SlideShare a Scribd company logo
1 of 24
Download to read offline
ULIMWENGU WA SIKOSELI . AFYA
MAISHA NA MATUKIO . BURUDANI
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
ULIMWENGU
WA SIKOSELI
01
|
MAUDHUI
|
|
03
MATUKIO
02
JARIDA LA SHUJAA
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
MITINDO YA
MAISHA
04
DONDOO
ZAAFYA
|
MHARIRI
|
UJUMBE WA MHARIRI:
“Sikoseli sio ugonjwa wa kurogwa” hayo ni maneno ya Bi. Fatuma Ubwa, Jarida la Shujaa ni ndoto yetu sote katika
jumuiya ya Sikoseli, Kupata nafasi ya kukaribisha dunia yetu kushiriki na kujifunza mengi kuhusu ugonjwa wa sikoseli,
Tunapotamka neno, “Ugonjwa” Kila mmoja wetu anakimbilia udhaifu, kama wahariri wa jarida hili la SHUJAA
lengo letu kuu ni kuchora picha chanya juu ya sikoseli, ndio maana ukiendelea kusoma jarida hili utaona kuwa
kuna stori za mashujaa kama, Aboubakari Kilaza ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Flava;
ambao wanakupa motisha na kuhimiza kuwa Sikoseli haikuzuii kuishi Maisha ya kawaida na kutimiza ndoto zako.
Utakutana na muigizaji wa Bongo Movies Thadeus al-maaruf kama shetani wa mguu mmoja, yeye anatuhimiza
kutokata tamaa pamoja na changamoto za kiafya alizopata, hadithi yake ni dhahiri kuwa ni hadithi ya ushindi.
|
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
Ndani ya Jarida pia utajifunza
kuhusu afya, mitindo ya Maisha
na pia utapata taarifa muhimu
kwa yale yanayojiri katika
ulimwengu wetu wa Sikoseli.
Lengo kuu la Jarida hili ni
kuwafungulia dunia wanajamii
wa sikoseli kuwawezesha kupata
chombo ambacho kitawawezesha
kupaza sauti yao na kuufikia
ulimwengu kwa ujumla.
Tunapenda kutoa shukrani za
dhati kwa waandaji wote na timu
nzima iliyoshiriki
katika kuwezesha jarida hili
kukamilika.
Ni matumaini yetu kuwa
utalipokea na kulisoma kwa
mikono miwili jarida
hili la SHUJAA.
Kuwa Mjanja Ijue Sikoseli.
Arafa Salim.
Emmy Mwita.
_
_
SIKU YA SIKOSELI DUNIANI
K
01
|
wanza tuelekee Arusha, ambapo kwa
mara ya kwanza maadhimisho hayo
yaliadhimishwa jijini huko Kitaifa
katika Hospitali kuu ya jiji la Arusha ya
Mount Meru Referral Regional Hospital;
Mgeni Rasmi akiwa Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe
kwa niaba ya Naibu Waziri Dkt. Godwin Mollel,
Jumuiya ya Watu Wenye Sikoseli Tanzania
iliwakilishwa na wajumbe wao kutoka
Sickle Cell Community group, ambapo
walishiriki katika matembezi ya kilomita 1,
yaliyoanzia ofisi ya Halmashauri ya Manispaa
ya jiji la Arusha na kumalizika katika Hospitali
ya Mount Meru; Na baada ya hapo utambulisho
na hotuba kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe na wageni
muhimu waalikwa,
Ikifuatiwa na tukio maalum
la uzinduzi wa kliniki mpya ya sikoseli
Hospitalini hapo ikiwa ni jambo la kheri kwa
watu wenye sikoseli maana watapata huduma
kwa ukaribu zaidi na pia itasaidia kuepuka
gharama za kuhudhuria kliniki binafsi.
Pia maadhimisho hayo yalipambwa
na risala na shuhuda kutoka kwa watu wenye
sikoseli waliohudhuria ambapo walipata
kushirikisha adhara juu ya safari zao kama watu
wanaoishi na sikoseli na kutoa hamasa na
ufahamu kwa hadhara.
Kila mwaka, juni 19 ni siku maalum kwa jamii ya sikoseli duniani kama ilivyoazimiwa na umoja wa mataifa
mwaka 2004 kila siku ya tarehe 19 itakua siku ya uhamasishaji na ufahamu wa sikoseli duniani. Hivyo kila mwaka,
juni 19, jamii ya kimataifa ya sikoseli inaungana kuadhimisha, kutoa elimu na uelewa juu ya sikoseli.
Leo tutatazama yaliyojiri katika maadhimisho ya siku ya sikoseli duniani, nchini Tanzania. Tutaangalia matukio na
taarifa kutoka mikoa mbalimbali ambazo ziliadhimisha siku hiyo rasmi ambayo ni Juni 19, 2022.
|
ULIMWENGU WA SIKOSELI
JUNI 19,
|
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
Kutoka Bara tunavuka bahari hadi visiwani Zanzibar ambapo nao hawakuachwa nyuma katika maadhimisho
hayo kwani siku ya Tarehe 17 Juni 2022 waliadhimisha siku ya sikoseli duniani katika Hospitali ya rufaa
ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Maadhimisho hayo yalifana huku yakiwaleta pamoja wana jumuiya wote wa Sikoseli
kisiwani hapo pamoja na watoa huduma za afya.
|
|
|
|
SIKU YA SIKOSELI DUNIANI
01
|
ULIMWENGU WA SIKOSELI
JUNI 19,
|
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
|
K
utoka Zanzibar tunaelekea hadi Pwani, Bagamoyo ambapo Sickle Cell Disease Patients' Community of
Tanzania iliandaa maadhimisho ya siku ya sikoseli duniani kushirikiana na hospitali ya wilaya ya Bagamoyo,
siku ya Tarehe 25 Juni, 2022. Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwambao,
wilayani Bagamoyo; Mgeni rasmi akiwa Mheshimiwa Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo Bw. Majid Mhina.
Sherehe hizi zilifana kwa burudani kutoka kwa vikundi vya waaigizaji na wasanii wa ngoma za asili Bagamoyo pamoja
na Elimu ya somo la Lishe Bora kutoka kwa mtaalamu wa Lishe na Afya Bora; ikifuatiwa na hotuba kutoka wa mgeni
rasmi Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Bagamoyo Bw. Majid Mhina na uzinduzi rasmi wa kliniki ya sikoseli wilayani
Bagamoyo.
Ziada ya hayo kulikuwa na upimaji wa uviko pamoja na elimu ya afya ya kinywa kutoka Colgate, vilevile ugawaji wa
kitabu cha Amana Shujaa wa Sikoseli kilichoandikwa na Bi. Arafa Said huku tukio hilo likiambatana na ushuhuda
kutoka kwa shujaa mwenye umri wa miaka 70, akieleza ni jinsi gani ameweza kuishi na kustahimili adha za ugonjwa
huo hadi kufikia miaka hiyo 70 huku akivunja Imani potofu za kuwa mtu mwenye sikoseli hawezi kuishi zaidi ya
miaka mitano au kupata mafanikio katika Maisha. Tafrija hizi zikiwa ni kilele cha maadhimisho ya sikoseli duniani
nchini Tanzania, zillfika kikomo mida ya jioni.
|
| |
|
|
SIKU YA SIKOSELI DUNIANI
01
|
ULIMWENGU WA SIKOSELI
JUNI 19,
|
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
SERIKALI YAWAFUTA MACHOZI
YA MIAKA MINGI WATU WAIISHIO NA SIKOSELI
ama umewahi kusikia au unafahamu kuhusu dawa ya hydroxyurea utakuwa pia unatambua umuhimu wake
kwa watu wenye sikoseli katika kuhakikisha kuwa wanaishi Maisha yenye ubora na afya kwa kupunguza
dalili hatarishi zinazosababishwa na ugonjwa wa sikoseli.Hivi karibuni katika kongamano la Kisayansi
lililofanyika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
K
Prof. Abel Makubi akiwa mojawapo ya wageni rasmi aliahidi
kushughulikia suala hilo na kulikamilisha haraka hii
ni katika kuhakikisha utekelezaji wa mojawapo ya sera za wizara ya
afya Tanzania ikiwa pamoja na kuboresha huduma za afya kwa watu
wenye sikoseli nchini. Mheshimiwa wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Prof. Abel Makubi aliagiza hayo wakati alipokiwa anahitimisha
kongamano la saba la kisayansi, chuo kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS).Nukuu ya Mheshimiwa
Prof. Abel Makubi, “NHIF hakikisheni mnatekeleza hili,
hivi vidonge vipatikane kwenye vifurushi vyote vya bima,
mnipe majibu mapema mlipofikia, ili tufanye maamuzi”
Aliagiza Mheshimiwa wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Prof. Abel Makubi.
Pia Mhe. Katibu Mkuu, Aliongeza kwa kusema kuwa suala hilo,
kuhusu upatikanaji wa Hydroxyurea litazamwe na kushughulikiwa
kwa uzito kwani Dawa ya Hydroxyurea ni muhimu kutokana na
Kwamba watu wengi wenye sikoseli wanaishi katika Maisha ya
kupata maumivu mara kwa mara na dawa ya hydroxyurea inawasaidia kupunguza dalili nyingi zingi zinazosaba-
bishwa na sikoseli ikiwemo pamoja na kupunguza hali ya kuishiwa damu; na ukosekanaji wa dawa hiyo katika
vifurushi vya mfuko wa Afya wa NHIF unawalazimu wanajamii ya sikoseli kulipia gharama ambazo wengi hawa-
zimudu kwa ajili ya kupata Hydroxyurea kwa matibabu yao. Mheshimiwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Prof. Abel Makubi aliongeza kwa kusema, “Tuangalie jinsi ya kusaidia wagonjwa hawa katika hili, hukabiliwa
na maumivu makali, wanaishiwa damu lakini dawa hii inawasaidia kuwapunguzia hayo” mwisho wa nukuu.
Jarida la Shujaa linatumaini kuwa habari hii ni furaha kwa jamii nzima
ya sikoseli kwani baada ya kilio na changamoto za muda mrefu katika
upatikanaji wa dawa ya Hydroxyurea sasa wahusika wote wenye
Bima ya NHIF wanaweza kupata dawa hiyo bila malipo katika vituo vya
Afya; Habari hii inaleta mawanga na matumaini ya kuishi Maisha bora
na afya tele bila masumbuko kwa watu wote wenye sikoseli nchini.
|
| |
|
|SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
01
|
ULIMWENGU WA SIKOSELI
|
U
Pia kutokana na uhaba wa upatikanaji wa huduma za afya na matibabu sahihi
kwa wagonjwa wa sikoseli bila kusaha gharama za juu za matibabu, hii inapelekea
asilimia kubwa ya watu wenye sikoseli kushindwa kumudu gharama za matibabu
katika vituo binafsi na kupelekea kufeli kupata matibabu sahihi hivyo afya zao
kuzorota kutokana na athari zinazoletwa na ugonjwa huo hivyo kupelekea wengi
wao kupoteza Maisha katika umri mdogo kwasababu ya kukosa uangalizi wa
mapema.
Kwa miaka mingi jamii ya sikoseli ukijumuisha na wanaharakati wa sikoseli
wamekua wakipaza sauti juu ya umuhimu wa upatikanaji wa huduma bora na
matibabu sahihi kwa wanajamii ya sikoseli ili kuongeza ubora wa Maisha na
afya zao. Hatimaye serikali kushirikiana na washika dau mbalimbali katika
sekta ya afya walisikia vilio vyao na toka mwaka 2007 mpaka sasa, kumekua
ongezeko la kliniki mpya za sikoseli katika vituo vya afya vya ngazi ya msingi,
wilaya na hata Taifa kwa ajili ya uangalizi wa karibu kwa watu wenye sikoseli.
