Diese Präsentation wurde erfolgreich gemeldet.
Wir verwenden Ihre LinkedIn Profilangaben und Informationen zu Ihren Aktivitäten, um Anzeigen zu personalisieren und Ihnen relevantere Inhalte anzuzeigen. Sie können Ihre Anzeigeneinstellungen jederzeit ändern.

Sadaka na-maana-ya-utoaji

28.252 Aufrufe

Veröffentlicht am

 • Sex in your area is here: ❶❶❶ http://bit.ly/2F90ZZC ❶❶❶
     Antworten 
  Sind Sie sicher, dass Sie …  Ja  Nein
  Ihre Nachricht erscheint hier
 • Follow the link, new dating source: ♥♥♥ http://bit.ly/2F90ZZC ♥♥♥
     Antworten 
  Sind Sie sicher, dass Sie …  Ja  Nein
  Ihre Nachricht erscheint hier
 • Kwa kweli Mungu ametupatia vyote..... kikubwa ni kuzifuata kanuni zake ili tuweze kupokea baraka tulizopewa. Ubarikiwe sana mtumishi wa Jehova
     Antworten 
  Sind Sie sicher, dass Sie …  Ja  Nein
  Ihre Nachricht erscheint hier

Sadaka na-maana-ya-utoaji

 1. 1. SADAKA NA DHANA YA UTOAJI (The concept of Giving and Offerings) UTANGULIZI : MAANDIKO NA MISTARI YA KUSIMAMIAKumb 28: 1-14; “Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunzakuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana Mungu wako, atakapokutukuza juuya mataifa yote ya dunia; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata, usikiapo sauti ya Bwana,Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako,na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, nawadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa utokapo. Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako,kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako;naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. Bwana atakuweka uwe taifa takatifukwake … na mataifa yote ya dunia watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofukwako. Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako … Bwanaatakufunulia hazina yake nzuri … nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe. Bwanaatakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakaposikizamaagizo ya Bwana, Mungu wako ... kuyaangalia na kuyafanya; msipokengeuka … kwa lolote,kwenda mkono wa kuume wala kushoto…” Kumb 8:10-20; “Nawe utakula ushibe, utamshukuru Bwana, Mungu wako, kwa nchi nzurialiyokupa. Jihadhari usije ukamsahau Bwana, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, nahukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo. Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, nakujenga nyumba nzuri, na kukaa ndani yake; na makundi yako ya ng’ombe na kondooyatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu chakokitakapoongezeka; basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoakatika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa … Hapo usiseme moyoni mwako, nguvu zangu nauweza wa mkono wangu, ndio ulionipatia utajiri huo. Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako,maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake …” 1
 2. 2. SEHEMU YA KWANZA KWANINI MUNGU ANATUPA UTAJIRI MALI NA FEDHA ?1. ILI KUIMARISHA AGANO LAKE (UFALME WAKE)* Kumb 8:18 (12-18) - Agano la Mungu kwa siku za leo, ni Agano JIPYA. Kuimarisha Agano lake maana yake; ni kuimarisha kazi ya injili ya Yesu Kristo, ili wokovu uwafikie watu wote. - Gal 3:11,23-26,29; Rum 10:13 – 15; Fillip 4:15 –192. ILI KUVITUMIA KWA MAHITAJI YETU BINAFSI *Yoh16:24 Soma tena 1Timotheo 6:17 na 2Wakorintho 9:8 – 11 - Mungu kama Baba yetu na kama Mchungaji Mwema, anajali sana mahitaji yetu na haja zetu au shauku za mioyo yetu. (vitu vitupavyo furaha na kuridhika). Ndio maana hutupa utajiri, ili tufurahie maisha. - Si mapenzi ya Mungu tuwe masikini. Ndio maana Yesu alifanyika maskini (kimwili) ili kwa umasikini wake, (sisi) tupate kuwa matajiri (kimwili)” 2 Kor 8:9 - Ni mapenzi ya Mungu tupate vitu vyote vitakavyotufanya tufurahie maisha yetu duniani. Nyumba nzuri, mavazi mazuri, chakula kizuri, kazi nzuri, magari mazuri, biashara nzuri, mifugo mizuri, mashamba mazuri, mshahara mzuri, n.k. (Zab23:1- 2; Fil 4:6-7,19; Zab37:4; Zab145:17- 19)3. ILI KUWAGAWIA WAHITAJI *2KOR 9:8-13; Pia soma 1Timotheo 6:17-19; Waefeso 4:28 na Luka 6:38. - Tunapowapa wahitaji fedha, nguo, viatu, chakula au vitu vya aina nyingine ili kuwasaidia kimaisha, tunapata thawabu kubwa kwa Mungu. Kumsaidia mhitaji kitu, ni kumpa Mungu. Hebu soma vizuri Mathayo 25:31-40; Mathayo 10:40 – 42 na Yohana 13:20. - Mungu ametupa mali, fedha na utajiri wa namna nyingi ili tuwasaidie wahitaji na masikini, wajane na yatima, wagonjwa na walemavu. Thawabu yake ni kubwa mbele za Mungu, na Mungu ataona sababu ya kukupa tena na kukuzidishia. Tena Mungu atakufanya uwe njia/mkondo wa baraka zake kwa watu wengine. 2Kor 8:14-15, Mdo 20:35 2
