SlideShare a Scribd company logo
1 of 5
Maana ya maana ni mojawapo ya dhana inayoibua changamoto katika nadharia za lugha
(Ullman 1964:54). Kwa muda mrefu kumekuwepo na maelezo ya namna mbalimbali
kutoka kwa wataalamu kama vile wanafalsa, wanasaikolojia na wanaisimu kuhusu nini
maana ya maana. Mjadala huu umekuwa na kutoelewana kwingi kati ya wataalamu hawa.
Kutakana na hali hii, kubainisha maana ya maana wataalamu mbalimbali wamejaribu
kulipunguzia wigo na kujishughulisha na maana ya neno kwa kulipa sifa bainifu.


Japo kwa kutumia kigezo hiki, ugumu wa kuelezea maana ya maana unapunguzwa kwa
kiasi fulani, lakini bado tatizo la msingi kuhusu nini maana ya maana lipo pale pale. Hii
ni kwa sababu vipashio vingi vya kiisimu (hata tukiachilia mbali maneno) vimefumbata
maana fulani. Mathalani, mofimu za maneno hufumbata maana fulani, kwani maana za
msingi zinazotokana na muunganiko wa mofimu hizo huleta maana ya jumla ya neno
husika.


Katika insha hii, ‘maana’ itamaanisha mchanganyiko wa uhusiano wa kimuktadha,
fonimu, sarufi, leksikografia na semantiki ambapo kila kimoja kinachangia katika maana
ya msingi ya tungo kwa kuzingatia muktadha wa matumizi1.


Kwa kuwa swali la “nini maana ya maana” limekuwa ni jambo la mjadala lenye
kutoelewana kwingi, nadharia mbalimbali zimeasisiwa ili kujaribu kuondoa uvulivuli
unaofumbatwa katika maana ya maana. Miongoni mwa nadharia hizo ni pamoja na
nadharia ya kitajwa, nadharia ya dhana, nadharia ya mwitiko na nadharia ya matumizi.
Katika insha hii, nadharia ya matumizi kuhusu nini maana ya maana ndiyo
itakayojadiliwa kwa mapana. Hata hivyo, nadharia nyingine zitaelezewa japo kwa ufupi
ili kuweka mtiririko wa mantiki.


Tukianza na nadharia ya kitajwa, hii inaangalia uhusiano kati ya tungo na kitu ua vitu
katika ulimwengu halisi. Kwa mantiki hii, maana ya tungo inapatikana kwa kuangalia
uhusiano baina ya neno hilo na kitu kinachorejelewa. Kwa kiasi fulani, nadharia hii ina
ukweli ndani yake kwani kila lugha ina maneno mengi yahusuyo ulimwengu na

1
    Fodor (1980)


                                                                                       1
malimwengu kulingana na wanajamii walivyoumega ulimwengu wao na kuainisha
malimwengu yaliyomo. Hata hivyo, mtazamo huu una mapungufu fulani ikiwa ni pamoja
na kwamba, si kila leksimu yenye maana inarejelea kitu fulani. Yapo maneno kama vile
na, sana, kwa, ni, ingawa na kadhalika yana maana pasipokuwa na virejelewa. Pili, ni
kwamba zaidi ya tungo moja zinaweza kurejelea kitu kile kile. Kwa mfano tungo “nyota
ya asubuhi” na “nyota ya jioni” ni tungo mbili tofauti lakini zinarejelea kitajwa kimoja
yaani sayari ya Zuhura.


Nadharia nyingine inayojaribu kuelezea maana ya maana ni nadharia ya dhana ambayo
inadai kuwa, maana ya tungo ni dhana au taswira inayoibuliwa akilini mwa mtu na tungo
hiyo. Kwa mantiki hii, badala ya kuhusisha maana na vitu halisi moja kwa moja, nadharia
hii inahusisha maana na wazo, taswira au hisia anazopata mtu pindi tungo husika
itajwapo. Upungufu wa nadharia hii ni kwamba, dhana si bainifu kwani haitabiri
chochote na haichunguziki. Pia, watu hupata dhana tofauti katika tungo moja.