Nikiongeza, na kwa mwaka 2022 Jarida letu lingependa kukuhabarisha kuwa sasa
wigo wa huduma za afya kwa watu wenye sikoseli unazidi kutanuka na kukukua
kwani kuacha kliniki za Mloganzila, Mwananyamala, Temeke na Kliniki iliyopo
Hospitali ya Taifa Muhimbili, serikali yetu kupitia wizara ya Afya imeongeza kliniki
nyingine mpya, hii ikiwemo Kliniki ya Sikoseli mkoani Kilimanjaro katika Hospitali
ya KCMC, tunapenda kuwahabarisha wanajamii wa sikoseli waliopo Moshi,
Kilimanjaro kuwa sasa huduma za afya kwao zimesogezwa karibu kabisa, kwani
kuna kliniki mpya ya sikoseli, katika jingo la Hemophilia Center, Kitengo cha
matibabu ya saratani.
Pia bila kusahau kuwa mwezi huu siku ya maadhimisho ya
sikoseli duniani, jijini Arusha katika Hospitali ya jiji Mount Meru, Mheshimiwa
Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Afya Dkt. Shekalaghe alizindua kliniki mpya
ya sikoseli katika Hospitali hiyo Kongwe, tukielekea mkoani Pwani, Wilayani
Bagamoyo napo hawakuwa nyuma katika harakati hizi, Mheshimiwa Kaimu
Mkurugenzi wilaya ya Bagamoyo, Pwani alikata utepe na kufungua rasmi Kliniki ya
Sikoseli Bagamoyo na Kuagiza kuwa wapewe ushirikiano na Halmashauri ya
Wilaya ya Bagamoyo, hii ni pamoja na uangalizi na upatikanaji wa vifaa tiba.
Tukifunga kurasa hii, Tunaweza kusema, “Harakati za sikoseli Tanzania, Kumenoga
” Ni matumaini yetu kuwa uwepo wa kliniki hizi utapunguza adha waliyokuwa
wakipitia wagonjwa wengi wa sikoseli mikoani nan je ya jiji la Dar es Salaam kwa
kusafiri umbali ili kupata matibabu au kulazimika kuhudhuria matibabu katika vituo
binafsi hivyo kubeba mzigo mkubwa wa gharama za matibabu na pia hatua hii
itapelekea kupunguza vifo vya awali vya wagonjwa wa sikoseli.
Shujaa ingependa kuendelea kuwahasa na kusisitiza wanajamii wa sikoseli
kuhudhuria kliniki hizi ili kupata matibabu sahihi na endelevu, pia kwa serikali
yetu tukufu tunasema, “shukrani na kazi iendelee”
|
UZINDUZI WA KLINIKI ZA SIKOSELI KWA
MWAKA 2022.
01
|
ULIMWENGU WA SIKOSELI
|
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
gonjwa wa Sikoseli ni ugonjwa wa kurithi ambao unaathiri seli hai nyekundu za damu na kubadili umbo lake kutoka
katika umbo la kawaida la donati na kuipa seli hai nyekundu umbo la ndizi au mundu hii hutokana na upungufu wa
oksijeni, protini katika Hemoglobin ya seli; Hivyo hali hii inapelekea mtu kupata dalili kama maumivu makali ya
viungo na hata hali ya kupungukiwa damu (anemia).
Tafiti zinaonesha kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazoongoza katika chati ya dunia kwa kuwa na asilimia kubwa ya
watu wenye sikoseli ikishika nafasi ya nne; Pia tafiti zinaonesha kuwa kila mwaka Watoto 11,000 huzaliwa na sikoseli nchini,
Tanzania. Pia makadirio yanaonesha karibu asilimia 20% ya watanzania wanazaliwa na vinasaba vya sikoseli;
|
|
W
WARSHA YA CONSA
(CONSORTIUM OF NEWBORN SCREENING IN AFRICA)
02
|
MATUKIO
|
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
arsha hii ilifanyika Juni 22, 2022 kuanzia saa tatu asubuhi
mpaka saa tisa alasiri katika ukumbi wa kampasi ya chuo
cha MUHAS; Ilijumuisha watoa huduma ya afya pamoja
na kitengo cha Sikoseli MUHAS, wazazi wote ambao wana
watoto wenye Sikoseli na waliogunduliwa kupitia kipimo
cha Newborn Screening.
Lengo la warsha hiyo likiwa ni kutoa elimu kwa wazazi hao
kupitia matabibu wenye ujuzi na weledi wa juu; Pia kuacha
elimu ya malezi kwa Watoto wenye Sikoseli walitoa elimu
juu ya umuhimu wa kuwa na bima ya Afya ya NHIF ili
kuwawezesha kupata huduma zote muhimu za matibabu na
kliniki kwa Watoto hao hivyo kuwapunguzia mzigo wa
gharama za kulipia kwa njia ya fedha.
Kuacha elimu iliyotolewa na wataalamu wa afya waalikwa,
wazazi walipata nafasi ya kueleza jamii juu ya safari zao
kama wazazi wa Watoto wenye Sikoseli na waliogundulika
katika umri mchanga na pia wazazi hao walieleza jinsi safari
hii ina milima na mabonde mengi na vile kuwa na mtoto
mwenye mahitaji maalum ni safari ya kuwa na Subira,
upendo na kuwa tayari kujifunza kila siku na kushirikiana
na asasi zilizopo na watoa huduma ili kuhakikisha malezi
ya mtoto yanapewa kipaumbele na anapata matibabu na
huduma sahihi za afya kwa ukuaji mzuri.
Huduma za vipimo vya Newborn Screening zinapatikana
katika vituo vya afya vya Amana, Temeke, Muhimbili na
Bugando nchini, Tanzania.
K
KONGAMANO LA SABA LA KISAYANSI,
CHUO KIKUU CHA MUHAS.
02
|
MATUKIO
|
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
ongamano la saba la kisayansi lililoandaliwa na wanazuoni na wataalamu wa tiba na sayansi wa chuo kikuu
cha Afya na Sayansi Shirikishi Mhumbili (MUHAS) na Kufanyika chuoni hapo siku ya Tarehe 26, Januari
2022 katika Kampasi kuu ya Dar-es-salaam; Lengo kuu ikiwa ni kujadili mwelekeo mpya wa nchi katika
kukabili ugonjwa wa sikoseli ambao unaathiri asilimia kubwa ya Watoto nchini, Tanzania.
Kongamano ilo lilishirikisha na kukutanisha washika dau mbalimbali katika sekta ya Afya na Sayansi, likijumuisha
Wizara ya Afya, wanazuoni na wakufunzi mbalimbali, watafiti katika sekta ya Afya, watoa huduma na Mfuko wa
Bima ya Afya NHIF pamoja na wengineo wengi. Mojawapo ya mambo yaliyozungumziwa ilikuwa ni pamoja na
utekelezaji wa sera ya bima ya afya pamoja na kujumuisha dawa ya Hydroxyurea katika vifurushi vya mfuko wa
Bima ya Afya Taifa, NHIF kwa faida ya wagonjwa wa sikoseli nchini.
Dkt. Agnes Jonathan, Daktari Bingwa wa Afya ya Jamii pamoja na kuwa Mratibu wa Mradi wa Sikoseli
(SPARCO, TANZANIA) MUHAS katika uwakilishi wake wa mada juu ya sikoseli alisema, tafiti zinaonesha kuwa
kadiri ya Watoto 11,000 huzaliwa na ugonjwa wa sikoseli, hivyo yeye kama mratibu wa mradi wa
SPARCO, TANZANIA pamoja na timu nzima wamefanikiwa kuwaingiza kwenye mfumo wa Tiba na ufuatiliaji wa
karibu katika matibabu ya kliniki ya sikoseli takribani Watoto 5000 na pia wamewapatia vitabu ambavyo vinabeba
taarifa zao muhimu za afya.
Dkt. Agnes Jonathan, aliongeza kuwa tafiti zinaonesha kuwa takribani asilimia 13 hadi 20 ya watanzania wamebeba
vinasaba vya ugonjwa wa sikoseli na asilimia iliyosalia bado hawajui hali zao.
Pia mojawapo ya wageni rasmi waalikwa alikua Mheshimiwa Prof. Abel Makubi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
ambapo alisisitiza juu ya umuhimu wa hydroxyurea kujumuishwa katika mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF
kwasababu ya umuhimu wa dawa hiyo kwa watu wenye sikoseli, Pia Mheshimiwa wa Prof. Abel Makubi, Katibu
Mkuu Wizara ya Afya aliongeza kwa kusema, “Tanzania inastahili iwe na kituo cha umahiri kwa upande wa sikoseli”
mwisho wa nukuu.
Taasisi ya Jumuiya ya Wagonjwa wa Sikoseli Tanzania (SCDPCT) nayo haikuachwa nyuma, ikiwakilishwa na
Mkurugenzi Mwanzilishi wake, Bi. Arafa Said; Akiwakilisha hoja juu ya umuhimu wa uboreshwaji huduma za afya
kwa watu wenye sikoseli Tanzania pia alichukua nafasi hiyo kuwaelimisha na kuzungumza juu ya, “Uzoefu na Maisha
ya wagonjwa wa sikoseli” akiwakilisha jumuiya ya wagonjwa wa sikoseli Tanzania.
Ni dhati kuwa Kongamano ilo la saba la Kisayansi lililoandaliwa na chuo kikuu cha MUHAS lilikuwa chachu ya
mabadiliko katika Tiba na Huduma za Afya kwa watu wenye Selimundu kwani Baada ya hapo,
Dawa za Hydroxyurea ziliweza kujumuishwa katika mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF, na sasa watu wote
wenye sikoseli wanaweza kupata dawa hizo bure bila kulipa gharama yeyote kupitia Bima ya NHIF.
M
MAONYESHO YA KAZI
YA WANAHARAKATI WA SIKOSELI TANZANIA
02
|
MATUKIO
|
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
aonesho ya vikundi vya wanaharakati wa sikoseli Tanzania yalifanyika Tarehe 28 Januari, 2022 katika kituo cha
Sickle Cell Centre, MUHAS. Maonesho hayo yaliandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Jumuiya ya wagonjwa
wa sikoseli Tanzania (SCDPCT) ikishirikiana na MUHAS Sickle Cell Program.
Lengo la maonesho likiwa ni kuwaleta pamoja wanaharakati wa Sikoseli nchini na kuwapa uwanja wa kuonesha
kazi zao na ufanisi walio nao katika kuhakikisha elimu na ufahamu juu ya Sikoseli unakuwepo nchini Tanzania.
Taasisi ya Jumuiya ya wagonjwa wa Sikoseli Tanzania (SCDPCT) ilipata nafasi ya kuonesha baadhi ya kazi zao
katika warsha hiyo ilifanyika katika kituo cha Sikoseli, MUHAS. Mojawapo ya Kazi zetu ambazo tulionesha
zilijuimusha vitabu vya SHUJAA na AMANA SHUJAA WA SIKOSELI na machapisho ya elimu ya Sikoseli,
hii ikijumuisha toleo la kwanza la kijitabu cha SAUTI YA SHUJAA ambapo ni mjumuisho wa masomo kuhusu
mambo mbalimbali ya Afya ambayo yanaathiri wagonjwa wa Sikoseli kwa ujumla. Pia tulipata nafasi ya kuonesha
kupitia picha Kampeni na Kazi za Kijamii ambazo Taasisi inafanya ili kueneza elimu na ufahamu wa Sikoseli katika
maeneo na mikoa mbalimbali Tanzania.
Lengo la kazi hizi zote ni kuhakikisha kuwa elimu na ufahamu juu ya ugonjwa wa sikoseli unafikia watanzania wote
na pia wanaharakati wa sikoseli wanapata fursa ya kuonesha kazi zao na kujumuika na jumuiya wa wenye Sikoseli
na kujua mahitaji yao ili kuwepo na maboresho kwa kipindi kijacho mbeleni.
Maonesho yalifika kilelel na wanavikundi pamoja na waalikwa walipata kujifunza na kuona kazi mbalimbali ambazo
vikundi hivyo vya wanaharakati na wajumbe wa jumuiya ya Sikoseli wanazifanya ili kukabiliana na changamoto
zilizopo katika jamii juu ya sikoseli na pia ili kuhakikisha dhana potofu zinapotea na kunakuwepo na uelewa,