 3. 3. MAANA YA UTOAJI WA SADAKA ~ DHANA YA UTOAJI ~ Utoaji wa sadaka unasimama katika kweli zifuatazo;1. KUTOA SADAKA NI NAMNA YA KUMHESHIMU MUNGU, KUMTAMBUA MUNGU NA KUMTHAMINI MUNGU KUWA NDIYE ATUPAYE UTAJIRI/VITU. *Kumb 8:10 –20, Mith 3:9 – 10 “Mheshimu Bwana kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, na mashinikizo yako yatafurika divai mpya”… Tena “hawatakuwepo masikini kwenu, kwakuwa Bwana atakubarikia kweli, katika nchi akupayo Bwana Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako.” Kumb 15:4 Mungu ndiye chanzo cha baraka zote tulizonazo. Sadaka ni ishara ya kumtambua na kumthanini kuwa yeye Mungu tunayemtolea sadaka, ndiye mpaji wa hizo mali na vitu vyote. Kwa ufahamu huu, tunatakiwa kumpa Mungu kile cha kwanza kabisa, tena kile kilicho bora zaidi. (“The first and the best”).2. SADAKA NI NAMNA YA KUONYESHA SHUKURANI KWA MUNGU. *Zab 116:18,12-13, Zab103:1-5, Zab 136:1-3 Sadaka ni namna ya kumshukuru Mungu kwa wema wake, fadhili zake na matendo yake makuu katika maisha yetu. Matendo ya Mungu kwetu ni mengi na makuu. Sadaka zetu ni njia tu ya kumshukuru, ni kiwakilishi cha shukurani zetu kwake, kwa maana hatuwezi kumlipa kwa mema anayotutendea *2Nyak 20:21 (1-30)3. SADAKA NI NAMNA YA KUMUABUDU MUNGU *Mwa 8:15-22; Ebr 7:1-3; Mwa 4:1-7 Utoaji ni heshima kwa anayepewa. Ndio maana washindi hutunukiwa zawadi/tuzo, kwasababu wanastahili. Vivyo hivyo kwa Mungu wetu; kwa kuwa yeye ni Mkuu, Mtakatifu, na Muweza wa yote, anastahili kuabudiwa. Hivyo sadaka zetu ni ishara ya kumtukuza, kumheshimu na kumuabudu Mungu. 3
 4. 4. 4. UTOAJI WA SADAKA NI NAMNA YA KUONYESHA UPENDO WAKO KWA MUNGU *Luk 7:36-48 Utoaji ni ishara ya Upendo. Unaweza kutoa bila kupenda, lakini huwezi kupenda bila kutoa. Utoaji mwingi, husukumwa na upendo mwingi. Upendo kidogo husababisha utoaji mdogo. Kwasababu ya upendo wa Mungu kwetu, alimtoa mwanaye.(Yoh 3:16; Rum 5:8). Kwasababu ya upendo wa Yesu kwetu, aliutoa uhai wake (Yoh 15:13.) Kwasababu ya kusamehewa dhambi nyingi sana, Yule kahaba akapenda sana, na ndio maana akatoa sana yaani nyingi/kubwa (Luk 7:36-48). Utoaji ni ishara ya Upendo. Katika *Mith 8:17 Mungu anasema “Nawapenda wale wanipendao, nao wanitafutao kwa bidii, wataniona.” Je, unadhani Mungu anawatambuaje wale wanaompenda sana? Moja ya ishara ya wazi wazi ya upendo ni ‘utoaji’ (giving & offering). Upendo si kwa maneno tu, ni kwa matendo zaidi. Kama kweli unampenda Mungu, hauhitaji kutuambia, wenyewe tutaona jinsi unavyojishughulisha na mambo yake. Kumbuka kuwa matendo yetu yanaongea kuliko maneno yetu. Tunajua kuwa Mungu anawapenda watu wote (hata wenye dhambi pia) kama ilivyoanndikwa katika Yohana 3:16 na Warumi 5:8 kwamba Mungu alitupenda tungali wenye dhambi. Lakini kwa kusoma Mithali 8:17 inayosema “nawapenda wale wanipendao…” tunagundua Mungu anawapenda watu fulani zaidi kwa upendo mwingine tofauti na ule wa watu wote (Yoh 3:16). Hii ni ngazi nyingine kabisa ya upendo. Ni ngazi ya juu zaidi au class ya juu zaidi. Ni upendo wa ‘kirafiki’. Kupewa upendo wa ngazi ya juu, upendo wa kirafiki, ni lazima nawe ufanye kitu cha ziada kwa Mungu. Hivyo ukimpenda Mungu kwa upendo wa ziada, naye atakuonyesha upendo wa ziada, tofauti na ule wa kijumla anaowapenda nao watu wote (Yoh 3:16 na Rum 5:8). Atakupenda kipekee, upendo wa kirafiki, kwasababu Mungu anawapenda wale wamendao.5. UTOAJI WA SADAKA NI USHIRIKA WETU KATIKA KAZI YA MUNGU. * Malaki 3:7-12; Rum 10:13-15;* Hagai 1:3-11 Mungu ametupa mali na utajiri, ili tushiriki katika ujenzi wa ufalme wake duniani Mungu anatutaka tutoe sadaka nzuri “Ili kiwemo chakula nyumbani mwa Mungu” (Kanisani / Huduma ya Injili) Kama kweli unampenda Mungu, hauhitaji kutuambia, wenyewe tutaona jinsi unavyojishughulisha na mambo yake. Matendo yanaongea kuliko maneno. 4