Nadharia ya mwitiko ni nadharia nyingine inayojaribu kuelezea nini maana ya maana. Hii
ni nadharia inayojikita kwenye mawazo ya Bloomfield (1933:139), kwamba maana ya
tungo ni hali ambamo msemaji hutamka tungo hiyo na mwitiko unaoibuliwa na
msikilizaji. Nadharia hii inadai kuwa maana ya tungo ni lazima iwe na uhusiano na
mwitiko unaoendana na tungo hiyo. Hii inajaribu kuelezea uhusiano uliopo kati ya
wanajamii na malimwengu.


Kwa mujibu wa mtazamo wa nadharia hii, tungo mbili zitakuwa na maana moja kama
zinatokana na uchocheo mmoja na pia kuna mwitiko sawa. Kama tukitafsiri uhusiano wa
uchocheo na mwitiko kwa maana ya msingi, watu wasemacho katika mazingira tofauti na
mwitiko wao kutoka kwa wasemacho wengine hakiwezi kuwa sawa vya kutosha kuleta
uhusiano huo na maana. Kasoro za nadharia hii ni pamoja na kwamba, watu huwa na
mwitiko tofauti katika uchocheo wa aina moja kutokana na jinsi wanavyochukulia
uchocheo huo.




                                                                                      2
Kwa ufupi, nadharia za kitajwa, dhana na mwitiko zinachukulia kuwa, maana ya tungo ni
kile kinachorejelewa na tungo au dhana inayoambatana na tungo hiyo au mwitiko
unaosababishwa na uchocheo wa tungo hiyo (Fodor 1980:13). Kimsingi nadharia hizi
hazitakuwa msingi wa insha hii.


Nadharia nyingine inayojaribu kuelezea maana ya maana ni nadharia ya matumizi. Hii
ndiyo nadharia itakayojadiliwa kwa undani katika insha hii. Nadharia hii inahusishwa
moja kwa moja na mwanafalsafa Ludwig Wittgenstein (1963:43) anayedai kuwa maana
ya neno ni matumizi yake katika lugha.


Kutokana na nadharia hii, ni makosa kuchukulia maana kama kitu kinachojitosheleza.
Jambo la msingi ni kuangalia namna lugha inavyotumika na kwa jambo gani ua kuashiria
nini. Nadharia hii inazingatia kanuni ambazo zinaongoza katika kuamua matumizi au
kiwango cha tungo zenye maana.


Kimsingi, nadharia hii inakosoa nadharia zilizotangulia (kama zilivyoelezewa hapo juu)
ambazo ni nadharia ya kitajwa, dhana na mwitiko. Katika kiwango cha semo, tunapata
maana ya tungo hiyo kutokana na jinsi ilivyotumika. Hii ina maana kwamba, maana ya
tungo inabainika kwa kutokana na matumizi yake.


Kwa mujibu wa Wittgenstein (keshatajwa) ni makosa kujaribu kunasibisha maana katika
neno fulani au kuliwekea neno fulani maana fulani ya msingi. Kinyume chake anadai
kuwa, maana ya neno au tungo inapatikana kutokana na muktadha wa matumizi, ambayo
ni pamoja na uelewa wa nyuma na mtazamo wa maisha ambayo wahusika
wanashirikiana. Kwa mfano; tungo “amevaa miwani” inaweza kuwa na maaa ya amelewa
ua amevaa kitu kinachomsaidia aone vizuri au anajifanya haoni kutegemea na muktadha
wa matumizi yake.


Kwa mujibu wa Wittgenstein, ili kuelewa maana ya tungo fulani haina budi kuwa na
uelewa mkubwa kuhusu matumizi yake ikiwa ni pamoja na imetumika wapi. Hapa




                                                                                    3
anataka kuonesha jinsi muktadha wa matumizi na uhusiano wa msemaji na msemeshwaji
vinavyoathiri maana ya tungo. Kwa mfano, uhusiano wa kijamii kati ya wahusika.


Jambo lingine la nadharia hii ni kwamba, inajihusisha zaidi na mazingira ya utumizi wa
tungo badala kuangalia kitajwa, dhana au mwitiko vinavyorejelewa na tungo hiyo. Kwa
kuzingatia hoja hii, nadharia za tendo uneni na utabia zinaongozwa kwa kiasi fulani na
mawazo ya nadharia hii.


Wittgenstein anasisitiza kuwa, lugha ina dhima nyingi na sio tu kuelezea dhana fulani au
kutaja kitu fulani. Pamoja na kudokeza jambo, kuongea kunatenda vitendo ambavyo ni
pamoja na kuuliza, kutania, kuomba, kushawishi na kadhalika. Hapa ndipo dhana ya
tendo uneni, inayojaribu kuelezea jinsi watu wanavyotumia lugha na kutenda jambo
inapoingia.