ufahamu na elimu juu ya Sikoseli.
DONDOO MUHIMU ZA KUISHI NA
UGONJWA WA SIKOSELI
02
|
DONDOO ZA AFYA
|
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
Siko seli/seli mundu ni nini?
Siko seli ni ugonjwa wa kurithi unaosababisha
mabadiliko yasiyo ya kawaida katika umbo la
chembechembe nyekundu za damu.
Kwa kawaida chembe nyekundu za damu
zina umbo la mviringo
ambalo huzirahisishia kupita kwenye mishipa
midogo ya damu
ili kusafirisha hewa safi ya oxygen katika sehemu
mbalimbai za mwili.
Kwa mtu mwenye ugonjwa wa siko seli,
seli hizi huwa tofauti;
zinanata na zina umbo la mwezi mchanga (mundu).
Tanzania ni mojawapo kati ya nchi zenye
wagonjwa wengi wa siko seli
duniani ambapo inakadiriwa takribani watoto 11,000
huzaliwa na ugonjwa wa siko seli kila mwaka.
Pia inakadiriwa kuwa 12% hadi 20% ya watu wote nchi
wana vinasaba vya ugonjwa wa siko seli
(sickle cell trait), kutegemeana na eneo.
Dondoo Muhimu za kuishi na ugonjwa wa Siko seli.
a. Uchunguzi wa kiafya wa mara kwa mara ni muhimu kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja.
Wanapaswa kumuona daktari kila baada ya miezi miwili au mitatu
b. Watoto kuanzia mwaka mmoja mpaka mitano wanatakiwa kumwona daktari kila baada ya miezi mitatu
Kuzuia Maambukizi
c. Hakikisha watoto wanapata chanjo zote za kawaida
d. Watoto wapewe chanjo ya ziada ya kuzuia kichomi (Pneumococcal vaccine)
e. Watoto wote wenye umri chini ya miaka 6 wapatiwe dawa ya penicillin ili kujikinga na maambukizi
f. Hakikisha watoto wanakingwa na maambukizi ya malaria kwa kutumia chandarua chenye dawa
Zingatia Ushauri wa Kitaalamu
g. Watoto wanatakiwa kunywa maji ya kutosha wakati wote na wapewe mlo kamili, ukijumuisha matunda,
mbogamboga, vyakula vya kutia nguvu na vya kujenga mwili wa mtoto.
h. Watoto waepuke kukaa katika mazingira ya joto kali ama baridi sana
i. Watoto wajishungulishe na michezo mbalimbali ili wawe na furaha na afya njema,
wasicheze kiasi cha kuwachosha sana.
W
UMUHIMU WA LISHE BORA
KWA WENYE SIKOSELI
02
|
DONDOO ZA AFYA
|
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
agonjwa wengi wa sikoseli wanaweza kuwa na mwili mdogo lakini kuna hatari ya kuwa na unene uliopita
kiasi. Wanashauriwa kula vyakula vyenye kalori ya juu na vyenye virutubisho vingi tangu utotoni.
Lishe Bora; ni ile ambayo inajumuisha aina zote za vyakula ambavyo vina virutubisho vinavyohitajika mwilini.
Ili lishe iwe bora lazima sahani iwe na mjumuisho ufuatao: 1/4 iwe Wanga, 1/4 iwe Protini na 1/2 iwe na
vyakula vyenye Vitamini.
Sahani yako inatakiwa kuwa na Wanga (ugali, wali,mtama, mhogo, gimbi, viazi, ndizi etc), Protini, Vitamini A,
B6, C, D, E na virutubisho vingine vidogo kama zinki, kalsiamu na magnesiamu. Lishe bora ni muhimu katika
kuongeza chembe za damu, kuimarisha mifupa, kuupa
mwili nguvu na kuongeza kinga ya mwili.
Ili kuhakikisha kuwa unapata lishe bora katika mlo wako wa kila siku ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo;
Angalau sahani yako iwe na aina 1 ya Protini na mboga
na matunda (chakula kimoja kinaweza kuwa na
kirutubisho zaidi ya kimoja), kwa wale ambao ni
ngumu kuepuka kuongezewa damu mara kwa
mara wanashauriwa kupunguza vyakula vyenye
madini chuma kwa asilimia kubwa pia
unashauriwa kula vyakula vinavyotoka/
vinalimwa ardhini kwa njia ya asili
(organic foods) hivyo ni bora zaidi ya
vile vya viwandani na vinavyochakatwa
kupita kiasi. Bila kusahau umuhimu wa
maji katika mmeng'enyo wa chakula,
usafirisha virutubisho katika mwili,
msukumo mzuri wa damu.
Unashauriwa glasi 8 sawa na
Lita 2 au 3 kwa siku.
Watu wengi wanashindwa kula lishe bora kutokana
na kuwa na uhusiano mbovu na vyakula;
Lishe bora ni vile unavyopangilia
sahani yako na virutubisho utakavyoweka.
Makala hii ya Lishe Bora
imenukuliwa kutoka katika chapisho la kwanza
la SAUTI YA SHUJAA, somo ambalo
lilitolewa na Dkt. Victoria Msambichaka,
mtaalamu wa lishe kutoka
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
|
“HUU SI UGONJWA
WA KUROGWA”
03
|
MITINDO YA MAISHA
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
“Ninaishi na Siko Seli miaka 70 sasa.
Nikiwa na miaka 15 nilianza kuugua mara kwa mara,
awali haikujulikana tatizo langu nini, nilikuwa naishiwa
damu mara kwa mara, nalazwa kuna nyakati pia niliongezewa maji,”
anasimulia.
“HUU SI UGONJWA
WA KUROGWA”
03
|
MITINDO YA MAISHA
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
“Ninaishi na Siko Seli miaka 70 sasa.
Nikiwa na miaka 15 nilianza kuugua mara kwa mara, awali haikujulikana tatizo langu nini, nilikuwa naishiwa
damu mara kwa mara, nalazwa kuna nyakati pia niliongezewa maji,” anasimulia.
Jamii imegubikwa na dhana nyingi potofu juu ya ugonjwa huu, wengi hukimbilia kwa waganga wa kienyeji
wakiamini wamerogwa au kukumbwa na pepo wabaya; Pamoja na hao wapo wengine ambao huamini mgonjwa
wa Siko Seli hawezi kuishi zaidi ya miaka 18.
Lakini maisha ya Fatuma Ubwa, Mkazi wa Bagamoyo mkoani hapa ni ushuhuda tosha kwamba mtizamo huo
si sahihi. Mwanamama huyo Juni, mwaka huu amesherehekea miaka 70 ya kuzaliwa kwake, ni mgonjwa wa
Siko Seli.
Zaidi anasimulia....
“Nikiwa na miaka 15 nilianza kuugua mara kwa mara, awali haikujulikana tatizo langu nini, nilikuwa naishiwa
damu mara kwa mara, nalazwa kuna nyakati pia niliongezewa maji,” anasimulia.
Anasema kutokana na hali hiyo wazazi wake walihisi amerogwa na wapo wanajamii ambao walishauri apelekwe
haraka kwa wataalamu {waganga wa kienyeji akatibiwe huko}.
“Lakini baba yangu alikataa, hivyo niliendelea kupelekwa hospitalini na huko baadae niligundulika nina Siko Seli.
Hivyo, nimezaliwa na Siko Seli, naishi nayo kwa miaka 70 sasa.”
Anasema amejaliwa kupata watoto wanne ambao wao hawana Siko Seli, vile vile amejaliwa wajukuu kadhaa
ambao nao hawana ugonjwa huu.
Uso wake umejaa tabasamu, kila anaposimulia simulizi yake wengi huvutiwa na kustaajabu namna gani ameweza
kumudu kuishi nao kwa miaka yote hiyo?
Anasema wazazi wake walizingatia kumpeleka kliniki kila alipohitajika na kwamba ameishi hivyo akizingatia
maelekezo anayopatiwa na wataalamu wa afya.
Fatuma anaongeza “Siko Seli si ugonjwa wa kurogwa, hautokani na uchawi… mtu anazaliwa nao pale anapokuwa
amerithi vinasaba kutoka kwa wazazi wetu wote wawili {baba na mama}; Tusiuone ni kitu cha ajabu au ugonjwa
wa ajabu ni wa kawaida tu, Mungu keshatupa tunapokea,” anatoa rai.
Anasema watu wasiwe na wasiwasi kuhusu ugonjwa huo, huku akishauri
“Ukimuona mtoto wako {ana ugonjwa huu} mpeleke hospitali afuatiliwe afya/hali yake ili apatiwe tiba stahiki na
elimu ni jambo la msingi hakikisha unampeleka shule kama watoto wengine.
Anaongeza “Kuna watu wapo kazini na wana Siko Seli na mimi nilisoma mpaka 'form two' {kidato cha pili}
Shule ya Sekondari Miembe Saba.
“Zamani shule zilikuwa mbali za sekondari, lakini nilishindwa kuendelea Siko Seli ilinizidi sana; Na nina uchungu
sana kwa sababu nilishindwa kumaliza lakini napenda sana, nilitamani niendelee lakini ndiyo hivyo ilinibana sana,”
anasema.
Shujaa huyo wa Siko Seli anasisitiza “Nawaombeeni dua mlio na matatizo haya mpone,
muendelee na kazi zenu vizuri.”
“Madaktari wangu wote nawaombea, mnanisikiliza vizuri, mnanitibia vizuri, nashukuru Mungu kwa hilo.”
_
MAISHA, SANAA
NA SIKOSELI
03
|
MITINDO YA MAISHA
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
Martin Deus Theo al maarufu Shetani wa mguu mmoja au unaweza
kumuita Chiba Kismati ni kijana wa umri wa miaka 36, alizaliwa
mpanda Agosti 1985 na alipofika umri wa miaka 2, wazazi wake
waligundua kuwa ana sikoseli, taarifa ambazo walizipokea
kwa ugumu kutokana na kwamba waliambiwa kuwa
ugonjwa huo hauna tiba na mwanao asingeweza
kuishi kupita miaka 18.
Chiba Kismati anatoa simulizi yake kwa jarida la shujaa
kwa kuongeza kuwa, baada ya wazazi wake kuambiwa
kuwa asingeweza kupona na kuwa asingeishi kwa zaidi ya
miaka 18, walichukua maamuzi ya kugeukia kwenye tiba za
Kienyeji ambapo alipelekwa kwa waganga mbalimbali, mikoa
tofauti tofauti nchini huku akipewa tiba za madawa ya kienyeji
kwa ahadi ya kuwa dawa hizo zingetibu na kuondoa ugonjwa huo
wa Sikoseli, anasema kuwa alitumia tiba za ajabu ambazo haziku-
saidia bali zilizidi kudhoofisha afya yake, mfano kuna wakati
alishauriwa kutumia kinyesi kilichokauka kwa madai ya ku-
wa ni tiba ya sikoseli. Haya yote yalitokea kutokana na kw-
amba yeye pamoja na wazazi wake hawakuwa na ufahamu
na elimu ya sikoseli.
Sikoseli iliathiri Maisha yake katika Nyanja kama elimu, ali-
shindwa kuendelea na elimu kutokana na kuumwa kwa vipindi
vya mda mrefu hadi miezi 6, hivyo ilimlazimu kusitisha elimu
yake pale alipofika kidato cha saba ndio ikawa kikomo kwake
lakini pia anasema kutokana na kupata vidonda katika mguu am-
bacho kilipelekea yeye kupata osteomyelitis na kupelekea kupot-
eza mguu kutokana na maambukizi hayo ya mifupa. Baadae aliha-
ma kutoka mpanda na kuhamia Dar es salaam ambapo alikua anapata
matibabu katika kliniki ya Watoto pale Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika Kukua kwake anasema alihisi kama watu walikua wanampuuza
aswa kutokana na kuwa na ulemavu wa mguu, yeye kama msanii wa
sanaa ya uigizaji inakua ngumu kupata kazi na pia kutokana na changa-
moto za afya na pia kukosa elimu kulipelekea Maisha yake kuwa duni ku-
tokana na kukosa kazi na hivyo akaamua kuingia katika tasnia ya uigizaji
lakini na huko pia alipata changamoto kutokana na hali yake ya ulemavu.