 5. 5. Moja ya sabau kwanini Mungu amepitisha utajiri na fedha katika mikono yetu ni ili kuimarisha agano lake (ufalme wake) * Kumb 8:18 (12-18). Agano la Mungu kwa siku za leo, ni Agano JIPYA. Kuimarisha Agano lake maana yake; ni kuimarisha kazi ya injili ya Yesu Kristo, ili wokovu uwafikie watu wote. (Rum 10:13 – 15). Nyumba ya Mungu na kazi ya Mungu isipopungukiwa na kitu, injili itasonga mbele kwa kasi na kwa urahisi zaidi. Ndio maana Mungu ametupatia pesa, utajiri na mali. (2Kor 8:1-15)6. UTOAJI WA SADAKA NI UPANDAJI WA MBEGU ILI KUPOKEA (KUVUNA) BARAKA NA UTAJIRI MWINGI ZAIDI * 2Kor 9:6, 2Kor 9:8,Gal 6:7 – 10, Malaki 3:10 – 12, Luk 6:38, Mtoaji wa sadaka ni kama mpanzi wa mbegu shambani. Mbegu moja huzaa nyingi zaidi kuliko ile iliyapandwa. Tunapotoa sadaka, tunatakiwa kutoa huku tukitarajia kupokea vingi kulilo tulivyotoa. Atakaye mavuno mengi ni lazima:- i. Achague(atenge) mbegu bora zaidi (the best) ii. Afuate masharti ya upandaji (Kilimo)(Isa 1:19) iii. Apande mbegu nyingi (2kor 9:8) Kwa kutokufuata maagizo na kanuni za Mungu katika utoaji wa sadaka, wengi hawavuni kama vile ahadi za Mungu zilivyo. Matokeo yake, hukata tama kutarajia baraka katika sadaka watoazo. Ndipo huanza kutoa kidogo kidogo sana kuepuka hasara. Lakini kama mpanzi alipanda kwa kufuata kanuni sahihi za kilimo, siku zote mavuno yake huwa mengi zaidi kuliko mbegu alizopanda. Vivyo hivyo, kila atoae matoleo (sadaka) vizuri, kwa kufuata maagizo na kanuni za Mungu, hupokea kwa wingi zaidi ya vile alivyotoa. Kila apandaye vizuri, huvuna vizuri. Utoaji ni njia ya Mungu kutupa na kutujaza tunavyohitaji *1Fal 17:1-16 Mungu ndiye alieyewaka kanuni ya kupanda na kuvuna, kutoa na kupokea. Hivyo, mara nyingi tunapomwomba Mungu atubariki/atujaze mahitaji yetu, anatuletea mafasi ya kutoa kwanza, ili tupokee mahitaji yetu tumwombayo. Kwasababu, ndiyo kanuni ya kupokea. Ni ajabu, sicho tunachotegemea (kutoa wakati wewe binafsi unahitaji). Badala ya Mungu kukupa moja kwa moja kitu ulichomwomba, anakuletea nafsi ya kutoa hicho hicho kidogo ulichonacho, kiwe kama mbegu, ili hatimaye upokee (uvune) kile ulichomwomba, na hata zaidi ya ulivyoomba. 5
 6. 6. Biblia pia inasema hivi katika Waefeso 3:20 na Wafilipi 4:15-19; kwamba, “Basi atakuzwe Mungu awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tumwombaye au kuliko yote tuyawazayo, kwa kadri ya nguvu, itendayo kazi ndani yetu” (Efe 3:20; Fil 4:15-19). 1Wafalme 17:13-16; Eliya akamwambia (yule mama mjane); usiogope (kutoa hicho kidogo kilichobaki) … enenda ukafanye kwa ajili yangu (kwa maana ukinipa mimi, utakuwa umempa Mungu) na Mungu wa Isarael anasema, unga wako wala mafuta yako hayatapunguka kamwe, mpaka njaa itakapoondoka juu ya nchi. Yaani Mungu atavizidisha. Si ajabu anliongezea Kama ukikubali na kutii, utakula mema ya nchi. Lakini ukikataa, utaangamia (kama wengine wanavyoangamia). (Isa 1:19) Si jambo rahisi kutoa wakati wewe mwenyewe umepumgukiwa au una uhitaji. Inahitajika imani kubwa kutoa kidogo kilichobaki, ili uhitai wako ujazwe. Hivyo, usishangae siku utakapomwomba Mungu pesa au vitu, halafu badala ya kukupa, anakuletea mhitaji ili umpe pesa au vitu, au analeta nafasi ya wewe kutoa sadaka. Kumbuka kanuni yake, huwezi kuvuna bila kupanda! Hivyo, ukikubali na kutii, utavuna na kupata mema, tena zaidi ya ulivyotarajia. Hii ni kanuni ya Mungu; ukipanda haba utavuna haba, ukipanda nyingi, utavuna nyingi. Huwezi kuvuna bila kupanda *Malaki 3:10–12, Fil 4:10 – 20, 1Kor 4: 1-2, Mdo 20:35, Luk 6:387. UTOAJI WA SADAKA NI KUWEKA AKIBA MBINGUNI *Luk 12:30-34; Math 6:19-20. Imeandikwa kwamba “Hazina yako ilipo, ndipo moyo wako utakapokuwepo” Je ulishajiouliza? Hivi, akiba yako au hazina yako huko mbinguni ina kazi gani? Au inafanya nini? Mambo yafuatayo, ni baadhi tu ya kazi za hazina yako iliyoko mbinguni. (i) Kutusaidia wakati wa uhitaji “basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji” Ebr 4:16 Mtume Paulo alisema ninajua kupungukiwa na ninajua kuwa na vingi. Katika mambo yote nimefundishwa kushiba na kuona njaa (Wafilipi 3:12.) Katika maisha kuna vipindi vya kupungukiwa na kuna vipindi vya kujazwa. Katika nyakati zote tunayaweza yote kwa yeye Yesu anayetutia nguvu. 6