Jambo la kuzingatia ni kwamba, kuna vitu vilivyo nje ya dhana au kitajwa. Viashiria
vinavyobainisha semo kuwa ombi au amri ni pamoja na viashiria vya mwili vya
mazungumzo kama vile mjongeo wa macho, midomo au mabega, kidatu, kiimbo, hadhi
ya kijamii na kadhalika.


Kwa kuzingatia hili, tunashawishika kusema kuwa, maana ya tungo inategemea
muktadha mzima wa matumizi na sio tu katika matumzi funge. Kwa mantiki hii, dhima
ya lugha katika muktadha wa kijamii inatiliwa maanani (Austin na Grice)2.


Kutokana na hoja hizi, Wittgenstein anahitimisha kuwa, maana haiwezi kuelezwa kwa
misingi ya utabirikaji, kwani maana inaendana na vigezo vya kijamii kuhusu ni tabia ipi
ya ukweli au uongo. Hoja hii inapingana na mtazamo kuwa, tunaweza kumuelezea
mmilisi wa lugha kama mtu anayeelewa sarufi ya lugha akilini tu.




2
    http:/www.shunley.eril.net/armoore/


                                                                                      4
Kwa ufupi, nadharia ya matumizi inajaribu kutatua matatizo yanayojitokeza katika
nadharia zilizotangulia kwa kuzingatia muktadha wa tungo inayotumika. Hii inatokana na
ukweli kwamba, maana ya neno au tungo inatokana na muktadha wa matumizi yake.
Kwa kuzingatia hoja hii, ni vyema kuungana na Ullmann (keshatajwa) anayeeleza kuwa,
maana ichukuliwe kama mfumo wa mahusiano ya kimuktadha, fonetiki, sarufi,
leksografia na semantiki.


MAREJEO
Austin, J. L. (1975). How to do things with words. Oxford: Oxford University Press


Bloomfield L (1933), Language, London-New York. Routledge and Legan Paul


Floor J.D.(1980) semantics; theory of meaning in Generetive Grammar Harvad university
press, Cambridge.


Ullmann. S.(1964).    Semantics: An Introdactio to the Science of Meaning. Alden
Press.Oxford.


http:/www.shunley.eril.net/armoore/




                                                                                     5

More Related Content

What's hot

Literary approach to translation theory
Literary  approach to translation theoryLiterary  approach to translation theory
Literary approach to translation theoryAbdullah Saleem
 
semantics and pragmatics (1)
semantics and pragmatics (1)semantics and pragmatics (1)
semantics and pragmatics (1)ramazan demirtas
 
Speech acts theory in sociolinguistics
Speech acts theory in sociolinguistics Speech acts theory in sociolinguistics
Speech acts theory in sociolinguistics Aseel K. Mahmood
 
Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)
Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)
Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)Mwl. Mapesa Nestory
 
Philosophical approaches to translation
Philosophical approaches to translationPhilosophical approaches to translation
Philosophical approaches to translationHabibeh khosravi
 
Gender and discourse difference= an investigation of discourse markers in per...
Gender and discourse difference= an investigation of discourse markers in per...Gender and discourse difference= an investigation of discourse markers in per...
Gender and discourse difference= an investigation of discourse markers in per...Bhe Si
 
Discourse analysis
Discourse analysisDiscourse analysis
Discourse analysisVale Caicedo
 
The Different Theories of Semantics
The Different Theories of Semantics The Different Theories of Semantics
The Different Theories of Semantics Nusrat Nishat
 
Fairclough et al, critical discourse analysis
Fairclough et al, critical discourse analysisFairclough et al, critical discourse analysis
Fairclough et al, critical discourse analysisSamira Rahmdel
 
Computational stylistics ppt
Computational stylistics pptComputational stylistics ppt
Computational stylistics pptsyila239
 

What's hot (20)

TAFSIRI NA UKALIMANI
TAFSIRI NA UKALIMANITAFSIRI NA UKALIMANI
TAFSIRI NA UKALIMANI
 
Mjengo wa tungo 3
Mjengo wa tungo 3Mjengo wa tungo 3
Mjengo wa tungo 3
 
Literary approach to translation theory
Literary  approach to translation theoryLiterary  approach to translation theory
Literary approach to translation theory
 
semantics and pragmatics (1)
semantics and pragmatics (1)semantics and pragmatics (1)
semantics and pragmatics (1)
 