Chiba anakanusha kauli ya kuwa mtu mwenye sikoseli hawezi kuishi miaka zaidi ya 18 kwa
kusema kuwa, yeye ana miaka 36 na yupo, anahimiza kikubwa ni kupata elimu na kuzingatia
ushauri wa madaktari na lishe bora na kuepuka kazi nzito kupita kiasi; anatoa ushauri kuwa inawez-
ekana kuishi miaka zaidi ya miaka 70 pia anahimiza kuwepo semina mkoa kwa mkoa, nchini.
Pamoja na kuwa na sikoseli anasema hawezi kukata tamaa kwani anatumia fursa za usanii katika kuelimisha umma
kuhusu sikoseli na pia yeye ni baba wa familia na anategemewa kama kichwa cha familia yake hivyo sikoseli haija-
mzuia kuwa na Maisha mazuri. Anafuatilia matibabu kwa kuhudhuria kliniki, anazingatia lishe bora pamoja na kan-
uni za afya, anashukuru madaktari, jumuiya ya Sikoseli Tanzania. Inaendelea...
_
KUWA MJANJA IJUE SIKOSELI NA
KILAZA
03
|
MITINDO YA MAISHA
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
Aboubakar Juma Kilaza, Miaka 35 ni Msanii wa Muziki wa Bongo Flava; Alizaliwa
na Sikoseli na kwasababu wazazi walipata elimu kuhusu Sikoseli kwasababu Mama ya-
ke alikua ni muuguzi na Baba yake alikua ni muuguzi; kutokana na kwamba wazazi wa-
ke walikua na ufahamu wa sikoseli walijitoa katika yeye kupata matibabu, walihangaika
katika zahanati mbalimbali kutafuta matibabu na hatimae walifika Hospitali ya Taifa
Muhimbili, hapo ndipo alipopata matibabu yake na kuanza kliniki ya sikoseli.Kuwa
na Sikoseli hakukufanya ajione tofauti na Watoto wengine, isipokuwa aliku-
wa anahitajika kumeza dawa kama Folics Acid na Pen V kila siku na kuhu-
dhuria kliniki.
Alizidi kukua na kuelewa hadi kupelekea yeye kuwa balozi wa Sikoseli
Tanzania. Anasema kwa ujumla hajaathiriwa na sikoseli kabisa kwani
Sikoseli kwake imekua kama fursa ya kuwa kijana mwadilifu na kuepu-
ka makundi kama ya wavuta bangi na mambo ambayo yanaenda kin-
yume na jamii na pia kwakuwa anafanya kazi za sanaa Sikoseli ina-
mpa fursa ya kutumia sanaa yake katika kuhamasisha umma kuhusu
Sikoseli. Yeye kama msanii anawakilisha na kuelimisha kuhusu si-
koseli kwenye nyimbo anazotunga na anapenda kujulikana kwa
jina la Mr. Sickle Cell Kila nyimbo anayotoa anaweka jina hilo
kama utambulisho.
Anasema yeye hawezi kuonekana dhaifu kwa kuwa familia y-
ake anaiendesha mwenyewe, anaongeza kusema kuwa Sikos-
eli haimfanyi kuwa dhaifu kwani hata bila Sikoseli mtu una-
weza kuwa dhaifu.Anahudhuria kliniki na anafurahishwa na hu-
duma zinazotolewa lakini pia anaomba serikali pamoja na jamii itambue Si-
koseli na washirikiane katika kuboresha na kuimarisha huduma za matiba-
bu ya Sikoseli.
...jumuiya ya Sikoseli Tanzania. Inaendelea...
Lengo kuu la kuwa na taasisi ya Chiba Kismati ni kutoa fursa na jukwaa kwa wasanii wenye ulemavu na
kuondoa matabaka na unyanyapaa uliopo. Yupo kwa ajili ya jamii na kwa lengo la kujitoa kwa jamii.
Anategemea kutoa elimu zaidi kupitia taasisi yake ya chiba kismati; kuanzia mikoa ya Arusha, Tanga,
Pwani na Zanzibar. Anaomba serikali kuangalia watu wenye sikoseli kwasababu ugonjwa ni wa mda mrefu,
anaomba wizara husika iwasaidie katika kup-unguza gaharama za matibabu na kuwajumuisha katika bima.
Matarajio yake ni kutumia sanaa yake kufikisha ujumbe kwa wanajamii kuhusu Sikoseli. changamoto ni
kukosa miundombinu na rasilimali za kuwezesha kazi hiyo ya uhamasishaji.
Ujumbe wake kwa jamii, wasikatishe watu wenye sikoseli tamaa na kusema kuwa hawawezi kuishi
mda mrefu kwani yeye ni mfano tosha kuwa ameishi mpaka sasa ana miaka 36, na wengine wengi
wenye miaka 60, 70, 90 na kuendelea; Pia anawahasa wanajamii ya sikoseli wasitumie sikoseli kama
kudeka na kurahisisha Maisha yao, wafanye kazi zao kwa bidii na vizuri kwani Sikoseli ni ugonjwa
kama mengine tu.
SEPTEMBA, MWEZI WA
UELEWA WA SIKOSELI.
03
|
MITINDO YA MAISHA
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
Kwa wasiojua na kwa faida ya wanajua sio mbaya tukikumbushana kuwa mwezi wa septemba ni mwezi wa kutoa
uelewa na ufahamu juu ya ugonjwa wa Sikoseli duniani. Hivyo Taasisi ya Sickle Cell Disease Patients' of Tanzania
kuungana na taasisi na jumuiya kimaifa iliadhimisha siku hiyo kwa kuandaa matukio mbalimbai ya uhamasishaji,
uelimishaji na kutoa uelewa juu ya ugonjwa wa sikoseli nchini ikishirikiana na taasisi na washika dau katika sekta
ya afya. Kama jumuiya ya wagonjwa wa sikoseli Tanzania na kama wanaharakati na washika dau katika elimu na
ufahamu juu ya sikoseli waliandaa Jukwaa la Mashujaa mkoani Pwani, wilaya ya Mkuranga kushirikiana na Hos-
pitali ya Wilaya Mkuranga lengo kuu la jukwaa hili likiwa ni kutoa fursa ya majadiliano ya wazi kati ya wanajam-
ii wa mkuranga na wataalamu wa afya kuhusu Sikoseli na pia wataalamu waliruhusu wasaa wa maswali na majib-
u ambapo changamoto mbalimbali na Imani potofu zinazozunguka ugonjwa wa sikoseli zilijadiliwa na kutolewa
majibu sahihi ili kuelimisha wahudhuriaji; pia wahudumu walitoa fursa ya ushauri nasaha kwa mtu mmoja mmoja.
Tamasha la Jukwaa la Mashujaa lilifuatiwa na tukio la mnamo tarehe 27, Septemba ambapo taasisi ya SCDPCT
iliandaa Upimaji wa Sikoseli bure ikishirikiana na Hospitali ya Wilaya Bagamoyo na Zahanati ya Mwavi iliyopo
kata ya fukayosi, mkoani Pwani, upimaji huu uliambatana na ushauri na elimu juu ya sikoseli,
pia Sickle Cell Disease Patients' Community of Tanzania kushirikiana na wafadhili wake walifanikiwa kuwafadhili
bima Watoto walio chini ya umri wa miaka 16, Bima za afya za NHIF ili kuwasaidia kupata matibabu kwa gharama
rahisi na pia kuwahamasisha kuhudhuria kliniki za sikoseli kwa matibabu sahihi ili kuboresha afya zao.Mwezi
septemba ulifungwa na kampeni za sauti ya shujaa, ambapo tulipokea video mbalimbali kutoka kwa wanajamii,
madaktari na wauguzi, washirika katika sekta ya afya wakitoa elimu na ufahamu juu ya sikoseli kwa wanajamii
kupitia njia ya video.
Septemba ilinoga, tunakukumbusha na kuhamasisha kuwa usikose kushiriki harakati hizi kwa msimu mwingine
wa septemba yani mwaka 2023 kwani yajayo yanafurahisha.
CHANGIA DAMU,
OKOA MAISHA.
03
|
MITINDO YA MAISHA
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
Maji ni uhai lakini umewahi kukaa na kufikiri kuwa Damu ni uhai pia?
Tukizidi kuhimiza jamii juu ya umuhimu wa kuwa na ufahamu na uelewa wa sikoseli, tungependa kuwakumbusha
pia kuwa zaidi ya watu 100,000 uzaliwa na ugonjwa wa sikoseli kila mwaka na Tanzania ni mojawapo kati ya nchi
ambazo zinaongoza kwa kuwa na asilimia kubwa ya watu wenye sikoseli duniani.
Mgonjwa wa sikoseli anaweza kuhitaji mpaka uniti 100 za damu kwa mwaka kwa ajili ya matibabu ya athari zina-
zotokana na ugonjwa huo.
Hakuna aliyewahi kupungukiwa kwa kutoa na pia kutoa kutoka moyoni ni zawadi kwa muhitaji; kukosa damu ni
mojawapo ya sababu zinazochangia katika kupoteza Maisha kwa wagonjwa wengi wa sikoseli kwasababu kwao
damu ni uhai.
Unaweza kuwa mwokozi wa Maisha ya wengi kupitia kuchangia damu, unaweza kuokoa Maisha ya mtu aliyepata
ajali ya gari, mgonjwa wa saratani anayehitaji damu kwa matibabu yake, zaidi kwa wagonjwa wa sikoseli ambao
wanahitaji damu kwa Maisha yao yote ili kuishi.
Faida za kuchangia damu ni pamoja na kuchangia damu ni faida kwa moyo wa binadamu kwani kwa kuchangia
damu utaweza kuulinda moyo wako na maradhi ya moyo kama vile shinikizo na kuganda kwa damu. Pia utapata
kujua hali ya afya yako kupitia vipimo vinavyofanywa kabla ya kutoa damu, pia ni furaha kujua kuwa kupitia ku-
changia damu unaokoa Maisha ya wengi ni furaha ya kuishi na kujitoa kwa ajili ya wengine wenye uhitaji kwenye
jamii.
Kuchangia damu ni bure kabisa, hakuna malipo unaweza kuwa shujaa wa mtu kwa kuchangia dam una kuokoa
Maisha yake bure kabisa. Fikiria ni lini mara ya mwisho ulipata kutoa msaada bure bila kulipia gharama yeyote
bila kuhitajika shahada yeyote au ubunifu wowote.
Mwishoni niseme, unapochangia damu unaongeza mwaka mwingine wa Maisha kwa mpokeaji damu, unatoa siku
ingine ya Maisha, siku ingine ya sherehe ya kuzaliwa, zaidi unaongeza siku ingine chini ya usiku wa nyota uliojaa
tabasamu na afya, unatoa nafasi nyingine ya kutimiza ndoto na unatoa zawadi nyingine ya Maisha kwa wapendwa
wa mpokeaji damu.
Hivyo ni kuhimize changia damu, okoa Maisha…Timiza ndoto.
Umuhimu wa
Uchangiaji Damu
04 MATANGAZO
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
MATUKIO NA MAISHA
matukionamaisha.blogspot.com
Kwa habari na makala za
kina kuhusu masuala mbalimbali ya afya na
jamii tembelea jukwaa la
matukionamaisha.blogspot.com ni
akaunti iliyotambuliwa kwa tuzo na
Baraza la Habari Tanzania (MCT) mwaka 2021
jukwaa bora katika kuripoti masuala ya afya Tanzania,
Aidha Mmiliki wake Veronica Mrema mwaka 2021 alitunukiwa
tuzo na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa
Yasiyoambukiza Afrika Mashariki
miongoni mwa waandishi bora wanaoripoti vema.
04 MATANGAZO
SHU AA
JARIDA LA
J
Arafa
Na Arafa Said & Emmy Mwita
BLACKART
SHU AA
MAGAZINE
J
With Arafa Salim & Emmy Mwita
|
Meals on Wheel is a private
registered enterprise that
offers catering services for
more than three years now
Meals on Wheel works to make
any event or
meal time a delicious one
04 MATANGAZO
SHU AA
MAGAZINE
J
With Arafa Salim & Emmy Mwita
|
04 MATANGAZO
+255743222145
SHU AA
JARIDA LA
J
Na Arafa Said & Emmy Mwita
Ahsante kwa kusoma
Tufuatilie kupitia
IG: @sicklecellpatientstz
FB: Sickle Cell Disease Patients Community of Tanzania