 7. 7. Huwa kuna neena maalum kutoka kwa Mungu, inayoachiliwa ili kutuvusha katikavipindi vigumu maishani mwetu, vipindi vya uhitaji. Sikia Neno linavyosema; “basi natukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema yakutusaidia wakati wa mahitaji” (Waebrania 4:16). Ni hii neema iliyomfanya MtumePaulo kusema nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu (Wafilipi 4:13).Ni kanuni ya Mungu kwamba, huwezi kuvuna bila kupanda. Hivyo, wakati wa uhitajiukikufikia, Mungu atakutaka utoe kitu ili upokee mahitaji yako. Watu wengiwanashangaa kwamba, wakati wamepungukiwa, ule wakati wa uhitaji wao, ndioMungu anaruhusu nafasi ya kutoa ije. Na wengi wanakosa baraka na msaada wa Mungukwasababu hawaelewi utendaji wa kanuni za Mungu. Maana katika uhitaji wao,wamemwomba Mungu awajaze.Lakini kitu cha kushangaza kabisa ni kwamba, badala ya kupokea, wanajikuta katikamazingira ambayo wanaombwa au wanatakiwa watoe kitu. Wengi hawajuai kuwanyakati hizo, ni Mungu aliyeleta nafasi hiyo ya kutoa hicho kidogo kilichobaki ilikanuni yake ifanye kazi na upako wa Mungu uingie kazini kuwaletea mavuno kwakadri ya utii wao katika utoaji. Ukitii utakula mema ya nchi. Kumbuka kilichompatayule mama wa Sarepta katika 1Fal 17:8-16.Hivyo, wakati wa uhitaji ukikufikia, Mungu atakutaka utoe kitu ili upokee mahitajiyako. Lakini, utafanyaje wakati umepatwa na mahitaji ya lazima (emergency) na nafasiya utoaji imekuijia ili uote kitu, na hatimaye Bwana akufungulie madirisha ya mbingunikukupa ulichokuwa unamwomba Mungu, lakini huna cha kutoa? Hapo ndipo ile akibayako mbinguni inaingia kazini. Moyoni mwako Roho atakukumbusha kuwa umawezakuomba neema maalum ya kutusaidia wakati wa mahitaji.Kama una hahika na maisha yako ya utoaji wa sadaka katika kazi mbalimbali za Munguhapa duniani, utajikuta unapewa au anapata ujasiri wa kumwendea Mungu katika kitichake cha rehema, ili akupe neema ya kukusaidia wakati wa uhitaji kwasababu unahazina/akiba kule mbinguni. Kipindi unachotakiwa kutoa ili kuikamilisha kanuni yaMungu ya kupanda na kuvuna, lakini una cha kutoa, hazina yako mbinguni inakupaujasiri wa kuomba neema ya kukuvusha katika kipindi hicho kigumu cha ukata. Lakinikama hazina yako mbinguni iko tupu, then huwezi kupata ujasiri ndani yako, kwasabuunajua kabisa kuwa, akaunti yako mbinguni iko tupu. Huwezi kuwa na uhakika wamsaada wa Mungu. Unaweza ukajikuta unateseka sana katika kipindi cha uhitaji. 7
 8. 8. Ila kwa mtu mtoaji mzuri wa sadaka, siku akiishiwa , ana ujasiri wa kwenda mbele zaMungu kuomba neema ya kumvusha wakati wa mahitaji yake na hakika atapata msaadawa Mungu. Mungu alisha sema katika Neno lake kwamba, vile tunavyo mfanyia yeyekuhusu kazi yake, naye atatufanyia sisi vivyo hivyo katika kazi zetu. Japo kuwaalikuwa anaongea na taifa takatifu la watu aliowaahidi baraka nyingi (kama sisi kanisa)alisema nao katika Malaki hivi,Malaki 3:7-12; (Hebu tuisome mistari hii kwa utaratibu huu; tuanzie mstari wa 9) 9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana! Naam, taifa hili lote (kwasababu) 8 naniibia mimi. Lakini mnasema tumekuibia kwa namna gain? 10 Mmeniibia zaka na dhabihu (sadaka). Leteni zaka kamili ghalani…nami nitawafungulia madirisha ya Mbinguni na kuwamwagieni 12 baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha. Na mataifa yote watawaiteni heri, maana mtakuwa nchi yenye kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi. (lakini) ikiwa baada ya yote hayo hamtaki kunisikiliza, bali mwaendelea kunishika kinyume, ndipo nami nitakwnda kwa kuwashika nanyi kinyume katika ghadhabu yangu; nami nitawaadhibu mara saba katika dhambi zenu. (Walawi 26:27-28)Kwahiyo, kama tunataka msaada wa Mungu katika mahitaji yetu, ni muhimu sana tuwewaaminifu pia na watoaji wazuri wa sadaka zetu, ili zile siku za kudhiliwa zikija,zitukute tuna neema ya kutusaidia katika siku hizo. Wakati tunapokuwa wa fedha zakutosha, watu wengi hawawi na moyo wa kupenda kutoa sadaka nyingi. Wenginewanaona kutoa ni kupoteza. Na wako tayari kuchanga fedha nyingi katika maharusi namasherehe kwa wingi kuliko kutoa sadka katika kazi ya Mungu.Huko ni kutolijua Nemo la Mungu au ni kuto kumwamini Mungu. Hebu tubadili fikrazetu katika utoaji. Kutoa si kupoteza. Wala kutoa si kuchangia. Kutoa ni kuwekeza.Kutoa ni kweka akiba au hazina mbinguni. Neno la Mungu ni hakika. Na Mungu nimwaminifu sana hasa kwa wale watu wanaomcha yeye na kuyashika maagizo yake.“Mungu Mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao,na kushika amri zake.”( Daniel 9:4) 8