Speech acts theory in sociolinguistics
Speech acts theory in sociolinguistics Speech acts theory in sociolinguistics
Speech acts theory in sociolinguistics
 
SYSTEMIC FUNCTIONAL LINGUISTICS: INTRODUCTION
SYSTEMIC FUNCTIONAL LINGUISTICS: INTRODUCTIONSYSTEMIC FUNCTIONAL LINGUISTICS: INTRODUCTION
SYSTEMIC FUNCTIONAL LINGUISTICS: INTRODUCTION
 
Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)
Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)
Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)
 
Philosophical approaches to translation
Philosophical approaches to translationPhilosophical approaches to translation
Philosophical approaches to translation
 
Gender and discourse difference= an investigation of discourse markers in per...
Gender and discourse difference= an investigation of discourse markers in per...Gender and discourse difference= an investigation of discourse markers in per...
Gender and discourse difference= an investigation of discourse markers in per...
 
Discourse analysis
Discourse analysisDiscourse analysis
Discourse analysis
 
The Different Theories of Semantics
The Different Theories of Semantics The Different Theories of Semantics
The Different Theories of Semantics
 
Fairclough et al, critical discourse analysis
Fairclough et al, critical discourse analysisFairclough et al, critical discourse analysis
Fairclough et al, critical discourse analysis
 
CHIMBUKO LA FASIHI
CHIMBUKO LA FASIHICHIMBUKO LA FASIHI
CHIMBUKO LA FASIHI
 
Stylistics
Stylistics Stylistics
Stylistics
 
Stylistics
StylisticsStylistics
Stylistics
 
flowerdew basics
 flowerdew basics  flowerdew basics
flowerdew basics
 
Genre
GenreGenre
Genre
 
Tafsiri na ukalimani
Tafsiri na ukalimaniTafsiri na ukalimani
Tafsiri na ukalimani
 
Computational stylistics ppt
Computational stylistics pptComputational stylistics ppt
Computational stylistics ppt
 
Social semiotics
Social semioticsSocial semiotics
Social semiotics
 

Maana ya maana!