More Related Content

Featured

How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthHow Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
ThinkNow
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Kurio // The Social Media Age(ncy)
 

Featured (20)

2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by Hubspot2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by Hubspot
 
Everything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTEverything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPT
 
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsProduct Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
 
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthHow Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
 
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfAI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
 
Skeleton Culture Code
Skeleton Culture CodeSkeleton Culture Code
Skeleton Culture Code
 
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
 
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
 
How to have difficult conversations
How to have difficult conversations How to have difficult conversations
How to have difficult conversations
 
Introduction to Data Science
Introduction to Data ScienceIntroduction to Data Science
Introduction to Data Science
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best Practices
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project management
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
 

JARIDA LA SHUJAA.pdf

  • 1. ULIMWENGU WA SIKOSELI . AFYA MAISHA NA MATUKIO . BURUDANI SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita
  • 2. ULIMWENGU WA SIKOSELI 01 | MAUDHUI | | 03 MATUKIO 02 JARIDA LA SHUJAA SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita MITINDO YA MAISHA 04 DONDOO ZAAFYA |
  • 3. MHARIRI | UJUMBE WA MHARIRI: “Sikoseli sio ugonjwa wa kurogwa” hayo ni maneno ya Bi. Fatuma Ubwa, Jarida la Shujaa ni ndoto yetu sote katika jumuiya ya Sikoseli, Kupata nafasi ya kukaribisha dunia yetu kushiriki na kujifunza mengi kuhusu ugonjwa wa sikoseli, Tunapotamka neno, “Ugonjwa” Kila mmoja wetu anakimbilia udhaifu, kama wahariri wa jarida hili la SHUJAA lengo letu kuu ni kuchora picha chanya juu ya sikoseli, ndio maana ukiendelea kusoma jarida hili utaona kuwa kuna stori za mashujaa kama, Aboubakari Kilaza ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Flava; ambao wanakupa motisha na kuhimiza kuwa Sikoseli haikuzuii kuishi Maisha ya kawaida na kutimiza ndoto zako. Utakutana na muigizaji wa Bongo Movies Thadeus al-maaruf kama shetani wa mguu mmoja, yeye anatuhimiza kutokata tamaa pamoja na changamoto za kiafya alizopata, hadithi yake ni dhahiri kuwa ni hadithi ya ushindi. | SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita Ndani ya Jarida pia utajifunza kuhusu afya, mitindo ya Maisha na pia utapata taarifa muhimu kwa yale yanayojiri katika ulimwengu wetu wa Sikoseli. Lengo kuu la Jarida hili ni kuwafungulia dunia wanajamii wa sikoseli kuwawezesha kupata chombo ambacho kitawawezesha kupaza sauti yao na kuufikia ulimwengu kwa ujumla. Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa waandaji wote na timu nzima iliyoshiriki katika kuwezesha jarida hili kukamilika. Ni matumaini yetu kuwa utalipokea na kulisoma kwa mikono miwili jarida hili la SHUJAA. Kuwa Mjanja Ijue Sikoseli. Arafa Salim. Emmy Mwita. _ _
  • 4. SIKU YA SIKOSELI DUNIANI K 01 | wanza tuelekee Arusha, ambapo kwa mara ya kwanza maadhimisho hayo yaliadhimishwa jijini huko Kitaifa katika Hospitali kuu ya jiji la Arusha ya Mount Meru Referral Regional Hospital; Mgeni Rasmi akiwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe kwa niaba ya Naibu Waziri Dkt. Godwin Mollel, Jumuiya ya Watu Wenye Sikoseli Tanzania iliwakilishwa na wajumbe wao kutoka Sickle Cell Community group, ambapo walishiriki katika matembezi ya kilomita 1, yaliyoanzia ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya jiji la Arusha na kumalizika katika Hospitali ya Mount Meru; Na baada ya hapo utambulisho na hotuba kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe na wageni muhimu waalikwa, Ikifuatiwa na tukio maalum la uzinduzi wa kliniki mpya ya sikoseli Hospitalini hapo ikiwa ni jambo la kheri kwa watu wenye sikoseli maana watapata huduma kwa ukaribu zaidi na pia itasaidia kuepuka gharama za kuhudhuria kliniki binafsi. Pia maadhimisho hayo yalipambwa na risala na shuhuda kutoka kwa watu wenye sikoseli waliohudhuria ambapo walipata kushirikisha adhara juu ya safari zao kama watu wanaoishi na sikoseli na kutoa hamasa na ufahamu kwa hadhara. Kila mwaka, juni 19 ni siku maalum kwa jamii ya sikoseli duniani kama ilivyoazimiwa na umoja wa mataifa mwaka 2004 kila siku ya tarehe 19 itakua siku ya uhamasishaji na ufahamu wa sikoseli duniani. Hivyo kila mwaka, juni 19, jamii ya kimataifa ya sikoseli inaungana kuadhimisha, kutoa elimu na uelewa juu ya sikoseli. Leo tutatazama yaliyojiri katika maadhimisho ya siku ya sikoseli duniani, nchini Tanzania. Tutaangalia matukio na taarifa kutoka mikoa mbalimbali ambazo ziliadhimisha siku hiyo rasmi ambayo ni Juni 19, 2022. | ULIMWENGU WA SIKOSELI JUNI 19, | SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita
  • 5. Kutoka Bara tunavuka bahari hadi visiwani Zanzibar ambapo nao hawakuachwa nyuma katika maadhimisho hayo kwani siku ya Tarehe 17 Juni 2022 waliadhimisha siku ya sikoseli duniani katika Hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Maadhimisho hayo yalifana huku yakiwaleta pamoja wana jumuiya wote wa Sikoseli kisiwani hapo pamoja na watoa huduma za afya. | | | | SIKU YA SIKOSELI DUNIANI 01 | ULIMWENGU WA SIKOSELI JUNI 19, | SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita
  • 6. | K utoka Zanzibar tunaelekea hadi Pwani, Bagamoyo ambapo Sickle Cell Disease Patients' Community of Tanzania iliandaa maadhimisho ya siku ya sikoseli duniani kushirikiana na hospitali ya wilaya ya Bagamoyo, siku ya Tarehe 25 Juni, 2022. Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwambao, wilayani Bagamoyo; Mgeni rasmi akiwa Mheshimiwa Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo Bw. Majid Mhina. Sherehe hizi zilifana kwa burudani kutoka kwa vikundi vya waaigizaji na wasanii wa ngoma za asili Bagamoyo pamoja na Elimu ya somo la Lishe Bora kutoka kwa mtaalamu wa Lishe na Afya Bora; ikifuatiwa na hotuba kutoka wa mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Bagamoyo Bw. Majid Mhina na uzinduzi rasmi wa kliniki ya sikoseli wilayani Bagamoyo. Ziada ya hayo kulikuwa na upimaji wa uviko pamoja na elimu ya afya ya kinywa kutoka Colgate, vilevile ugawaji wa kitabu cha Amana Shujaa wa Sikoseli kilichoandikwa na Bi. Arafa Said huku tukio hilo likiambatana na ushuhuda kutoka kwa shujaa mwenye umri wa miaka 70, akieleza ni jinsi gani ameweza kuishi na kustahimili adha za ugonjwa huo hadi kufikia miaka hiyo 70 huku akivunja Imani potofu za kuwa mtu mwenye sikoseli hawezi kuishi zaidi ya miaka mitano au kupata mafanikio katika Maisha. Tafrija hizi zikiwa ni kilele cha maadhimisho ya sikoseli duniani nchini Tanzania, zillfika kikomo mida ya jioni. | | | | | SIKU YA SIKOSELI DUNIANI 01 | ULIMWENGU WA SIKOSELI JUNI 19, | SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita
  • 7. SERIKALI YAWAFUTA MACHOZI YA MIAKA MINGI WATU WAIISHIO NA SIKOSELI ama umewahi kusikia au unafahamu kuhusu dawa ya hydroxyurea utakuwa pia unatambua umuhimu wake kwa watu wenye sikoseli katika kuhakikisha kuwa wanaishi Maisha yenye ubora na afya kwa kupunguza dalili hatarishi zinazosababishwa na ugonjwa wa sikoseli.Hivi karibuni katika kongamano la Kisayansi lililofanyika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, K Prof. Abel Makubi akiwa mojawapo ya wageni rasmi aliahidi kushughulikia suala hilo na kulikamilisha haraka hii ni katika kuhakikisha utekelezaji wa mojawapo ya sera za wizara ya afya Tanzania ikiwa pamoja na kuboresha huduma za afya kwa watu wenye sikoseli nchini. Mheshimiwa wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi aliagiza hayo wakati alipokiwa anahitimisha kongamano la saba la kisayansi, chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).Nukuu ya Mheshimiwa Prof. Abel Makubi, “NHIF hakikisheni mnatekeleza hili, hivi vidonge vipatikane kwenye vifurushi vyote vya bima, mnipe majibu mapema mlipofikia, ili tufanye maamuzi” Aliagiza Mheshimiwa wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi. Pia Mhe. Katibu Mkuu, Aliongeza kwa kusema kuwa suala hilo, kuhusu upatikanaji wa Hydroxyurea litazamwe na kushughulikiwa kwa uzito kwani Dawa ya Hydroxyurea ni muhimu kutokana na Kwamba watu wengi wenye sikoseli wanaishi katika Maisha ya kupata maumivu mara kwa mara na dawa ya hydroxyurea inawasaidia kupunguza dalili nyingi zingi zinazosaba- bishwa na sikoseli ikiwemo pamoja na kupunguza hali ya kuishiwa damu; na ukosekanaji wa dawa hiyo katika vifurushi vya mfuko wa Afya wa NHIF unawalazimu wanajamii ya sikoseli kulipia gharama ambazo wengi hawa- zimudu kwa ajili ya kupata Hydroxyurea kwa matibabu yao. Mheshimiwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi aliongeza kwa kusema, “Tuangalie jinsi ya kusaidia wagonjwa hawa katika hili, hukabiliwa na maumivu makali, wanaishiwa damu lakini dawa hii inawasaidia kuwapunguzia hayo” mwisho wa nukuu. Jarida la Shujaa linatumaini kuwa habari hii ni furaha kwa jamii nzima ya sikoseli kwani baada ya kilio na changamoto za muda mrefu katika upatikanaji wa dawa ya Hydroxyurea sasa wahusika wote wenye Bima ya NHIF wanaweza kupata dawa hiyo bila malipo katika vituo vya Afya; Habari hii inaleta mawanga na matumaini ya kuishi Maisha bora na afya tele bila masumbuko kwa watu wote wenye sikoseli nchini. | | | | |SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita 01 | ULIMWENGU WA SIKOSELI |