 9. 9. (ii) Kutuandalia makao mazuri mbinguni (Yohana 14:1-2) Yesu akasema “…nakwenda kuwaandalia mahali …” Mimi naamini kwamba, tutakapofika mbinguni, tutakuta majumba makubwa ya kifahari, yenye kuta na vitasa vya dhahabu, yameandaliwa kwa ajili yetu. (Ufu 21:1-4, 18,22) Lakini “binafsi” nina wasiwasi kuwa wengi wasiopenda kutoa sadaka nzuri hapa duniani, wakifika mbinguni, si ajabu watakuta hazina zao huko juu, ni ndogo sana, kiasi ambacho hakikutosha kuwezesha watengenezewe makao yao, yenye ubora na uzuri kama wa wengine walioweka “hazina kubwa” kwa utoaji wao wa hapa duniani. Tafakari: Math 20 : 21 – 23 vizuri. Utagundua kwamba, mbinguni kuna utaratibu wa kupangwa viti vya kukalia katika mahali ambapo tutakuwa na Bwana Yesu. Labda ni katika ukumbi wa ibada au pengine ni katika ukumbi wa sherehe/karamu ya Mwanakondoo. Tafakari yangu mimi iko hivi; kama kuna watu watakaokaa karibu na Yesu, basi hii ina maana kwamba, pia wapo watu ambao watakaokaa mbali na Yesu. Ni wazi kwamba hayo ni madaraja (classes) tofauti, japo sote tuko mbinguni. Hebu soma vizuri 1Kor 3:10-15. Kwasababu kazi zingine zitakuwa na ubora wa dhahabu, zingine chuma, udongo, miti na manyasi, haiwezekani hawa wote wakawa katika msatari mmoja. Mimi naamnini, atakaye mletea Bwana mavuno au talanta ya ubora wa dhahabu atalipwa thawabu kubwa zaidi kuliko mtumishi atakayemletea Bwana mavuno ya ubora wa shaba Na huyu wa shaba atalipwa zaidi kuliko yule wa udongo. Hivyo basi, ukaribu wa kiti chako na Yesu kule mbinguni, unategemeana sana ubora wa kazi yako na utumishi wako (utendaji wako) wa kazi ya Bwana hapa duniani. Ubora wa kazi ya mtu ndio utakao mpa nafasi nzuri na tuzo nzuri zaidi mbinguni. Pia wapo watakaokosa kabisa tuzo, ni wale ambao kazi zao zilikuwa za ubora wa miti au manyasi, kwa maana kazi zote zitajaribiwa kwa moto, kazi ya mtu ikitoka katika moto, huyo mtu atapata thawabu/tuzo; lakini kazi ya mtu ikiteketea, mtu huyo atapata hasara, kwasababu hawakufanya kazi ya Mungu vizuri walipokuwa duniani, japo yeye mwenyewe ataokolewa na moto. Kwahiyo, katika ile siku ya hukumu, moto wa Mungu utaijaribu kila kazi ya kila mtu kuona ipo katika ubora wa aina gani. Kama Mungu anashauku ya kufanya zaezi hilo, hivi unadhani anatafuta nini? Kama Mungu hajali ubora au madaraja ya kazi za watu, hili zoezi la upimaji kwa moto, ni la nini basi? 9
 10. 10. Ooh! Ni wazi kwamba; Mungu anajali sana ubora wa kazi zetu. Na ndio kusema anajalisana (yuko interested) na madaraja ya watenda kazi wake (classes). Ndugu yangu,usifanye mchezo. Ni waza na hakika ya kwamba kazi zetu zitapimwa na ni lazimakwamba, kazi zetu zitatofautiana. Hii ni inamaanisha kwamba, hata tuzo zetu nathawabu zetu hazitafanana. Zitatofautiana. Kuna wengine watakuwa na taji zinazong’aasana kuliko wemgine. Kuna wengine, viti vyao vitawekwa wakae karibu sana na Yesukuliko wengine.Kama Yohana aliuona ule mji mtakatifu una upana una urefu wa maili 1500, (Yaani kikama kutoka Cairo ya Misri, mpaka Johanersburg ya Afrika Kusini) Soma Ufu 21:10-16 utaona mwenyewe. Duh! Kwa lugha na mtazamo wa kibinadamu, ina maana kunawatu viti vyao vitawekwa umbali ambao hawataweza hata kumwaona Yesu mezanikwake (kama ni ibadani au ni chakulani). Labda kwasababu si duniani bali ni mbinguni,inawezekana kutakuwa na mwanda wa tofauti. Sina uhakika. Wewe je?Well, kwa ufupi, Hiki ndicho kinachonifanya niamini kwamba, si ajabu huko mbingunikukawa na madaraja (classes) tofauti (nionavyo mimi). Basi, si ajabu pia, hata ubora wanyumba zetu mbinguni zita tofautiana, kulingana na madaraja hayo. Inawezekanakabisa ubora wa nyumba zatu ukatofautiana katokana na utofauti wa “utoaji wetu” hapaduniani na “hazina zetu” mbinguni.(Nionavyo mimi). Basi nikupe tu ushauri binafsi;Angalia usije ukafika mbinguni, katika jumba la kifahari, lenye kuta na vitasa vyadhahabu, lakini kwa aibu, ukakalia stuli milele. Weka hazina yako mbinguni, kwautoaji mzuri wa sadaka zako. Inalipa! Sadaka zako hazipotei, bali zinawekwa kama‘akiba’ mbinguni. “Msijiwekwee hazina duniani, nondo na kutu viharibipo, na wezi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusiko haribika kitu kwa nondo wala kutu, wala wezi hawavunji wala hawaibi; kwakuwa hazina yako ilipo, ndipoutakuwapo na moyo wako.” (Mathayo 6:19-21) 10