  • 1. Maana ya maana ni mojawapo ya dhana inayoibua changamoto katika nadharia za lugha (Ullman 1964:54). Kwa muda mrefu kumekuwepo na maelezo ya namna mbalimbali kutoka kwa wataalamu kama vile wanafalsa, wanasaikolojia na wanaisimu kuhusu nini maana ya maana. Mjadala huu umekuwa na kutoelewana kwingi kati ya wataalamu hawa. Kutakana na hali hii, kubainisha maana ya maana wataalamu mbalimbali wamejaribu kulipunguzia wigo na kujishughulisha na maana ya neno kwa kulipa sifa bainifu. Japo kwa kutumia kigezo hiki, ugumu wa kuelezea maana ya maana unapunguzwa kwa kiasi fulani, lakini bado tatizo la msingi kuhusu nini maana ya maana lipo pale pale. Hii ni kwa sababu vipashio vingi vya kiisimu (hata tukiachilia mbali maneno) vimefumbata maana fulani. Mathalani, mofimu za maneno hufumbata maana fulani, kwani maana za msingi zinazotokana na muunganiko wa mofimu hizo huleta maana ya jumla ya neno husika. Katika insha hii, ‘maana’ itamaanisha mchanganyiko wa uhusiano wa kimuktadha, fonimu, sarufi, leksikografia na semantiki ambapo kila kimoja kinachangia katika maana ya msingi ya tungo kwa kuzingatia muktadha wa matumizi1. Kwa kuwa swali la “nini maana ya maana” limekuwa ni jambo la mjadala lenye kutoelewana kwingi, nadharia mbalimbali zimeasisiwa ili kujaribu kuondoa uvulivuli unaofumbatwa katika maana ya maana. Miongoni mwa nadharia hizo ni pamoja na nadharia ya kitajwa, nadharia ya dhana, nadharia ya mwitiko na nadharia ya matumizi. Katika insha hii, nadharia ya matumizi kuhusu nini maana ya maana ndiyo itakayojadiliwa kwa mapana. Hata hivyo, nadharia nyingine zitaelezewa japo kwa ufupi ili kuweka mtiririko wa mantiki. Tukianza na nadharia ya kitajwa, hii inaangalia uhusiano kati ya tungo na kitu ua vitu katika ulimwengu halisi. Kwa mantiki hii, maana ya tungo inapatikana kwa kuangalia uhusiano baina ya neno hilo na kitu kinachorejelewa. Kwa kiasi fulani, nadharia hii ina ukweli ndani yake kwani kila lugha ina maneno mengi yahusuyo ulimwengu na 1 Fodor (1980) 1
  • 2. malimwengu kulingana na wanajamii walivyoumega ulimwengu wao na kuainisha malimwengu yaliyomo. Hata hivyo, mtazamo huu una mapungufu fulani ikiwa ni pamoja na kwamba, si kila leksimu yenye maana inarejelea kitu fulani. Yapo maneno kama vile na, sana, kwa, ni, ingawa na kadhalika yana maana pasipokuwa na virejelewa. Pili, ni kwamba zaidi ya tungo moja zinaweza kurejelea kitu kile kile. Kwa mfano tungo “nyota ya asubuhi” na “nyota ya jioni” ni tungo mbili tofauti lakini zinarejelea kitajwa kimoja yaani sayari ya Zuhura. Nadharia nyingine inayojaribu kuelezea maana ya maana ni nadharia ya dhana ambayo inadai kuwa, maana ya tungo ni dhana au taswira inayoibuliwa akilini mwa mtu na tungo hiyo. Kwa mantiki hii, badala ya kuhusisha maana na vitu halisi moja kwa moja, nadharia hii inahusisha maana na wazo, taswira au hisia anazopata mtu pindi tungo husika itajwapo. Upungufu wa nadharia hii ni kwamba, dhana si bainifu kwani haitabiri chochote na haichunguziki. Pia, watu hupata dhana tofauti katika tungo moja. Nadharia ya mwitiko ni nadharia nyingine inayojaribu kuelezea nini maana ya maana. Hii ni nadharia inayojikita kwenye mawazo ya Bloomfield (1933:139), kwamba maana ya tungo ni hali ambamo msemaji hutamka tungo hiyo na mwitiko unaoibuliwa na msikilizaji. Nadharia hii inadai kuwa maana ya tungo ni lazima iwe na uhusiano na mwitiko unaoendana na tungo hiyo. Hii inajaribu kuelezea uhusiano uliopo kati ya wanajamii na malimwengu. Kwa mujibu wa mtazamo wa nadharia hii, tungo mbili zitakuwa na maana moja kama zinatokana na uchocheo mmoja na pia kuna mwitiko sawa. Kama tukitafsiri uhusiano wa uchocheo na mwitiko kwa maana ya msingi, watu wasemacho katika mazingira tofauti na mwitiko wao kutoka kwa wasemacho wengine hakiwezi kuwa sawa vya kutosha kuleta uhusiano huo na maana. Kasoro za nadharia hii ni pamoja na kwamba, watu huwa na mwitiko tofauti katika uchocheo wa aina moja kutokana na jinsi wanavyochukulia uchocheo huo. 2