  • 8. U Pia kutokana na uhaba wa upatikanaji wa huduma za afya na matibabu sahihi kwa wagonjwa wa sikoseli bila kusaha gharama za juu za matibabu, hii inapelekea asilimia kubwa ya watu wenye sikoseli kushindwa kumudu gharama za matibabu katika vituo binafsi na kupelekea kufeli kupata matibabu sahihi hivyo afya zao kuzorota kutokana na athari zinazoletwa na ugonjwa huo hivyo kupelekea wengi wao kupoteza Maisha katika umri mdogo kwasababu ya kukosa uangalizi wa mapema. Kwa miaka mingi jamii ya sikoseli ukijumuisha na wanaharakati wa sikoseli wamekua wakipaza sauti juu ya umuhimu wa upatikanaji wa huduma bora na matibabu sahihi kwa wanajamii ya sikoseli ili kuongeza ubora wa Maisha na afya zao. Hatimaye serikali kushirikiana na washika dau mbalimbali katika sekta ya afya walisikia vilio vyao na toka mwaka 2007 mpaka sasa, kumekua ongezeko la kliniki mpya za sikoseli katika vituo vya afya vya ngazi ya msingi, wilaya na hata Taifa kwa ajili ya uangalizi wa karibu kwa watu wenye sikoseli. Nikiongeza, na kwa mwaka 2022 Jarida letu lingependa kukuhabarisha kuwa sasa wigo wa huduma za afya kwa watu wenye sikoseli unazidi kutanuka na kukukua kwani kuacha kliniki za Mloganzila, Mwananyamala, Temeke na Kliniki iliyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili, serikali yetu kupitia wizara ya Afya imeongeza kliniki nyingine mpya, hii ikiwemo Kliniki ya Sikoseli mkoani Kilimanjaro katika Hospitali ya KCMC, tunapenda kuwahabarisha wanajamii wa sikoseli waliopo Moshi, Kilimanjaro kuwa sasa huduma za afya kwao zimesogezwa karibu kabisa, kwani kuna kliniki mpya ya sikoseli, katika jingo la Hemophilia Center, Kitengo cha matibabu ya saratani. Pia bila kusahau kuwa mwezi huu siku ya maadhimisho ya sikoseli duniani, jijini Arusha katika Hospitali ya jiji Mount Meru, Mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Afya Dkt. Shekalaghe alizindua kliniki mpya ya sikoseli katika Hospitali hiyo Kongwe, tukielekea mkoani Pwani, Wilayani Bagamoyo napo hawakuwa nyuma katika harakati hizi, Mheshimiwa Kaimu Mkurugenzi wilaya ya Bagamoyo, Pwani alikata utepe na kufungua rasmi Kliniki ya Sikoseli Bagamoyo na Kuagiza kuwa wapewe ushirikiano na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, hii ni pamoja na uangalizi na upatikanaji wa vifaa tiba. Tukifunga kurasa hii, Tunaweza kusema, “Harakati za sikoseli Tanzania, Kumenoga ” Ni matumaini yetu kuwa uwepo wa kliniki hizi utapunguza adha waliyokuwa wakipitia wagonjwa wengi wa sikoseli mikoani nan je ya jiji la Dar es Salaam kwa kusafiri umbali ili kupata matibabu au kulazimika kuhudhuria matibabu katika vituo binafsi hivyo kubeba mzigo mkubwa wa gharama za matibabu na pia hatua hii itapelekea kupunguza vifo vya awali vya wagonjwa wa sikoseli. Shujaa ingependa kuendelea kuwahasa na kusisitiza wanajamii wa sikoseli kuhudhuria kliniki hizi ili kupata matibabu sahihi na endelevu, pia kwa serikali yetu tukufu tunasema, “shukrani na kazi iendelee” | UZINDUZI WA KLINIKI ZA SIKOSELI KWA MWAKA 2022. 01 | ULIMWENGU WA SIKOSELI | SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita gonjwa wa Sikoseli ni ugonjwa wa kurithi ambao unaathiri seli hai nyekundu za damu na kubadili umbo lake kutoka katika umbo la kawaida la donati na kuipa seli hai nyekundu umbo la ndizi au mundu hii hutokana na upungufu wa oksijeni, protini katika Hemoglobin ya seli; Hivyo hali hii inapelekea mtu kupata dalili kama maumivu makali ya viungo na hata hali ya kupungukiwa damu (anemia). Tafiti zinaonesha kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazoongoza katika chati ya dunia kwa kuwa na asilimia kubwa ya watu wenye sikoseli ikishika nafasi ya nne; Pia tafiti zinaonesha kuwa kila mwaka Watoto 11,000 huzaliwa na sikoseli nchini, Tanzania. Pia makadirio yanaonesha karibu asilimia 20% ya watanzania wanazaliwa na vinasaba vya sikoseli; | |
  • 9. W WARSHA YA CONSA (CONSORTIUM OF NEWBORN SCREENING IN AFRICA) 02 | MATUKIO | SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita arsha hii ilifanyika Juni 22, 2022 kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa tisa alasiri katika ukumbi wa kampasi ya chuo cha MUHAS; Ilijumuisha watoa huduma ya afya pamoja na kitengo cha Sikoseli MUHAS, wazazi wote ambao wana watoto wenye Sikoseli na waliogunduliwa kupitia kipimo cha Newborn Screening. Lengo la warsha hiyo likiwa ni kutoa elimu kwa wazazi hao kupitia matabibu wenye ujuzi na weledi wa juu; Pia kuacha elimu ya malezi kwa Watoto wenye Sikoseli walitoa elimu juu ya umuhimu wa kuwa na bima ya Afya ya NHIF ili kuwawezesha kupata huduma zote muhimu za matibabu na kliniki kwa Watoto hao hivyo kuwapunguzia mzigo wa gharama za kulipia kwa njia ya fedha. Kuacha elimu iliyotolewa na wataalamu wa afya waalikwa, wazazi walipata nafasi ya kueleza jamii juu ya safari zao kama wazazi wa Watoto wenye Sikoseli na waliogundulika katika umri mchanga na pia wazazi hao walieleza jinsi safari hii ina milima na mabonde mengi na vile kuwa na mtoto mwenye mahitaji maalum ni safari ya kuwa na Subira, upendo na kuwa tayari kujifunza kila siku na kushirikiana na asasi zilizopo na watoa huduma ili kuhakikisha malezi ya mtoto yanapewa kipaumbele na anapata matibabu na huduma sahihi za afya kwa ukuaji mzuri. Huduma za vipimo vya Newborn Screening zinapatikana katika vituo vya afya vya Amana, Temeke, Muhimbili na Bugando nchini, Tanzania.
  • 10. K KONGAMANO LA SABA LA KISAYANSI, CHUO KIKUU CHA MUHAS. 02 | MATUKIO | SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita ongamano la saba la kisayansi lililoandaliwa na wanazuoni na wataalamu wa tiba na sayansi wa chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Mhumbili (MUHAS) na Kufanyika chuoni hapo siku ya Tarehe 26, Januari 2022 katika Kampasi kuu ya Dar-es-salaam; Lengo kuu ikiwa ni kujadili mwelekeo mpya wa nchi katika kukabili ugonjwa wa sikoseli ambao unaathiri asilimia kubwa ya Watoto nchini, Tanzania. Kongamano ilo lilishirikisha na kukutanisha washika dau mbalimbali katika sekta ya Afya na Sayansi, likijumuisha Wizara ya Afya, wanazuoni na wakufunzi mbalimbali, watafiti katika sekta ya Afya, watoa huduma na Mfuko wa Bima ya Afya NHIF pamoja na wengineo wengi. Mojawapo ya mambo yaliyozungumziwa ilikuwa ni pamoja na utekelezaji wa sera ya bima ya afya pamoja na kujumuisha dawa ya Hydroxyurea katika vifurushi vya mfuko wa Bima ya Afya Taifa, NHIF kwa faida ya wagonjwa wa sikoseli nchini. Dkt. Agnes Jonathan, Daktari Bingwa wa Afya ya Jamii pamoja na kuwa Mratibu wa Mradi wa Sikoseli (SPARCO, TANZANIA) MUHAS katika uwakilishi wake wa mada juu ya sikoseli alisema, tafiti zinaonesha kuwa kadiri ya Watoto 11,000 huzaliwa na ugonjwa wa sikoseli, hivyo yeye kama mratibu wa mradi wa SPARCO, TANZANIA pamoja na timu nzima wamefanikiwa kuwaingiza kwenye mfumo wa Tiba na ufuatiliaji wa karibu katika matibabu ya kliniki ya sikoseli takribani Watoto 5000 na pia wamewapatia vitabu ambavyo vinabeba taarifa zao muhimu za afya. Dkt. Agnes Jonathan, aliongeza kuwa tafiti zinaonesha kuwa takribani asilimia 13 hadi 20 ya watanzania wamebeba vinasaba vya ugonjwa wa sikoseli na asilimia iliyosalia bado hawajui hali zao. Pia mojawapo ya wageni rasmi waalikwa alikua Mheshimiwa Prof. Abel Makubi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, ambapo alisisitiza juu ya umuhimu wa hydroxyurea kujumuishwa katika mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF kwasababu ya umuhimu wa dawa hiyo kwa watu wenye sikoseli, Pia Mheshimiwa wa Prof. Abel Makubi, Katibu Mkuu Wizara ya Afya aliongeza kwa kusema, “Tanzania inastahili iwe na kituo cha umahiri kwa upande wa sikoseli” mwisho wa nukuu. Taasisi ya Jumuiya ya Wagonjwa wa Sikoseli Tanzania (SCDPCT) nayo haikuachwa nyuma, ikiwakilishwa na Mkurugenzi Mwanzilishi wake, Bi. Arafa Said; Akiwakilisha hoja juu ya umuhimu wa uboreshwaji huduma za afya kwa watu wenye sikoseli Tanzania pia alichukua nafasi hiyo kuwaelimisha na kuzungumza juu ya, “Uzoefu na Maisha ya wagonjwa wa sikoseli” akiwakilisha jumuiya ya wagonjwa wa sikoseli Tanzania. Ni dhati kuwa Kongamano ilo la saba la Kisayansi lililoandaliwa na chuo kikuu cha MUHAS lilikuwa chachu ya mabadiliko katika Tiba na Huduma za Afya kwa watu wenye Selimundu kwani Baada ya hapo, Dawa za Hydroxyurea ziliweza kujumuishwa katika mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF, na sasa watu wote wenye sikoseli wanaweza kupata dawa hizo bure bila kulipa gharama yeyote kupitia Bima ya NHIF.
  • 11. M MAONYESHO YA KAZI YA WANAHARAKATI WA SIKOSELI TANZANIA 02 | MATUKIO | SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita aonesho ya vikundi vya wanaharakati wa sikoseli Tanzania yalifanyika Tarehe 28 Januari, 2022 katika kituo cha Sickle Cell Centre, MUHAS. Maonesho hayo yaliandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Jumuiya ya wagonjwa wa sikoseli Tanzania (SCDPCT) ikishirikiana na MUHAS Sickle Cell Program. Lengo la maonesho likiwa ni kuwaleta pamoja wanaharakati wa Sikoseli nchini na kuwapa uwanja wa kuonesha kazi zao na ufanisi walio nao katika kuhakikisha elimu na ufahamu juu ya Sikoseli unakuwepo nchini Tanzania. Taasisi ya Jumuiya ya wagonjwa wa Sikoseli Tanzania (SCDPCT) ilipata nafasi ya kuonesha baadhi ya kazi zao katika warsha hiyo ilifanyika katika kituo cha Sikoseli, MUHAS. Mojawapo ya Kazi zetu ambazo tulionesha zilijuimusha vitabu vya SHUJAA na AMANA SHUJAA WA SIKOSELI na machapisho ya elimu ya Sikoseli, hii ikijumuisha toleo la kwanza la kijitabu cha SAUTI YA SHUJAA ambapo ni mjumuisho wa masomo kuhusu mambo mbalimbali ya Afya ambayo yanaathiri wagonjwa wa Sikoseli kwa ujumla. Pia tulipata nafasi ya kuonesha kupitia picha Kampeni na Kazi za Kijamii ambazo Taasisi inafanya ili kueneza elimu na ufahamu wa Sikoseli katika maeneo na mikoa mbalimbali Tanzania. Lengo la kazi hizi zote ni kuhakikisha kuwa elimu na ufahamu juu ya ugonjwa wa sikoseli unafikia watanzania wote na pia wanaharakati wa sikoseli wanapata fursa ya kuonesha kazi zao na kujumuika na jumuiya wa wenye Sikoseli na kujua mahitaji yao ili kuwepo na maboresho kwa kipindi kijacho mbeleni. Maonesho yalifika kilelel na wanavikundi pamoja na waalikwa walipata kujifunza na kuona kazi mbalimbali ambazo vikundi hivyo vya wanaharakati na wajumbe wa jumuiya ya Sikoseli wanazifanya ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika jamii juu ya sikoseli na pia ili kuhakikisha dhana potofu zinapotea na kunakuwepo na uelewa, ufahamu na elimu juu ya Sikoseli.