 11. 11. SEHEMU YA PILI AINA ZA MATOLEO. 1 LIMBUKO (Malimbuko): Mith 3:9-10 Limbuko ni zao la kwanza la kazi ya mikono yako. (First Fruits)Mfano:- Kama umefuga kuku 200 wa mayai, mayai 200 ya kwanza, si ya kula wala kuuza, ni ya BWANA. Ndama wa kwanza kuzaliwa ni wa Mungu, mshahara wa kwanza wa ajira yako ni wa Mungu. Mazao ya kwanza ya shamba lako ni ya Bwana. • Kazi ya limbuko, ni kumheshimu Mungu kuwa ndiye chanzo cha baraka zetu na mpaji wa mali zetu. Ukimtambua Mungu hivyo atakubariki zaidi na kukuzidishia. 2. ZAKA ( FUNGU LA KUMI): Walawi 27:30, Malaki 3:7 – 7 - Zaka ni 10% (asilimia kumi) au 1/10 au sehemu moja kati ya kumi ya baraka yoyote aliyokupa Mungu. Mfano - Ukikamua lita 50 za maziwa ya ngo’mbe kwa wiki, basi lita 5 ni zaka ya Mungu. Mshahara wako, ukiugawa katika sehemu kumi, basi sehemu moja, mpe Mungu kama zaka yako kwake. Tena kumbuka kupiga hesabu kutoka kwenye mshahara kamili kabla ya makato. Kumbuka, Mungu anajua hesabu vizuri. Ndio maana anasema “lete zaka kamili nyumbani kwangu” (Malaki 3:10) Kazi ya zaka – ni kufungua madirisha ya mbinguni ili baraka zimiminwe. Zaka haipimi baraka (mavuno) bali inafungua madirisha ya mbinguni ili upimiwe baraka kutoka kwenye matoleo ya sadaka yako baada ya zaka. • Endapo utazidiwa na matumizi, na ikakulazimu kuitumia zaka takatifu ya Mungu, fahamu kwamba, Mungu anakudai. Siku utakapomrudishia, utatakiwa kulipa pamoja na riba, ili zaka yako ikombolewe. 11
 12. 12. • Kukombolewa maana yake ili iwe zaka takatifu tena ni lazima uiongezee 20% au 1/5 (sehemu ya tano )ya hiyo zaka, iwe kama riba, ndipo Mungu ataipokea kuwa ni zaka takatifu ya Bwana. Laa sivyo, zaka yako, si kamili, hivyo si takatifu. Kwahiyo, haitafungua madirisha ya mbinguni. • Mfano- Kama ulimkopa Mungu zaka ya Tshs 10,000/= siku utakapolipa, unatakiwa upeleke na nyongeza ya 20% ya 10,000/= (1/5 ya 10,000/=) ambayo ni Tshs 2,000/=. Hivyo Jumla utamlipa Mungu Tsh. 12,000/= kwa mkopo wa Tsh. 10,000/= ulipotumia zaka ya Mungu. • Mungu aliweka utaratibu wa namna hiyo ili kuwafanya watu wake, wasiiguse zaka yake. Waiheshimu na kuilipa kwa uaminifu.3. DHABIHU (Sadaka ya kawaida) *2Kor 9:6-7 • Sadaka ya dhabihu haina hesabu toka kwa Mungu, bali kila mtoaji, anaamua mwenyewe atoe kiasi gani. Utakavyoamua ndivyo utakavyovuna. Ukitoa kidogo,utavuna au utapimiwa kidogo, ukitoa kwa wingi, utapimiwa vingi. Ni uamuzi wako. (Gal 6:7 – 10) • Kazi ya Dhabihu: Ni kupima kiwango cha mavuno ya baraka, unayotakiwa kumiminiwa kutoka mbinguni baada ya kutoa zaka. ANGALIZO: • Dhabihu itazuiliwa kukushukia, kama madirisha yako ya mbinguni yamefungwa. Hivyo kutoa dhabihu wakati unamwibia Mungu zaka, haitaleta mavuno unayotarajia. Watu wengi wana tatizo hili. Hutoa sana sadaka, lakini hawatoi zaka . Baraka zao huzuiliwa. • Kwahiyo, ili umiminiwe baraka katika mashamba, mifugo, afya, biashara, baraka ya pesa, kufaulu, ulinzi, fungua kwanza madirisha, si maombi, wala si kwa sadaka, bali ni kwa zaka yako. • Baada ya kutoa zaka, dhabihu inaweza kufanya baraka nyingi sana. Baada ya madirisha kufunguka, ndipo dhabihu yako itaamua, upimiwe kiasi gani, kijiko au kikombe au bakuli au sufuria au karai au ndoo au pipa au sim-tank au container. Baada ya zaka, dhabihu ndiyo inaamua apimiwe chem–chemi au kijito au mto au bwawa au ziwa au bahari, ni uamuzi wako. 12
 13. 13. SEHEMU YA TATUKWA NINI TUNATOA LAKINI HATUPOKEI? • Kanuni ya Mungu ni kupokea baada ya kutoa (kupanda na kuvuna). Kuna nyakati tunapanda lakini hatuvuni, Tunatoa lakini hatupokei. Katika hali kama hiyo, tatizo si Mungu, maana “Mungu, si mwanadamu hata aseme uongo” Hesabu 23:19. Bali ni sisi wapandaji/watoaji tunakosea masharti ya kupanda/kutoa. Mungu anasema katika Yakobo 4:3 “Hata mwaomba, wala hampati, kwasababu mwaomba vibaya”. Basi ni lazima na hakika ya kwamba, “tunatoa lakini hatupokei, ni kwasababu tunatoa vibaya” !! Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayotufanya tusipokee japo tunatoa. Kwa nini tunatoa lakini hatupokei? - CHECK LIST - 1. Kumwibia Mungu Zaka. (Mal 3:7-12) • Kutoa sadaka wakati unamwibia Mungu zaka, hakuna faida, kwa sababu madirisha ya mbinguni yamefungwa. Sadaka haitazaa. Sadaka yako italeta mavuno mazuri endapo tu madirisha yako ya mbinguni yamefunguliwa kwa zaka unayotoa. Usimwibie Mungu. Toa zaka kwa uaminifu. Utaanza kuona unapokea mavuno (baraka) katika kipimo cha kujaa na kushindiliwa hata kumwagika. 2. Kutoa sadaka bila imani (Ebr 11:1,6; Ebr 10:38) “Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo” wengi hutoa sadaka lakini hawana uhakika kuwa ile sadaka itazaa mara 30 au mara 60 au mara 100 (Mathayo 13:3,8) Kwa sababu wengi hutoa bila uhakika (imani) sadaka zao haziwi za kupendeza mbele za Mungu. Hivyo hazizai. Kwa sababu hiyo, wanajikuta wanaamini kwamba, ukitoa sadaka, ni kama wamechanga pesa tu, na haitazamiwi kuzaa. Ni kama imepotea. Hayo ni mawazo potofu ambayo shetani amewafanya wengi kuamini hivyo. 13
