni maalumu kama vile mofimu ya mzizi katika kitenzi
  4. 4. Uambatizi wa Vihusishi; Vihusishi huwa na dhima ya kuunganisha maneno. Mofimu mzizi ya maneno unganishi ni ( a-) mofimu tangulizi kadhaa huwekwa katika mzizi (-a ) mfano za , ya ,pa, la vinapotumika katika kuunganisha maneno kama vile pesa za shule, shamba la kaka. Ufanano wa uambatizi na unyambuzi ninaweza kusema kwamba yote ni matawi ya uambashaji kwa sababu uambatizi na unyambuzi huhusika na uwekaji na viambishi katika mzizi wa neno kwa kulingana nadhima mahususi ya kila moja kama ni kubadili kategoria ya neno nakuunda neno jipya au kuleta upatanisho wa kisarufi. Utofauti katika maana; Uambatizi ni utaratibu wa uwekaji wa viambishi kwenye mzizi wa neno ili kulipa neno hilo maana maalamu yaani kupachika viambishi vyenye dhima kisarufi wataalamu wengine huuita Uambishaji Kisarufi ambapo Unyambuzi ni uwekaji wa viambishi fuatishi kwenye mzizi wa neno na tokeo lake likiwa ni kubadili maana au kategoria ya neno.Mifano ya uambatizi ni kama vile; Wa-na-pig-a ambapo wa- inadokeza nafsi ya tatu wingi pia inadokeza ngeli ya wingi, na- inadokeza njeo ya wakati uliopo Uambatizi hufanana kimaana kila kila kiambishi kinapopachikwa ; Kiambishi –m huweza kuwa na sifa ya ufanano kwani kiambishi hiki huwa ni sehemu ya ngeli moja yaani huwa katika kundi moja kwa mfano; mke, mto , mtume, mti, mtoto Hatuorodheshi viambishi kama leksimu, Hii ina maana kwamba mabadiliko ya kisarufi hatuyaingizi katika kamusi kwa mfano anacheza analima anapika. Uambatizi haubadili kategoria ya maana ya maneno; viambishi vinavyowekwa mwanzoni mwa mzizi wa neno hauwezi kubadili kategoria ya maneno kwani maneno huweza kuandikwa kwa aina mbalimbali japo mzizi wake hubaki kama ulivyo na bado maana ikabaki kama ilivyo mfano; kitenzi cheza A-na-chez-a , a-ta-chez-a a-li-chez-a hivyo basi maana ya neno haijabadilika. Uzalishaji wa vipashio unajitokeza mara nyingi; Katika uambatizi viambishi tangulizi huwa ni vingi ikilinganishwa na viambishi fuatizi, miifano ya viambishi katika uambatizi ni kama vile; Wa-na-o-chez-a, ni-si-ngali-m-pend-a viambishi ni Wa-,na,-o, ni-,si-,ngali-, na m- Michakato ya unyambuzi vile vile huwa kama ilivyo katika uambatizi utofauti wake upo kwamba unyambuzi huweza kubadili kategoria Unyambuzi hujihusisha na mabadiliko ya maana ya leksimu au aina za maneno, kwa mfano katika utaratibu wa kuunda nomino. Lugha ya Kiswahili huunda nomino nyingi kutokana na vitenzi, vivumishi.
  5. 5. Kwa mfano; Kitenzi Nomino Lima Kilimo penda mapendo Vilevile katika unyambuzi, nomino huweza kubadilika kategoria yake na kwenda katika vitenzi kwa mfano Nomino vitenzi Sababu Sababisha Makini Makinisha Maneno hufuatwa au kuundwa kwa utaratibu maalumu kwani sio kila kinominishi kinaweza kutumika kama kinyambuzi mfano tatuwezi kusema kitenzi lima kiwe Kilime Uzalishaji wa viambishi ni mchache ; katika unyambuzi vipashio vichache hupatikana ikilinganishwa na viambishi katika uambatizi . mfano wa viambishi vya unyambuzi Uambatizi unyambuzi a-li-ye-chez-a m-chez-o wa-li-o-fund-ish-a ma-fund-ish-o Kuna mabadiliko kidogo katika viambishi;Katika unyambuzi kuna mabadiliko kidogo ukilinganisha na uambatizi kwani viambishi huwa ni vya ngeli na kinominishi katika uambatizi viambishi hufanana kimaana kila kinapopachikwa Viambishi huweza kutofautiana kimaana viambishi vinapowekwa katika shina au mzizi mfano kiambishi fuatishi cha Kiingereza Vaporize, Hospitalize Winterize, kuandaa kwa majira ya baridi Unyambuzi hutokea baada ya mzizi wa neno; mahali ambapo hufanyika unyambuzi au unyambuaji wa maneno ni baada ya mzizi wa neno lenyewe kwani neno hunyumbuliwa ili kuzalishwa au kuunda neno jingine jipya. Unyambuzi huweza kuorodhesha katika kamusi, Katika kamusi maneno yaliyozalishwa yaani mapya huweza kuwa kama sehemu ya vidahizo katika kamusi kwa mfano neno Upendo, kilimo, msomi, kisomo, mchezo huweza kuwa kama vidahizo ikilinganishwa na vitenzi vyake katika uambatizi. Hivyo ninaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa kutokana na mikanganyiko juu ya ipi ni dhana sahihi ya Uambatizi na Unyambuzi ni vema kuelewa pia dhana halisi ya Uambishaji kama ilivyojadiliwa katika kazi hii kwani kutokana na uambishaji ndio tunaweza kupata uambatizi na unyambuzi.
  6. 6. MAREJELEO Massamba D.P.B. na Wenzake (2009) Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA) Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar se Salaam Massamba, D.P.B. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Taaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es salaam. Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es- Salaam. Habwe, J. and Karanja, P (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi, Phonix Publishers Rubanza Y, (1996) Mofolojia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es- Salaam.

×