  • 12. DONDOO MUHIMU ZA KUISHI NA UGONJWA WA SIKOSELI 02 | DONDOO ZA AFYA | SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita Siko seli/seli mundu ni nini? Siko seli ni ugonjwa wa kurithi unaosababisha mabadiliko yasiyo ya kawaida katika umbo la chembechembe nyekundu za damu. Kwa kawaida chembe nyekundu za damu zina umbo la mviringo ambalo huzirahisishia kupita kwenye mishipa midogo ya damu ili kusafirisha hewa safi ya oxygen katika sehemu mbalimbai za mwili. Kwa mtu mwenye ugonjwa wa siko seli, seli hizi huwa tofauti; zinanata na zina umbo la mwezi mchanga (mundu). Tanzania ni mojawapo kati ya nchi zenye wagonjwa wengi wa siko seli duniani ambapo inakadiriwa takribani watoto 11,000 huzaliwa na ugonjwa wa siko seli kila mwaka. Pia inakadiriwa kuwa 12% hadi 20% ya watu wote nchi wana vinasaba vya ugonjwa wa siko seli (sickle cell trait), kutegemeana na eneo. Dondoo Muhimu za kuishi na ugonjwa wa Siko seli. a. Uchunguzi wa kiafya wa mara kwa mara ni muhimu kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja. Wanapaswa kumuona daktari kila baada ya miezi miwili au mitatu b. Watoto kuanzia mwaka mmoja mpaka mitano wanatakiwa kumwona daktari kila baada ya miezi mitatu Kuzuia Maambukizi c. Hakikisha watoto wanapata chanjo zote za kawaida d. Watoto wapewe chanjo ya ziada ya kuzuia kichomi (Pneumococcal vaccine) e. Watoto wote wenye umri chini ya miaka 6 wapatiwe dawa ya penicillin ili kujikinga na maambukizi f. Hakikisha watoto wanakingwa na maambukizi ya malaria kwa kutumia chandarua chenye dawa Zingatia Ushauri wa Kitaalamu g. Watoto wanatakiwa kunywa maji ya kutosha wakati wote na wapewe mlo kamili, ukijumuisha matunda, mbogamboga, vyakula vya kutia nguvu na vya kujenga mwili wa mtoto. h. Watoto waepuke kukaa katika mazingira ya joto kali ama baridi sana i. Watoto wajishungulishe na michezo mbalimbali ili wawe na furaha na afya njema, wasicheze kiasi cha kuwachosha sana.
  • 13. W UMUHIMU WA LISHE BORA KWA WENYE SIKOSELI 02 | DONDOO ZA AFYA | SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita agonjwa wengi wa sikoseli wanaweza kuwa na mwili mdogo lakini kuna hatari ya kuwa na unene uliopita kiasi. Wanashauriwa kula vyakula vyenye kalori ya juu na vyenye virutubisho vingi tangu utotoni. Lishe Bora; ni ile ambayo inajumuisha aina zote za vyakula ambavyo vina virutubisho vinavyohitajika mwilini. Ili lishe iwe bora lazima sahani iwe na mjumuisho ufuatao: 1/4 iwe Wanga, 1/4 iwe Protini na 1/2 iwe na vyakula vyenye Vitamini. Sahani yako inatakiwa kuwa na Wanga (ugali, wali,mtama, mhogo, gimbi, viazi, ndizi etc), Protini, Vitamini A, B6, C, D, E na virutubisho vingine vidogo kama zinki, kalsiamu na magnesiamu. Lishe bora ni muhimu katika kuongeza chembe za damu, kuimarisha mifupa, kuupa mwili nguvu na kuongeza kinga ya mwili. Ili kuhakikisha kuwa unapata lishe bora katika mlo wako wa kila siku ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo; Angalau sahani yako iwe na aina 1 ya Protini na mboga na matunda (chakula kimoja kinaweza kuwa na kirutubisho zaidi ya kimoja), kwa wale ambao ni ngumu kuepuka kuongezewa damu mara kwa mara wanashauriwa kupunguza vyakula vyenye madini chuma kwa asilimia kubwa pia unashauriwa kula vyakula vinavyotoka/ vinalimwa ardhini kwa njia ya asili (organic foods) hivyo ni bora zaidi ya vile vya viwandani na vinavyochakatwa kupita kiasi. Bila kusahau umuhimu wa maji katika mmeng'enyo wa chakula, usafirisha virutubisho katika mwili, msukumo mzuri wa damu. Unashauriwa glasi 8 sawa na Lita 2 au 3 kwa siku. Watu wengi wanashindwa kula lishe bora kutokana na kuwa na uhusiano mbovu na vyakula; Lishe bora ni vile unavyopangilia sahani yako na virutubisho utakavyoweka. Makala hii ya Lishe Bora imenukuliwa kutoka katika chapisho la kwanza la SAUTI YA SHUJAA, somo ambalo lilitolewa na Dkt. Victoria Msambichaka, mtaalamu wa lishe kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili. |
  • 14. “HUU SI UGONJWA WA KUROGWA” 03 | MITINDO YA MAISHA SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita “Ninaishi na Siko Seli miaka 70 sasa. Nikiwa na miaka 15 nilianza kuugua mara kwa mara, awali haikujulikana tatizo langu nini, nilikuwa naishiwa damu mara kwa mara, nalazwa kuna nyakati pia niliongezewa maji,” anasimulia.
  • 15. “HUU SI UGONJWA WA KUROGWA” 03 | MITINDO YA MAISHA SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita “Ninaishi na Siko Seli miaka 70 sasa. Nikiwa na miaka 15 nilianza kuugua mara kwa mara, awali haikujulikana tatizo langu nini, nilikuwa naishiwa damu mara kwa mara, nalazwa kuna nyakati pia niliongezewa maji,” anasimulia. Jamii imegubikwa na dhana nyingi potofu juu ya ugonjwa huu, wengi hukimbilia kwa waganga wa kienyeji wakiamini wamerogwa au kukumbwa na pepo wabaya; Pamoja na hao wapo wengine ambao huamini mgonjwa wa Siko Seli hawezi kuishi zaidi ya miaka 18. Lakini maisha ya Fatuma Ubwa, Mkazi wa Bagamoyo mkoani hapa ni ushuhuda tosha kwamba mtizamo huo si sahihi. Mwanamama huyo Juni, mwaka huu amesherehekea miaka 70 ya kuzaliwa kwake, ni mgonjwa wa Siko Seli. Zaidi anasimulia.... “Nikiwa na miaka 15 nilianza kuugua mara kwa mara, awali haikujulikana tatizo langu nini, nilikuwa naishiwa damu mara kwa mara, nalazwa kuna nyakati pia niliongezewa maji,” anasimulia. Anasema kutokana na hali hiyo wazazi wake walihisi amerogwa na wapo wanajamii ambao walishauri apelekwe haraka kwa wataalamu {waganga wa kienyeji akatibiwe huko}. “Lakini baba yangu alikataa, hivyo niliendelea kupelekwa hospitalini na huko baadae niligundulika nina Siko Seli. Hivyo, nimezaliwa na Siko Seli, naishi nayo kwa miaka 70 sasa.” Anasema amejaliwa kupata watoto wanne ambao wao hawana Siko Seli, vile vile amejaliwa wajukuu kadhaa ambao nao hawana ugonjwa huu. Uso wake umejaa tabasamu, kila anaposimulia simulizi yake wengi huvutiwa na kustaajabu namna gani ameweza kumudu kuishi nao kwa miaka yote hiyo? Anasema wazazi wake walizingatia kumpeleka kliniki kila alipohitajika na kwamba ameishi hivyo akizingatia maelekezo anayopatiwa na wataalamu wa afya. Fatuma anaongeza “Siko Seli si ugonjwa wa kurogwa, hautokani na uchawi… mtu anazaliwa nao pale anapokuwa amerithi vinasaba kutoka kwa wazazi wetu wote wawili {baba na mama}; Tusiuone ni kitu cha ajabu au ugonjwa wa ajabu ni wa kawaida tu, Mungu keshatupa tunapokea,” anatoa rai. Anasema watu wasiwe na wasiwasi kuhusu ugonjwa huo, huku akishauri “Ukimuona mtoto wako {ana ugonjwa huu} mpeleke hospitali afuatiliwe afya/hali yake ili apatiwe tiba stahiki na elimu ni jambo la msingi hakikisha unampeleka shule kama watoto wengine. Anaongeza “Kuna watu wapo kazini na wana Siko Seli na mimi nilisoma mpaka 'form two' {kidato cha pili} Shule ya Sekondari Miembe Saba. “Zamani shule zilikuwa mbali za sekondari, lakini nilishindwa kuendelea Siko Seli ilinizidi sana; Na nina uchungu sana kwa sababu nilishindwa kumaliza lakini napenda sana, nilitamani niendelee lakini ndiyo hivyo ilinibana sana,” anasema. Shujaa huyo wa Siko Seli anasisitiza “Nawaombeeni dua mlio na matatizo haya mpone, muendelee na kazi zenu vizuri.” “Madaktari wangu wote nawaombea, mnanisikiliza vizuri, mnanitibia vizuri, nashukuru Mungu kwa hilo.”
  • 16. _ MAISHA, SANAA NA SIKOSELI 03 | MITINDO YA MAISHA SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita Martin Deus Theo al maarufu Shetani wa mguu mmoja au unaweza kumuita Chiba Kismati ni kijana wa umri wa miaka 36, alizaliwa mpanda Agosti 1985 na alipofika umri wa miaka 2, wazazi wake waligundua kuwa ana sikoseli, taarifa ambazo walizipokea kwa ugumu kutokana na kwamba waliambiwa kuwa ugonjwa huo hauna tiba na mwanao asingeweza kuishi kupita miaka 18. Chiba Kismati anatoa simulizi yake kwa jarida la shujaa kwa kuongeza kuwa, baada ya wazazi wake kuambiwa kuwa asingeweza kupona na kuwa asingeishi kwa zaidi ya miaka 18, walichukua maamuzi ya kugeukia kwenye tiba za Kienyeji ambapo alipelekwa kwa waganga mbalimbali, mikoa tofauti tofauti nchini huku akipewa tiba za madawa ya kienyeji kwa ahadi ya kuwa dawa hizo zingetibu na kuondoa ugonjwa huo wa Sikoseli, anasema kuwa alitumia tiba za ajabu ambazo haziku- saidia bali zilizidi kudhoofisha afya yake, mfano kuna wakati alishauriwa kutumia kinyesi kilichokauka kwa madai ya ku- wa ni tiba ya sikoseli. Haya yote yalitokea kutokana na kw- amba yeye pamoja na wazazi wake hawakuwa na ufahamu na elimu ya sikoseli. Sikoseli iliathiri Maisha yake katika Nyanja kama elimu, ali- shindwa kuendelea na elimu kutokana na kuumwa kwa vipindi vya mda mrefu hadi miezi 6, hivyo ilimlazimu kusitisha elimu yake pale alipofika kidato cha saba ndio ikawa kikomo kwake lakini pia anasema kutokana na kupata vidonda katika mguu am- bacho kilipelekea yeye kupata osteomyelitis na kupelekea kupot- eza mguu kutokana na maambukizi hayo ya mifupa. Baadae aliha- ma kutoka mpanda na kuhamia Dar es salaam ambapo alikua anapata matibabu katika kliniki ya Watoto pale Hospitali ya Taifa Muhimbili. Katika Kukua kwake anasema alihisi kama watu walikua wanampuuza aswa kutokana na kuwa na ulemavu wa mguu, yeye kama msanii wa sanaa ya uigizaji inakua ngumu kupata kazi na pia kutokana na changa- moto za afya na pia kukosa elimu kulipelekea Maisha yake kuwa duni ku- tokana na kukosa kazi na hivyo akaamua kuingia katika tasnia ya uigizaji lakini na huko pia alipata changamoto kutokana na hali yake ya ulemavu. Chiba anakanusha kauli ya kuwa mtu mwenye sikoseli hawezi kuishi miaka zaidi ya 18 kwa kusema kuwa, yeye ana miaka 36 na yupo, anahimiza kikubwa ni kupata elimu na kuzingatia ushauri wa madaktari na lishe bora na kuepuka kazi nzito kupita kiasi; anatoa ushauri kuwa inawez- ekana kuishi miaka zaidi ya miaka 70 pia anahimiza kuwepo semina mkoa kwa mkoa, nchini. Pamoja na kuwa na sikoseli anasema hawezi kukata tamaa kwani anatumia fursa za usanii katika kuelimisha umma kuhusu sikoseli na pia yeye ni baba wa familia na anategemewa kama kichwa cha familia yake hivyo sikoseli haija- mzuia kuwa na Maisha mazuri. Anafuatilia matibabu kwa kuhudhuria kliniki, anazingatia lishe bora pamoja na kan- uni za afya, anashukuru madaktari, jumuiya ya Sikoseli Tanzania. Inaendelea...