 14. 14. • Lakini NENO la Mungu linatupa uhakika (imani) kwa kuwa “imani huja kwa kusikia … Neno la Kristo (Rum 10:17). Mtu akiliamini neno la Mungu, kwamba Mungu hawezi kusema uongo, moyo wake utapokea uhakika (imani). Ndani yake, litajengeka taraja la kupokea, kila anapotoa. Atajua kuwa kutoa sadaka si kupoteza, bali ni kupanda kwa ajili ya mavuno (baraka) kutwa zaidi. • Kuanzia sasa, pokea uhakika kwamba, ukitoa kwa imani ya kupokea, utapokea. Ukitoa bila imani ya kupokea, hautapokea, utakuwa umechangia tu . Hivyo mbegu haiwezi kuzaa, kwa maana “….kila tendo isilotoka katika imani, ni dhambi” (Rum 14:23) • Hakuna mkulima anayeweza kutoa kidogo, wakati anaamini mavuno ni mengi. Atoae kidogo hana imani ya kupokea. Anaamini “inapotea”na ndio maana anaona ni bora apoteze kidogo. • Lakini mwenye imani ya kupokea, hutoa kwa wingi kwa sababu anajua sadaka yake haipotei, bali imepandwa na itazaa sana.3. Kutoa sadaka pungufu ya ile uliyoazimia mwanzo au pungufu ya ile aliyokuongoza Mungu kutoa. (Mdo 5:1-11; Mith 21:27) • Ukipanga moyoni mwako kutoka nyumbani, kumpa Mungu kiasi fulani cha sadaka, baada ya azma hiyo, Mungu anakuwa ameipokea sadaka tayari. Wakati wa utoaji, usipunguze. Laa sivyo utakuwa unamwibia Mungu. • Watu wengi hukosea kwa kufika ibadani wakiwa wamepunguza sadaka ya Mungu. Katika sadaka hiyo hiyo ananunua gazeti, pipi, au analipa nauli. Hiyo sadaka si takatifu tena. Kwa sababu umeipunguza. • Panga kutoa sadaka kwa maombi kabisa, uamue kiasi utakachomtolea Mungu na uwe mwaninifu kutokuipunguza, hata iweje. Baadhi ya mikosi itupatayo, ni matokeo ya kumwibia Mungu, kama Anania na Safira . 14
 15. 15. 4. Kutoa sadaka kilema Mal 1:13- 14, Walawi 22:20-25 Sadaka kilema ni ile ambayo hata wewe hauihitaji. Ni zile sadaka tunazotoa ili kupunguza mizigo. Mungu hapokei sadaka “reject” (zilizokataliwa) Kamwe, usitoe mabaki (ya dukani, shambani, nyumbani, n.k.) kuwa sadaka, si heshima! Ni laana mbele za Mungu. Mungu hupokea sadaka nono, sadaka nzuri, sadaka bora. “Mheshimu Mungu kwa matoleo yako” *Mith 3:9 • Kama ulichotoa, ndicho pekee kulikuwa kimebaki, Mungu atakipokea vizuri na machoni pake kitakuwa “kinono” hata kama ni kichache, kichakavu au kilema, kwa sababu ndicho pekee ulichobakiza.5. Kutoa sadaka dhalimu/haramu (Malaki 3:12-13) • Sadaka haramu ni ile iliyopatikana kwa udhalimu, kwa mfano; biashara haramu, dhuluma, rushwa, wizi, uuaji, utapeli, uasi n.k. Wewe ufanyaye mambo ya jinsi hii, ni chukizo mbele za Mungu. Sadaka ya namna hii, haitabarikiwa. Ni haramu. Isa 1:11 –17; Amosi 5:22-27.6. Kutoa sadaka bila upendo wa Kristo ndani yako. (1Kor 13:1-4) • Kama moyo wako unamchukia mtu, jirani, ndugu, au watu wa dhehebu jingine au kabila jingine, haufai kutoa sadaka. Biblia inasema “No profit” (Huna faida) • Kama umekorofishana na mtu, yakupasa kutengeneza uhusiano wenu kwanza, kabla ya kutoa sadaka.(Math 5:23-25) • Utoaji ni ibada kamili. Unatakiwa utoe sadaka bila hila, bila kinyongo, bila chuki, bila hasira wala ugomvi au kwazo juu ya mtu. Moyo wako uwe safi. Kama una neno juu ya mtu, “Ungamaneni dhambi ninyi kwa ninyi mpate kuponywa.” (Yak 5:16) • Upendo wa kweli unaunganishwa na amani ya rohoni (Efe 4:1-3) (Ebr 12:14) Mungu anataka tutafute kwa bidii amani (upendo na umoja) ili tupate na baraka zake maishani. Upendo wa kweli, huleta umoja, ambapo Mungu ameamuru baraka zake. (Zab 133:1-3) 15