  • 3. Kwa ufupi, nadharia za kitajwa, dhana na mwitiko zinachukulia kuwa, maana ya tungo ni kile kinachorejelewa na tungo au dhana inayoambatana na tungo hiyo au mwitiko unaosababishwa na uchocheo wa tungo hiyo (Fodor 1980:13). Kimsingi nadharia hizi hazitakuwa msingi wa insha hii. Nadharia nyingine inayojaribu kuelezea maana ya maana ni nadharia ya matumizi. Hii ndiyo nadharia itakayojadiliwa kwa undani katika insha hii. Nadharia hii inahusishwa moja kwa moja na mwanafalsafa Ludwig Wittgenstein (1963:43) anayedai kuwa maana ya neno ni matumizi yake katika lugha. Kutokana na nadharia hii, ni makosa kuchukulia maana kama kitu kinachojitosheleza. Jambo la msingi ni kuangalia namna lugha inavyotumika na kwa jambo gani ua kuashiria nini. Nadharia hii inazingatia kanuni ambazo zinaongoza katika kuamua matumizi au kiwango cha tungo zenye maana. Kimsingi, nadharia hii inakosoa nadharia zilizotangulia (kama zilivyoelezewa hapo juu) ambazo ni nadharia ya kitajwa, dhana na mwitiko. Katika kiwango cha semo, tunapata maana ya tungo hiyo kutokana na jinsi ilivyotumika. Hii ina maana kwamba, maana ya tungo inabainika kwa kutokana na matumizi yake. Kwa mujibu wa Wittgenstein (keshatajwa) ni makosa kujaribu kunasibisha maana katika neno fulani au kuliwekea neno fulani maana fulani ya msingi. Kinyume chake anadai kuwa, maana ya neno au tungo inapatikana kutokana na muktadha wa matumizi, ambayo ni pamoja na uelewa wa nyuma na mtazamo wa maisha ambayo wahusika wanashirikiana. Kwa mfano; tungo “amevaa miwani” inaweza kuwa na maaa ya amelewa ua amevaa kitu kinachomsaidia aone vizuri au anajifanya haoni kutegemea na muktadha wa matumizi yake. Kwa mujibu wa Wittgenstein, ili kuelewa maana ya tungo fulani haina budi kuwa na uelewa mkubwa kuhusu matumizi yake ikiwa ni pamoja na imetumika wapi. Hapa 3
  • 4. anataka kuonesha jinsi muktadha wa matumizi na uhusiano wa msemaji na msemeshwaji vinavyoathiri maana ya tungo. Kwa mfano, uhusiano wa kijamii kati ya wahusika. Jambo lingine la nadharia hii ni kwamba, inajihusisha zaidi na mazingira ya utumizi wa tungo badala kuangalia kitajwa, dhana au mwitiko vinavyorejelewa na tungo hiyo. Kwa kuzingatia hoja hii, nadharia za tendo uneni na utabia zinaongozwa kwa kiasi fulani na mawazo ya nadharia hii. Wittgenstein anasisitiza kuwa, lugha ina dhima nyingi na sio tu kuelezea dhana fulani au kutaja kitu fulani. Pamoja na kudokeza jambo, kuongea kunatenda vitendo ambavyo ni pamoja na kuuliza, kutania, kuomba, kushawishi na kadhalika. Hapa ndipo dhana ya tendo uneni, inayojaribu kuelezea jinsi watu wanavyotumia lugha na kutenda jambo inapoingia. Jambo la kuzingatia ni kwamba, kuna vitu vilivyo nje ya dhana au kitajwa. Viashiria vinavyobainisha semo kuwa ombi au amri ni pamoja na viashiria vya mwili vya mazungumzo kama vile mjongeo wa macho, midomo au mabega, kidatu, kiimbo, hadhi ya kijamii na kadhalika. Kwa kuzingatia hili, tunashawishika kusema kuwa, maana ya tungo inategemea muktadha mzima wa matumizi na sio tu katika matumzi funge. Kwa mantiki hii, dhima ya lugha katika muktadha wa kijamii inatiliwa maanani (Austin na Grice)2. Kutokana na hoja hizi, Wittgenstein anahitimisha kuwa, maana haiwezi kuelezwa kwa misingi ya utabirikaji, kwani maana inaendana na vigezo vya kijamii kuhusu ni tabia ipi ya ukweli au uongo. Hoja hii inapingana na mtazamo kuwa, tunaweza kumuelezea mmilisi wa lugha kama mtu anayeelewa sarufi ya lugha akilini tu. 2 http:/www.shunley.eril.net/armoore/ 4
  • 5. Kwa ufupi, nadharia ya matumizi inajaribu kutatua matatizo yanayojitokeza katika nadharia zilizotangulia kwa kuzingatia muktadha wa tungo inayotumika. Hii inatokana na ukweli kwamba, maana ya neno au tungo inatokana na muktadha wa matumizi yake. Kwa kuzingatia hoja hii, ni vyema kuungana na Ullmann (keshatajwa) anayeeleza kuwa, maana ichukuliwe kama mfumo wa mahusiano ya kimuktadha, fonetiki, sarufi, leksografia na semantiki. MAREJEO Austin, J. L. (1975). How to do things with words. Oxford: Oxford University Press Bloomfield L (1933), Language, London-New York. Routledge and Legan Paul Floor J.D.(1980) semantics; theory of meaning in Generetive Grammar Harvad university press, Cambridge. Ullmann. S.(1964). Semantics: An Introdactio to the Science of Meaning. Alden Press.Oxford. http:/www.shunley.eril.net/armoore/ 5