  • 17. _ KUWA MJANJA IJUE SIKOSELI NA KILAZA 03 | MITINDO YA MAISHA SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita Aboubakar Juma Kilaza, Miaka 35 ni Msanii wa Muziki wa Bongo Flava; Alizaliwa na Sikoseli na kwasababu wazazi walipata elimu kuhusu Sikoseli kwasababu Mama ya- ke alikua ni muuguzi na Baba yake alikua ni muuguzi; kutokana na kwamba wazazi wa- ke walikua na ufahamu wa sikoseli walijitoa katika yeye kupata matibabu, walihangaika katika zahanati mbalimbali kutafuta matibabu na hatimae walifika Hospitali ya Taifa Muhimbili, hapo ndipo alipopata matibabu yake na kuanza kliniki ya sikoseli.Kuwa na Sikoseli hakukufanya ajione tofauti na Watoto wengine, isipokuwa aliku- wa anahitajika kumeza dawa kama Folics Acid na Pen V kila siku na kuhu- dhuria kliniki. Alizidi kukua na kuelewa hadi kupelekea yeye kuwa balozi wa Sikoseli Tanzania. Anasema kwa ujumla hajaathiriwa na sikoseli kabisa kwani Sikoseli kwake imekua kama fursa ya kuwa kijana mwadilifu na kuepu- ka makundi kama ya wavuta bangi na mambo ambayo yanaenda kin- yume na jamii na pia kwakuwa anafanya kazi za sanaa Sikoseli ina- mpa fursa ya kutumia sanaa yake katika kuhamasisha umma kuhusu Sikoseli. Yeye kama msanii anawakilisha na kuelimisha kuhusu si- koseli kwenye nyimbo anazotunga na anapenda kujulikana kwa jina la Mr. Sickle Cell Kila nyimbo anayotoa anaweka jina hilo kama utambulisho. Anasema yeye hawezi kuonekana dhaifu kwa kuwa familia y- ake anaiendesha mwenyewe, anaongeza kusema kuwa Sikos- eli haimfanyi kuwa dhaifu kwani hata bila Sikoseli mtu una- weza kuwa dhaifu.Anahudhuria kliniki na anafurahishwa na hu- duma zinazotolewa lakini pia anaomba serikali pamoja na jamii itambue Si- koseli na washirikiane katika kuboresha na kuimarisha huduma za matiba- bu ya Sikoseli. ...jumuiya ya Sikoseli Tanzania. Inaendelea... Lengo kuu la kuwa na taasisi ya Chiba Kismati ni kutoa fursa na jukwaa kwa wasanii wenye ulemavu na kuondoa matabaka na unyanyapaa uliopo. Yupo kwa ajili ya jamii na kwa lengo la kujitoa kwa jamii. Anategemea kutoa elimu zaidi kupitia taasisi yake ya chiba kismati; kuanzia mikoa ya Arusha, Tanga, Pwani na Zanzibar. Anaomba serikali kuangalia watu wenye sikoseli kwasababu ugonjwa ni wa mda mrefu, anaomba wizara husika iwasaidie katika kup-unguza gaharama za matibabu na kuwajumuisha katika bima. Matarajio yake ni kutumia sanaa yake kufikisha ujumbe kwa wanajamii kuhusu Sikoseli. changamoto ni kukosa miundombinu na rasilimali za kuwezesha kazi hiyo ya uhamasishaji. Ujumbe wake kwa jamii, wasikatishe watu wenye sikoseli tamaa na kusema kuwa hawawezi kuishi mda mrefu kwani yeye ni mfano tosha kuwa ameishi mpaka sasa ana miaka 36, na wengine wengi wenye miaka 60, 70, 90 na kuendelea; Pia anawahasa wanajamii ya sikoseli wasitumie sikoseli kama kudeka na kurahisisha Maisha yao, wafanye kazi zao kwa bidii na vizuri kwani Sikoseli ni ugonjwa kama mengine tu.
  • 18. SEPTEMBA, MWEZI WA UELEWA WA SIKOSELI. 03 | MITINDO YA MAISHA SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita Kwa wasiojua na kwa faida ya wanajua sio mbaya tukikumbushana kuwa mwezi wa septemba ni mwezi wa kutoa uelewa na ufahamu juu ya ugonjwa wa Sikoseli duniani. Hivyo Taasisi ya Sickle Cell Disease Patients' of Tanzania kuungana na taasisi na jumuiya kimaifa iliadhimisha siku hiyo kwa kuandaa matukio mbalimbai ya uhamasishaji, uelimishaji na kutoa uelewa juu ya ugonjwa wa sikoseli nchini ikishirikiana na taasisi na washika dau katika sekta ya afya. Kama jumuiya ya wagonjwa wa sikoseli Tanzania na kama wanaharakati na washika dau katika elimu na ufahamu juu ya sikoseli waliandaa Jukwaa la Mashujaa mkoani Pwani, wilaya ya Mkuranga kushirikiana na Hos- pitali ya Wilaya Mkuranga lengo kuu la jukwaa hili likiwa ni kutoa fursa ya majadiliano ya wazi kati ya wanajam- ii wa mkuranga na wataalamu wa afya kuhusu Sikoseli na pia wataalamu waliruhusu wasaa wa maswali na majib- u ambapo changamoto mbalimbali na Imani potofu zinazozunguka ugonjwa wa sikoseli zilijadiliwa na kutolewa majibu sahihi ili kuelimisha wahudhuriaji; pia wahudumu walitoa fursa ya ushauri nasaha kwa mtu mmoja mmoja. Tamasha la Jukwaa la Mashujaa lilifuatiwa na tukio la mnamo tarehe 27, Septemba ambapo taasisi ya SCDPCT iliandaa Upimaji wa Sikoseli bure ikishirikiana na Hospitali ya Wilaya Bagamoyo na Zahanati ya Mwavi iliyopo kata ya fukayosi, mkoani Pwani, upimaji huu uliambatana na ushauri na elimu juu ya sikoseli, pia Sickle Cell Disease Patients' Community of Tanzania kushirikiana na wafadhili wake walifanikiwa kuwafadhili bima Watoto walio chini ya umri wa miaka 16, Bima za afya za NHIF ili kuwasaidia kupata matibabu kwa gharama rahisi na pia kuwahamasisha kuhudhuria kliniki za sikoseli kwa matibabu sahihi ili kuboresha afya zao.Mwezi septemba ulifungwa na kampeni za sauti ya shujaa, ambapo tulipokea video mbalimbali kutoka kwa wanajamii, madaktari na wauguzi, washirika katika sekta ya afya wakitoa elimu na ufahamu juu ya sikoseli kwa wanajamii kupitia njia ya video. Septemba ilinoga, tunakukumbusha na kuhamasisha kuwa usikose kushiriki harakati hizi kwa msimu mwingine wa septemba yani mwaka 2023 kwani yajayo yanafurahisha.
  • 19. CHANGIA DAMU, OKOA MAISHA. 03 | MITINDO YA MAISHA SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita Maji ni uhai lakini umewahi kukaa na kufikiri kuwa Damu ni uhai pia? Tukizidi kuhimiza jamii juu ya umuhimu wa kuwa na ufahamu na uelewa wa sikoseli, tungependa kuwakumbusha pia kuwa zaidi ya watu 100,000 uzaliwa na ugonjwa wa sikoseli kila mwaka na Tanzania ni mojawapo kati ya nchi ambazo zinaongoza kwa kuwa na asilimia kubwa ya watu wenye sikoseli duniani. Mgonjwa wa sikoseli anaweza kuhitaji mpaka uniti 100 za damu kwa mwaka kwa ajili ya matibabu ya athari zina- zotokana na ugonjwa huo. Hakuna aliyewahi kupungukiwa kwa kutoa na pia kutoa kutoka moyoni ni zawadi kwa muhitaji; kukosa damu ni mojawapo ya sababu zinazochangia katika kupoteza Maisha kwa wagonjwa wengi wa sikoseli kwasababu kwao damu ni uhai. Unaweza kuwa mwokozi wa Maisha ya wengi kupitia kuchangia damu, unaweza kuokoa Maisha ya mtu aliyepata ajali ya gari, mgonjwa wa saratani anayehitaji damu kwa matibabu yake, zaidi kwa wagonjwa wa sikoseli ambao wanahitaji damu kwa Maisha yao yote ili kuishi. Faida za kuchangia damu ni pamoja na kuchangia damu ni faida kwa moyo wa binadamu kwani kwa kuchangia damu utaweza kuulinda moyo wako na maradhi ya moyo kama vile shinikizo na kuganda kwa damu. Pia utapata kujua hali ya afya yako kupitia vipimo vinavyofanywa kabla ya kutoa damu, pia ni furaha kujua kuwa kupitia ku- changia damu unaokoa Maisha ya wengi ni furaha ya kuishi na kujitoa kwa ajili ya wengine wenye uhitaji kwenye jamii. Kuchangia damu ni bure kabisa, hakuna malipo unaweza kuwa shujaa wa mtu kwa kuchangia dam una kuokoa Maisha yake bure kabisa. Fikiria ni lini mara ya mwisho ulipata kutoa msaada bure bila kulipia gharama yeyote bila kuhitajika shahada yeyote au ubunifu wowote. Mwishoni niseme, unapochangia damu unaongeza mwaka mwingine wa Maisha kwa mpokeaji damu, unatoa siku ingine ya Maisha, siku ingine ya sherehe ya kuzaliwa, zaidi unaongeza siku ingine chini ya usiku wa nyota uliojaa tabasamu na afya, unatoa nafasi nyingine ya kutimiza ndoto na unatoa zawadi nyingine ya Maisha kwa wapendwa wa mpokeaji damu. Hivyo ni kuhimize changia damu, okoa Maisha…Timiza ndoto. Umuhimu wa Uchangiaji Damu
  • 20. 04 MATANGAZO SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita MATUKIO NA MAISHA matukionamaisha.blogspot.com Kwa habari na makala za kina kuhusu masuala mbalimbali ya afya na jamii tembelea jukwaa la matukionamaisha.blogspot.com ni akaunti iliyotambuliwa kwa tuzo na Baraza la Habari Tanzania (MCT) mwaka 2021 jukwaa bora katika kuripoti masuala ya afya Tanzania, Aidha Mmiliki wake Veronica Mrema mwaka 2021 alitunukiwa tuzo na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza Afrika Mashariki miongoni mwa waandishi bora wanaoripoti vema.
  • 21. 04 MATANGAZO SHU AA JARIDA LA J Arafa Na Arafa Said & Emmy Mwita BLACKART
  • 22. SHU AA MAGAZINE J With Arafa Salim & Emmy Mwita | Meals on Wheel is a private registered enterprise that offers catering services for more than three years now Meals on Wheel works to make any event or meal time a delicious one 04 MATANGAZO
  • 23. SHU AA MAGAZINE J With Arafa Salim & Emmy Mwita | 04 MATANGAZO +255743222145
  • 24. SHU AA JARIDA LA J Na Arafa Said & Emmy Mwita Ahsante kwa kusoma Tufuatilie kupitia IG: @sicklecellpatientstz FB: Sickle Cell Disease Patients Community of Tanzania