 16. 16. 7. Kutoa sadaka ili usifiwe (Math 6:2-4; Mith 21-27) • Maana ya andiko hili, sio sadaka yako kuonekana. Bali ni ile nia ya moyoni. Haimaanishi jirani (mkono) yako akiiona sadaka yako, itakuwa batili. Ila kama uliionyesha au uliitaja ili usifiwe, hapo imekuwa batili. Haitakuja na baraka yoyote.8. Kutoa sadaka mahali ambapo hukutakiwa kutoa (Kumb 12:13-14) • Kila sadaka (mbegu) ina mahali pake maalum pa kutolewa (kupandwa). Kuna mbegu hazioti vizuri Ulaya, Afrika, milimnani, mabondeni, mchangani, pwani, majini, n.k. • Ni muhimu kusikiliza uongozi wa Roho Mtakatifu. Kama sadaka yako Mungu alitaka uitoe kwa yatima, ukiitoa kanisani, utakuwa umekosea. Ni muhimu umuulize Mungu, umsikilize na umtii vizuri. Kuna sadaka za kanisani na za sehemu nyingine nje ya kanisa, kwa mfano; kwa yatima, wajane, masikini, mikutano, semina, safari za watumishi, nyumbani kwa watumishi n.k. • Tazama Math 13:1-9. Tatizo halikuwa kwa mpanzi, wala katika mbegu zake, bali katika “mahali” mbegu hizo zilipoangukia. • Si kila udongo, ni udongo tifu-tifu. Udongo tifu-tifu ni pale mahali Roho anakuongoza kutoa. Mahali ambapo kazi ya Mungu inafanyika vizuri kwa utukufu wa Mungu. Mfano:- *Kanisani / Mikutanoni, (Mdo 4:36) *Wahubiri wa injili (Fil 4:15-20; Gal 6:6). * Kwa Masikini, Yatima, Wajane (Mdo 10:1-4,Isa 1:10-17) • Roho Mtakatifu na akuongoze (Rum 8:14; Yoh 16:13)9. Kutoa sadaka wakati ambapo hukutakiwa kutoa. (Mhu 3:1-2, 6) Kila jambo lina wakati wake. Hata mbegu, hazipandwi kila siku. Zina majira yake ya kupandwa na kuvunwa. Jifunze kutoa sadaka kwa wakati ambao Mungu anakusukuma kutoa. Msukumo wa Mungu ukija kukugusa kutoa sasa, lakini ukaacha kutii, halafu ukaamua kutoa wiki ijayo, si ajabu usipokee mavuno ya sakaka yako. Kuchelewa kutii ni kutokutii (Late obedience is disobedience). Huwezi kujua, pengine dakika ile ya siku ile, sadaka yako hiyo ilihitajika sana mahali Mungu alipokuwa anakuongoza kutoa. Kwa kutokutii kwako, umekwamisha kazi yake na hutaweza kubarikiwa. (Isa 1:19) 16
 17. 17. 10. Kutoa sadaka ili kukubaliwa na Mungu. (Mdo10: 1-6) • Kornelio alidhani Mungu atamhesabia haki kwa wingi wa sadaka na sala zake. Lakini Mungu alimhurumia na akamwonyesha naman sahihi ya kuhesabiwa haki. Yaani wokovu kupitia kwa Yesu Kristo. • Watu wengi wanatumia sadaka kutafuta haki ya Mungu. Sadaka za hivyo, hazileti baraka. Zinafanana na hongo. Huwezi kumhonga Mungu kwa pesa au maombi. Haki ya Mungu inapatikana bure, kwa toba ya kweli na wokovu kupitia Yesu Kristo. (Mdo 10:17-48) (Efe 2:8-9). • Toa sadaka kwa moyo safi, kwa nia ya kumwabudu Mungu na kuisukuma injili mbele. Nawe utabarikiwa sana. • Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, naupendo wa Mungu Baba na Ushirika wa Roho Mtakaktifu, ukae nasi sote, sasa na hata milele, Amina. (2Kor13:14)NI BORA KUTOKUTOA KABISA.Baada ya kujua kuwa Mungu ana kiwango chake cha kuabudiwa kwa namna yautoaji wa sadaka, ni muhimu sana ujue haya mambo ili uone faida na baraka zautoaji wa sadaka. Mambo haya yatakusaidia kujipange vizuri kila mara unapotakakumwabudu Mungu kwa kutoa sadaka.Ni maombi yangu ukweli huu utajenga desturi ya kuji-check, point kwa point, iliusikosee katika utoaji wako. Hii ni kwasababu, Mungu anapenda UTII (wa maagizoyake/Neno lake) kuliko SADAKA; Ndio maana imeandikwa “Jitunze mguu wakouendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili kusikia kuliko kutoasadaka ya wapumbavu; ambao hawajui kuwa wanafanya mabaya” Mhubiri 5:1. 17
 18. 18. NI BARAKA AU LAANA.Kila mara ukamatapo sadaka mkononi, kumbuka kuwa kwa hiyo sadaka, unawezakubarikiwa au kulaaniwa. Sadaka yako ina nguvu ya kukubariki, kama utatoa vizurikwa kufuata maagizo ya Mungu; Lakini pia sadaka hiyo ina nguvu za kukulaani,kama utaitoa kiholela bila kufuata utaratibu wa Mungu. Kwa sadaka hizi hizi, Daudialibarikiwa, lakini kwa sadaka hizi hizi, Anania na Safira walikufa. Sikia Munguanachosema. Zishikeni kwa bidii sheria za Bwana, Mungu wenu, na mashuhudiza yake na amri zake alizokuagiza, Nawe fanya yaliyo sawa na mema machoni kwa Bwana, ili mpate kufanikiwa, nawe upate kuingia na kumiliki nchi nzuri Bwana aliyowaapia Baba zako…Tazama, mbele yako kuna baraka na laana, uzima na mauti, chagua uzima upate kuishi. Kumb 6:17-18 MUNGU WANGU AKUBARIKI SANA. “Lakini kueni katika neema na katika kumjua Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo … Heri wakaao nyumbani mwako Bwana, wakuhimidi Daima … Huendelea toka nguvu hata nguvu …na Kila mwenye pumzi, amsifu Bwana … Mheshimu Bwana kwa mali yako, … ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi” (2Pet 3:1 Zab 84:4-5,7 Mith 3:9-10) Wako katika kazi ya Mungu Mwl. Mgisa Mtebe +255 713 497 654 mgisamtebe@yahoo.com 18

×